Mhariri Majira
NIMEPOKEA kwa mshangao na masikitiko makubwa taarifa ya baadhi ya wanafunzi Waislam wanaosoma kidato cha tano na sita ndanda sekondari.
Napenda kutumia nafasi hii, kutoa maoni yangu kama mtanzania huru mwenye haki ya kutoa maoni bila kuvunja sheria na ninaamini kwa kufanya hivi sivunji sheria.
Naomba nizingatie kuwa, nchi yetu haina dini wala dhehebu, watanzania ndio wenye dini na madhehebu,.
Kila mwananchi ana dini yake na ana uhuru wa kuabudu bila kuvunja sheria za nchi na kuingilia uhuru wa mtu mwingine.
Tanzania ina shule na vyuo vinavyomilikiwa na Serikali, watu binafsi na nyingine mashirika ya Dini.
Wapo Watanzania wenye nia njema wanaosoma moja ya shule hizo, wanapoona hazina waalimu wa masomo fulani huwasiliana na wazazi wao ili wawatafutie shule itakayokidhi hitaji lao la kielimu.
Hao ni wale wanafunzi wenye nidhamu na kiu ya kuelimika, inashangaza kusikia baadhi ya wanafunzi wa Ndanda sekondari kugoma kusoma na kufanya fujo wakidai kujengewa msikiti.
Kama mnapenda kusoma dini mbona zipo shule
zinazomilikiwa na dini na zinatoa elimu ya dini? Wasilianeni na wazazi wenu wawahamishie huko.
Mlipokwenda huko mlijua kuwa shule inamilikiwa na serikali na sio ya kufundisha dini. Sasa mnadai msikiti shuleni jueni mna madhehebu tofauti yasiyo abudu pamoja, na wengine wakidai makanisa itakuaje?
Mlikwenda sekondari kusoma masomo yanayotolewa kwa mujibu wa mtaala wa wizara ya elimu, naamini hivyo pale mlipoambiwa mrudi shuleni mkafanye mtihani mkaendela kugoma msingesamehewa kwa kuwa, hamuhitaji kusoma.
Iko haja ya serikali kuhakikisha hampati shule wala chuo chochote maana mkimaliza hamtafanya kazi bali mtaendeleza mgomo.
Albert Sabina
Chikalule, Masasi

Uchochezi mkubwa kwa wanafunzi hawa umekuwa ukifanywa na Radio Iman FM iliyopo Morogoro. Radio hii inatumia chama cha wanafunzi wa kiislam kueneza chuki dhidi ya wakristo na hasa kanisa katoliki. Fuatilia kipindi chao cha mwangaza kwa jamii kila jumapili kuanzia saa 2 asubuhi.
ReplyDeleteKama uchochezi huu utaachiwa kuendelea basi tuendako tutegemee mpasuko mkubwa baina ya waislam na wakristo.