a Mwandishi Wetu, Unguja
MAKAMU wa Kwanza wa Rais kupitia Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, Maalim Seif Sharrif Hamad anatarajiwa kufungua mkutano wa pili juu ya uimarishaji wa siasa na utawala bora Zanzibar leo.
Mkutano huo ambao utakuwa wa siku mbili utafanyika katika mji wa Bwawani Zanzibar, chini ya uratibu wa Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kupitia mpango wake wa Utafiti na Elimu ya Demokrasia Tanzania (REDET).
Mwenyekiti Mwenza wa REDET, Dkt Benson Bana aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Zanzibar ambapo alifafanua kuwa mkutano huo utawashirikisha washiriki wapatao 250 kutoka kada mbalimbali wakiwemo wakulima, wakwezi, viongozi wa dini, asasi za kiraia, vyama vya ushirika, wajasiriamali na wanasiasa.
Alisema, lengo kuu la kufanyika kwa mkutano huo ni uimarishaji wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, ambapo jumla ya mada sita zitawasilishwa katika mkutano huo.
"Ikiwemo misingi ya Katiba ya Serikali hiyo, Serikali ya Kitaifa na masuala ya ushirikishwaji, uendeshaji wa shughuli za Baraza la Wawakilishi, mhimili wa utendaji katika Baraza la Mapinduzi Zanzibar na udumishaji wa imani ya Wazanzibari katika mfumo wa kisiasa," alisema.
No comments:
Post a Comment