28 March 2012

TPAWU yaanza maandalizi ya Mei Mosi

Na David John
KATIBU Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Mashambani na Kilimo (TPAWU) Bw. Kabengwe  Ndebile, amewataka wafanyakazi waliochini ya chama hicho kuandaa bidhaa za kilimo kwa ajili ya kuzionesha wakati wa maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi.
 Alisema maadhimisho hayo ambayo kwa mwaka huu yanatarajiwa kufanyika mkoani Tanga.  Bw. Ndebile alitoa mwito  wafanyakazi kuaza kujiandaa kwa ajili ya kuonesha zana za kilimo na mazao wanayozalisha.

Akizungumza na gazeti hili ofisini kwake Dar es Salaam jana, Bw. Ndebile alisema mwaka huu wanatalajia kutumia sh. milioni 120  kufanikisha sherehe hizo.

"Tumejipanga vema kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa na hasa tunapoelekea kwenye sherehe hizi na ndiyo maana unaona viongozi tunawajibika vilivyo,"alisema Bw. Ndebile

Alisema sh. milioni 120 zitatumika kununua vyakula, mapambo, usafirishaji na kuchapisha fulana.

Alisema wakati wa sherehe hizo watafanya tathmini ya ongezeko la ajira kupitia kilimo na jinsi ya kuboresha maslahi ya wafanyakazi wa mashambani.

Aliongeza kuwa kiwango cha sasa cha mshahara wa  sh. 70,000 wanaolipwa wafanyakazi wa mashambani ni kidogo na hakikidhi mahitaji yao

No comments:

Post a Comment