Na Mwandishi Maalumu, Dodoma
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Bw. Zitto Kabwe (Chadema) ameitaka Serikali kutoa kauli ikieleza ni lini itaacha kudharau maagizo ambayo yanatolewa na wabunge wawapo katika vikao vyao.
Kauli hiyo aliitoa jana bungeni alipokuwa akiuliza swali la nyongeza akitaka kujua ni lini Serikali itatoa taaarifa bungeni kama Kamati ya Mashirka ya Umma inayoongozwa na,Bw. Zitto ilivyoangiza baada ya kuagiza Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kufanya ukaguzi katika mashirika mbalimbali.
Alisema baada ya CAG kufanya ukaguzi alibaini kuwa zaidi ya sh. bilioni 18 zililipwa kwa kampuni hewa na sh. bilioni 48 hazikupatikana kutokana na baadhi ya kampuni kukataa kutoa nyaraka.
Alisema kitendo cha kutotoa taarifa hiyo bungeni kama kamati ilivyo agiza inaonesha wazi kuwa Serikali imekuwa na tabia ya kudharau maagizo yanayotolewa bungeni.
Akijibu swali hilo Waziri wa Fedha na Uchumi, Bw. Mstafa Mkulo, alisema si kweli kuwa Serikali inakaidi maagizo ya bunge, bali kinachosubiliwa ni mkaguzi kukamilisha taarifa yake na baada ya kukamilika itawasilishwa bungeni wakati wowote.
Awali katika swali la msingi mbunge wa Shinyanga Mjini, Bw. Stephen Masele (CCM), alitaka kujua ni kwa nini Serikali inashindwa kulipa madeni ambayo inadaiwa na mashirika ambayo yalikuwa yakinunua pamba katika Mikoa ya Mwanza na Shinyanga.
Alitaka kujua ni lini Serikali itamaliza kuwalipa fedha wanunuzi hao ambao wanaendelea kulipa gharama kubwa za mikopo katika mabenki.
Akilitolea ufafanuzi swali hilo Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Bw. Christopher Chiza, alisema kuwa Serikali haidaiwi na shirika lolote ambalo lilikuwa likiusika na ununuzi wa pamba.
Alisema kuwa jumla ya sh. bilioni 9.3 zililipwa na benki kuu kwa kampuni 15 za pamba zilizokidhi vigezo na nyingine 17 hazikulipwa kwani zilikuwa hazijakidhi vigezo.

Ndoa kati ya Serikali na Bunge inaashiria kuvurugika. Juzi Serikali ilikataa kuidhinisha posho za Wabunge. Wabunge nao wameigeuzia Kibao Serikali. Wabunge wala hawajihusishe kikamilifu na tatizo la Mgomo wa Madaktari. Wanangojea hadi Serikali iumbuke. Wabunge wasisahau kuwa Serikali ni ya watu wote na sio yao Itafika pahali Watanzania watawawajibisha Wabunge. Mimi naona ni dalili nzuri ya kuelekea kuvunjika kwa ndoa hii. Taifa litasonga mbele. Mambo ya nikune mgongo nawe unikue yatatokomea. Uwezo na utendaji kazi wa Mihimili hii utaimarika ikiwa Ndoa hii ya UTATU itavunjika. Heshima, usikivu na maelewano yatakuwapo. Bunge liheshimu Serikali na Serikali iliheshimu. Vile vile Mahakama iheshimu Serikali na Bunge kama Mihimili hii inavyo heshimu Mahakama. Inatakiwa Mihimili hii itengane na kuwa independent. Yetu Masikio na macho.
ReplyDelete