16 January 2012

Villa-Boas roho kwatu kwa Gary Cahil

LONDON, Uingereza

KOCHA Andre Villas-Boas amefurahishwa kwa kuwasili mlinzi Gary Cahill wakati ambao Chelsea inajianda kumtambulisha rasmi mchezaji huyo waliyemsaini kutoka Bolton.

Cahill alikuwepo katika mchezo wa Jumamosi dhidi ya Sunderland katika Uwanja wa Stamford Bridge,  ambapo Chelsea ilipata bao lake pekee kupitia kwa Frank Lampard ambapo katika saa 24 alitarajiwa kutangazwa rasmi kujiunga na timu hiyo.

Alikwenda London Ijumaa kwa ajili ya kupimwa vipimo baada ya muda mrefu wa kusaka suluhu ya uhamisho wake na Villas-Boas, anatumaini kupata matunda kutokana na mchezaji huyo wa England.

Kocha wa Ureno anaamini kuwa Cahill ataleta mafanikio Chelsea.

Villas Boas aliiambia Sky Sports kwamba ujio wa mchezaji huyo itasaidia kuimarisha safu ya ulinzi.

"Gary ni mchezaji mzuri ana ufundi kwa kucheza sehemu ya ulinzi wa kati, kitu ambacho tunakitaka," alisema na kuongeza kuwa mchezaji huyo wa England ana stamina na anajituma.

No comments:

Post a Comment