09 February 2012
Maige akana kuwafahamu walioua ng'ombe 56
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Bw. Ezekiel Maige, amesema Serikali hajui kama askari wa wanyamapori waliua ng’ombe 56 katika wilaya ya Mpanda mkoani Rukwa.
Kutokana na kutotambua tukio hilo ,Bw. Maige alisema hakuna mpango wowote ndani ya Serikali wa kulipa fidia wafugaji wa eneo hilo kutokana na hasara hiyo, kwani hakuna ushahidi kamili.
Katika swali la msingi, Bi. Anna Mallac (Viti Maalu-Chadema) aliyetaka kujua Serikali inachukua hatua gani kushughulikia kitendo cha askari wa wanyamapori kuua ng’ombe 56 katika vijiji vya Ikiba, Kishishi na Chamaledi Wilayani Mpanda.
Mbunge huyo alitaka Serikali itamke ni lini hasa italipa fidia hiyo kwa wafugaji ambao wamesubiri kwa muda mrefu.
Alisema tuhuma za mauaji ya mifugo ni mojwapo ya mashauri ya jinai ambayo mlalamikaji anatakiwa kupeleka polisi ili uchunguzi wa kina uweze kufanyika kwa ajili ya kubaini ukweli wa jambo hilo .
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment