Na Mwandishi Wetu, Mvomero
MBUNGE wa Jimbo la Mvomero Bw. Amos Makalla ametoa msaada wa jenereta lenye thamani ya sh. milioni 3.5 katika Kijiji cha Lukenge wilayani Mtibwa kwa ajili ya kuwezesha kusukuma maji.
Kutolewa kwa msaada huo wa jenereta ni kilio cha miaka sita toka lilipoharibika jenereta lililokuwa likisukama maji kijijini hapo na kusababbisha uhaba mkubwa wa maji.
Genereta hilo lililoharibika awali lilitolewa na Kiwanda cha Sukari Mtibwa mwaka 2006 na hivyo kusabisha tatizo la hupatikanaji maji safi na salama sambamba na vifo vinaongezeka siku hadi siku vinavyosabishwa na mamba kwa watekaji wa maji mtoni.
Akikabidhi msaada huo Bw. Makalla alisema kuwa akiwa kwenye kampeni mwaka 2010 wananchi walimuomba mara atakapochaguliwa awasaidie kutatua tatizo la maji Kijiji cha Lukenge jambo ambalo jana alilitekeleza.
“Ndugu zangu nimekuja hapa kutekeleza kwa vitendo juu ya kushughulikia tatizo la maji, mliniambia wakati wa uchaguzi niwasaidie leo (jana) nimekuja na jenereta ili lisaidie kutatua tatizo la maji tuondokane na hatari ya kuliwa na mamba mtoni sasa tuyapate maji hapa hapa kijijini,“alisema.
Akimshukuru mbunge kwa msaada wa jenereta Mwenyekiti wa Kijiji cha Lukenge Bw. Nomanus Daniel alisema, msaada alioutoa mbunge ni mkubwa na si wanasiasa wote wana moyo kama wa Bw. Makalla.
"Kiufupi nakushukuru sana leo (jana) umetufuta machozi Mungu akubariki sana ni wachache wenye moyo kama wako,”alisema.
Aidha, aliitaka Halmashauri ya Mvomero kushughulikia miundombinu ikiwemo mabomba yaliyopasuka na vifaa vidogo vidogo ili mradi wa maji utekelezwe kwa haraka na zaidi aliwataka wananchi na uongozi wa kijiji kulinda miundombinu ya maji na jenereta alilokabidhi ili kufanikisha maji kupatikana muda wote kijijini hapo.
Mhe. Makalla umetenda jambo jema kwa wananchi wako,Mungu akubariki na akulinde katika kazi yako ya utumishi mwema katika jimbo lako.Na Mungu ni mwema kila uligusalo kwa mikono yako Mungu aweke baraka.
ReplyDelete