24 December 2012
Tusiime aishikiki matokeo ya darasa la saba jijini Dar
Na Mwandishi Wetu
MKOA wa Dar es Salaam umetangaza matokeo ya waliohitimu darasa la saba mwaka huu ambapo shule ya Tusiime ya Tabata jijini Dar es Salaam imeongoza kwa Mkoa wa Dar es Salam.
Shule hiyo ndiyo imekuwa ikiongoza matokeo ya mkoa na wilaya ya Ilala tangu mwaka 2005. Katika matokeo hayo wanafunzi 10 bora wa kike waliofanya vizuri wanatoka shule ya Tusiime kati ya wavulana walioingia 10 bora saba wanatoka shule hiyo.
Akitangaza matokeo hayo juzi Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mbando,aliwataja wanafunzi kumi bora wa kike wanaotoka katika shule ya Tusiime na alama zao kwenye mabano kuwa ni Janeth Kijazi (234), Justina Kalalaa (234, Kellen Mudogo (234), Thecla Ngewe (231), Stella Kagumila (230), Asia Komba (229), Grace Nyondo (226), Praise Bagenda (226), Lisa Magoti (225) na Najima Majid (224) (Tusiime).
Kwa upande wa wavulana 10 bora waliofanya vizuri na alama zao kwenye mabano ni Jimmy Luhomvya (233) Dule Mutagwaba (231), Fray Seyumwe (231) Saad Mussa (229) Gerald Kasamala (229), Oel Mutagwaba (228) na Gift Kilupa (229) ambao wote wanatoka shule ya Tusiime.
Wengine ni Maximillian Machage (229) kutoka Shule ya Msingi Kinondoni,Shaban Kawaia (227) Mtoni Temeke na Alfred Shami wa Shule ya Msingi Mlimani.
Alisema waliofanya mtihani wa kumaliza la saba mwaka huu walikuwa 58,093 na waliofaulu ni 51,433 sawa na asilimia 88.5. Alisema waliochaguliwa kujiunga na shule mbalimbali za sekondari ni 39,681.
Kwa mujibu wa takwimu hizo wanafunzi waliofaulu mitihani ya kumaliza la saba mwaka 2011 walikuwa asilimia 79 wakati mwaka huu ni asilimia 88, hivyo ufaulu umeongezeka kwa asilimia 10.
Akizungumzia matokeo hayo, Ofisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mapunda, alipongeza shule ya Tusiime kwa kufaulisha wanafunzi wengi zaidi na kwa alama za juu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment