07 February 2012

Muhimbili 'kwachafuka'

*Madaktari bingwa nao wagoma, huduma zasimama
*JWTZ wakosa ushirikiano, wauguzi wabaki wapweke
*Wagonjwa: Nasi tutaandamana tukafie wizarani getini
Grace Ndossa na Goodluck Hongo

MGOMO wa madaktari katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), jana ulichukua sura mpya baada ya madaktari bingwa waliokuwa wakiendelea na kazi, kuanza mgomo rasmi ili kuishinikiza Serikali isikilize madai yao haraka.

Leo ni siku ya tatu tangu Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii, ianze kusikiliza madai ya madaktari waliogoma kurudi kazini na kutoa mapendekezo ambayo yatasaidia kumaliza mgogoro uliopo kati yao na Serikali.

Uamuzi wa madaktari bingwa kufanya mgomo huo, ulifikiwa katika kikao cha pamoja ambacho kilifanyika hospitalini hapo na kuanza mgomo rasmi saa nne asubuhi.

Akizungumza kwa niaba ya madaktari hao, Dkt.Catherine Mg'ong'o, ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya madaktari bingwa watano waliochaguliwa wiki iliyopita kwenda kuonana na Waziri Mkuu, Bw.Mizengo Pinda, alisema hawatafanya kazi hadi Serikali itakaposikiliza madai yao.

“Mgomo umeanza rasmi leo (jana), hatutafanya kazi hadi madai yetu yatakaposikilizwa, huduma zitasimama hadi tupate haki yetu kwani Serikali inafanya mzaha,” alisema.

Kutokana na azimio hilo, baadhi ya madaktari hao walionekana wakiingia katika magari yao na kuondoka huku wagonjwa wakiwa wameshika tama.

Mgomo huo ulisababisha hali ya matibabu hospitalini hapo kudorora na kuwaacha madaktari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), wasijue la kufanya.

“Kimsingi madaktari bingwa wametupa ushirikiano mkubwa sasa kutokana na mgomo huu, hatujui nini cha kufanya,” alisikika akisema mmoja wa madaktari wa JWTZ.

Wauguzi nao walisimama katika vikundi wakijadili mgomo huo nyuso zao zikionekana zenye huzuni. Katika wodi mbalimbali, wagonjwa walikuwa wakilalamika huku baadhi yao wakisema ni bora waandamane hadi katika Ofisi za Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ili wakafikishe kilio chao.


“Umefika wakati na sisi tunapaswa kuandamana, ni bora tufie mbele ya jengo la Wizara ijulikane moja kwani umaskini wetu ndiyo unaotutesa,” alisema mgonjwa aliyejitambulisha kwa jina la Bw. Ally Abdallah  anayesumbuliwa na maradhi ya moyo.

Katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI), huduma zilisimama kabisa huku wagonjwa wakiambiwa hakuna matibabu yanayotolewa.

Wakati huo huo, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii, jana iliendelea na vikao vyake jijini Dar es Salaam ikizungumza na wadau mbalimbali kwa lengo la kutafuta suluhu ya madaktari waliogoma.

Wakati hayo yakiendelea, Serikali imeshauriwa kuorodhesha majina ya madaktari wote walioshiriki katika mgomo, kuwachukulia hatua za kinidhamu na kuwafutia leseni zao.

Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC) Ubungo Kibangu, Antony Lusekelo (Mzee wa Upako), aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari.

“Hawa madaktari wanajiona wao ni zaidi ya wengine, wanasahau kuwa watumishi wote wanategemeana katika kazi zao, Muhimbili hali ni mbaya sana, madaktari wamekuwa wakatili zaidi ya wale wanaoua albino (walemavu wa ngozi) kwa kukataa kutoa huduma,” alisema Mchungaji Lusekelo.

Aliipongeza Serikali kwa kutaka suluhu na madaktari hao na kuongeza kuwa kiburi hicho, ndicho kimewafanya wakatae kwenda kuzungumza na Bw.Pinda.

Alisema katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), madaktari wanalipwa dola 10, lakini wanafanya kazi kwa uzalendo mkubwa na kuongeza kuwa inawezekana Serikali ina makosa lakini pamoja na kutaka suluhu, madaktari walikataa.

10 comments:

  1. Ukiona kiongozi wa dini anatoa matamshi yenye kuelemea upande mmoja ujue huyu hatauona ufalme wa mbiguni.Maana Kitabu cha mtume Matahayo chasema heri wapatanishi maana..,yeye angesema naomba niwapatanishe madaktari na serikali angeonekana wa maana.Ni bora angenyamaza na kuongea na wafuasi wake kanisani.anahitaji maombi ya kufunuliwa kupata busara kama za mfalume Sulemani.

    ReplyDelete
  2. mPUMBAVU HUYO lUSEKELO KWANI NANI HAJUI ANAVYOIBIA WATU SADAKA NA HUO U FREEMASON WAKE.HEBU LINGANISHA DKTARI ANA SHIKA UCHAFU KIASI GANI WAKATI ANAHUDUMIA NA ANGALIA MBUNGE AU MTU TRA NA BOT? NIKO NA HASIRA SANA HATA CJUI.WACHA TUFE JK NA WAJINGA WENZAKE WABAKI KWANI TULITAKA WENYEWE KWA KUWACHAGUA CCM.

    ReplyDelete
  3. Tanzania tusikatae imezidiwa na ufisadi mtupu, iweje kwa wabunge wadai posho kila kukicha na kusahau wananchi wengine, Madaktari, Walimu na sekta nyengine wanukata wa hali ya juu jee hamuoni nyie wakuu mnajali nafsi zenu tu kuliko maslahi ya wengi ?

    ReplyDelete
  4. Tatizo kubwa ni kwamba serikali ya CCM inadhani watumishi wenye umuhimu hapa nchini ni Wabunge, TRA, BOT na wanasiasa. Wanasahau kuwa wanafuja fedha tunazolipa kodi.Kada nyingine zimeachwa pembeni kwenye kugawana keki ya taifa. wajifunze. Baada ya sekta ya afya itafuata elimu nayo kugoma. Na huyo mwizi na tapeli wa sadaka za walalahoi (Lusekelo) akae kimya aendelee kuwaibia hao wagonjwa anaowapumbaza. Asidandie mambo ili kujipendekeza kwa serikali. mwisho wake umekaribia!

    ReplyDelete
  5. Lusekelo pambana na matatizo yako na mkeo, ndicho only u can do and not beyond that. Unataka wafukuzwe ili ukawapumbazishe na maombi yako ya kitapeli? Huwezi kutatua matatizo ya jamii, wewe na sehemu ya matatizo.

    ReplyDelete
  6. Honor the physician with the honor due him, according to your need of him, for the Lord created him; 2 for healing comes from the Most High, and he will receive a gift from the king. 3 The skill... of the physician lifts up his head, and in the presence of great men he is admired. 4 The Lord created medicines from the earth, and a sensible man will not despise them. 5 Was not water made sweet with a tree in order that his power might be known? 6 And he gave skill to men that he might be glorified in his marvelous works. 7 By them he heals and takes away pain; 8 the pharmacist makes of them a compound. His works will never be finished; and from him health is upon the face of the earth. 9 My son, when you are sick do not be negligent, but pray to the Lord, and he will heal you. 10 Give up your faults and direct your hands aright, and cleanse your heart from all sin. 11 Offer a sweet-smelling sacrifice, and a memorial portion of fine flour, and pour oil on your offering, as much as you can afford. 12 And give the physician his place, for the Lord created him; let him not leave you, for there is need of him. 13 There is a time when success lies in the hands of physicians, 14 for they too will pray to the Lord that he should grant them success in diagnosis and in healing, for the sake of preserving life. 15 He who sins before his Maker, may he fall into the care of a physician.
    Revised Standard Version of the Bible, copyright 1952 [2nd edition, 1971] by the Division of Christian Education of the National Council of the Churches of Christ in the United States of America. Used by permission. All rights reserved. (Revised Standard Version w/ Apocrypha)
    Study Tools For Ben Sira 38:1-15

    ReplyDelete
  7. NAMSHAURI ASOME Hekima ya Yoshua Bin Sira 38: 1-15

    ReplyDelete
  8. makubwa hivi serikali wenyewe hawaoni hilo nin tatizo kitaifa? wamedharau waalimu na sasa madaktari......wanataka nini hawa au kwasababu wenyewe wanatibiwa nje......?????

    ReplyDelete
  9. lusekelo anaongeo hivo ili watu watoke hosp waende kwake azidi kukusanya sadaka zake za kitapeli.anakusanya malaki,ana dau kubwa kama nini sijawahi kusikia mchungaji anachuma kama yeye.mbona makanisa mengine hayajawahi.madaktari lazima walipwe,ni wa muhimu sana,tusiojua india tufanyeje,hatuna uwezo wa bima ya afya,tuende wapi.jamani inatisha.wanyonge tutaisha.watabaki wakubwa wenyewe maana wao hawafi ngo!

    ReplyDelete
  10. ..A SILENT GENOCIDE IS HAPPENING RIGHT NOW IN TZ

    NCHI HII INA KILA AINA YA RASILIMALI MPAKA URANIUM,BOTSWANA WANACHIMBA ALMASI TU,LAKINI MBONA WANALIPA VIZURI MADAKTARI WAO.

    WATOTO WENGI WA NCHI HII WATAKUFA KWA KUKOSA HUDUMA BORA ZA AFYA,WALE WACHACHE WATAKAO ISHI WATAKOSA ELIMU BORA NA WATAKUMBANA NA MAISHA MAGUMU HIVYO,KUPELEKEA KUPUNGUZA UWEZO WA KUZAA,

    TAFITI ZINAONYESHA NUSU YA WANAUME WA TANZANIA NI WAGUMBA,......KWA MANENEO MENGINE THIS IS A SILENT GENOCIDE,IF WE DONT DO SOME THING, NCHI HII ITAKALIWA NA WAGENI NA WENYE UWEZO...............

    NCHI HII ITAKUWA YA WAJINGA NA WATU WENYE AFYA MBOVU.......HAKIKA UKOLONI UNAKUJA TENA

    ReplyDelete