01 June 2012

INUKA yawashukia madaktari Pwani



Na Zena Mohamed, Aliyekuwa Bagamoyo

WANACHAMA wa Chama cha Kutoa Mikopo kwa Wanawake Wajasiriamali nchini
(INUKA) wamewaalani madaktari na wauguzi wanaowanyanyasa wazee na
wajawazito katika Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.

Hayo yalisemwa jana mjini humo na Mkurugenzi wa INUKA Bw.David Msuya katika
mkutano wa kujadili vyanzo vya maambukizi ya Virusi vya Ugonjwa wa Ukimwi (VVU) kwa wanafunzi wa shule za sekondari na msingi wilayani hapa.

Mkutano huo uliudhuriwa na wajumbe wa chama hicho ambapo mada
zilizongumziwa ni pamoja na unyanyasaji kazini, huduma kwa wazee na
wajawazito, misaada kwa watoto yatima kutowafikia walengwa na mazingira.

Bw. Msuya alisema huduma za matibabu kwa wazee zimekuwa ngumu
kupatikana hali ambayo imepelekea wazee hao kuelekezwa vituo vingine vya
kupata huduma badala ya Hospitali ya Serikali kama ilivyohaidiwa na serikali.

"Huduma kwa wazee inatakiwa itolewe bure, lakini kwa hapa wazee
wanatozwa fedha na matokeo yake kuilaumu, Serikali kwajili ya mtu mmoja
kutokana na wagonjwa wenyewe kalalamika kimya kimya nakutotoa taarifa
sehemu husika," alisema Bw.Msuya.

Pamoja na hayo aliwaasa wanachama hao kwa kushirikiana na wananchi wengine
kutoa elimu jamii kwa jamii kwa ujumla ili kuweza kutatua matatizo hayo.

No comments:

Post a Comment