Wapiganaji dhidi ya Muammar Gaddafi wakionesha karavati ambalo kiongozi huyo alikuwa amejificha |
UTAWALA wa Kanali Muammar Gaddafi nchini Libya umefikia kikomo jana baada ya kiongozi huyo kuuawa katika mapigano ya
waasi ya miezi minane ya kuuondoa kumwondoa katika madaraka aliyokalia kwa miaka 42.
Gaddafi alikufa kutokana na majeraha aliyoyapata jana katika mapigano hayo, yaliyosababisha kujeruhiwa vibaya katika miguu yake miwili, na kufariki dunia muda mfupi baadaye.
Jinsi alivyouawa
Kwa mujibu wa taarifa za viongozi wa Serikali ya Mpito Libya (NTC), kiongozi huyo alikufa jana baada ya kukamatwa katika mji wa Sirte alikozaliwa. Hata hivyo, habari za kuuawa kwake zilijaa na utata kutokana na kuelezwa mazingira tofauti.
Mmoja wa walioshuhudia mauaji hayo, Bw. Abdel Majid Mlegta ambaye ni mmoja wa maofisa wa ngazi ya juu wa NTC, katika mahojiano na Shirika la Habari la Uingereza (Reuters), alisema kuwa kiongozi huyo alikufa baada ya kupigwa risasi kichwani.
"Gaddafi alipigwa risasi kichwani," Bw. Mlegta alisema na kuongeza kuwa kulikuwepo na mashambulizi makali dhidi ya wafuasi wake.
Bw. Mlegta aliiambia Reuters kwamba mbali na kupigwa kichwani, Kanali Gaddafi, alikamatwa baada ya kujeruhiwa miguu yote miwili, wakati akijaribu kukimbia na msafara ambao ulishambuliwa na ndege za NATO.
Mauji hayo ambayo yalikuja baada ya kukamatwa, ni miongoni mwa mapinduzi makubwa zaidi katika ukanda wa nchi za Kiarabu ambayo yalizing'oa tawala za Misri na Tunisia na kutishia usalama wa viongozi wa Syria na Yemen.
Mkuu wa majeshi auawa
Kamanda wa Brigedia ya 11, Bw. Abdul Hakim Al Jalil, alisema kuwa Mkuu wa majeshi ya Kanali Gaddafi, Bw. Abu Bakr Younus Jabr naye aliuawa, na alishuhudia mwili wake.
Pia, Ofisa mwingine wa NTC, alisema kuwa pia Bw. Moussa Ibrahim, msemaji wa Bw. Gaddafi, alikamatwa karibu na mji wa Sirte, alikouawa bosi wake.
"Moussa Ibrahim, vilevile amekamatwa na wote wamepelekwa chumba cha upasuaji," aliongeza.
Hata hivyo, awali Bw. Jamal abu-Shaalah, ambaye ni kamanda mkuu wa NTC, aliiambia Al Jazeera, kwamba Kanali Gaddafi alikuwa amekamatwa, lakini haikuwa ikifahamiki wazi kama yupo hai ama amekufa, lakini alionekana akipumua.
Taarifa hizo zimekuja muda mfupi baada ya wapiganaji wa baraza la NTC,kudaia kukuuteka mji wa alikozaliwa kiongozi huyo Sirte,baada ya wiki moja ya mapigano.
Taarifa zenye utata
Baada ta shambulio hilo taarifa za akila aina zilianza kusambaa, ambapo mmija wa wapiganai vijana, Bw. Mohammed (20) ambaye alikutwa akiwa amevaa kofia yenye maandishi yaliyosomeka New York Yankees, alisema kuwa Kanali Gaddafi alikutwa akiwa amejificha kwenye shimo ardhini.
Aliliambia Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) kuwa kiongozi huyo wa zamani, baada ya kukamatwa aliwaeleza wapiganaji wasimpige risasi.
Mpiganaji huyo wa waasi alisema kuwa baada ya kujeruhiwa alisafirishwa kwa gari la wagonjwa hadi katika mji wa Misrata.
"Alichukuliwa na gari la wagonjwa," alisema mpiganaji huyo. "Allah akbar" (Mungu ni mkubwa), alisema mpiganaji huyo huku akirusha risasi hewani.
Sherehe Tripoli
Mwandishi wa BBC, mjini Tripoli, Bi. Caroline Hawley, alisema kuwa baada ya kupata taarifa hizo, milio ya meli na magali ilisikika katika mji huo huku milio ya risasi ikisikika hewani na watu wakishangilia.
"Hakuna vikosi vya Gaddafi tena," Kanali Yunus al-Abdali, aliiambia Reuters. "Kwa sasa tunawafukuza wapiganaji wake ambao wanajaribu kukimbia," aliongeza.
Namuombea kwa Mwenyeezi Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi Amiin.Kila jambo lina mwisho wake na huu ndio mwisho wake na hakuna mwenye maovu bila kuwa na mazuri na mema,tutamuenzi, tutamkumbuka na Walibya watamkumbuka pia na hata hao wanaodai wameikomboa Libya!! nao watakuja hukumiwa kwa maovu yao, hawako saafi kama watu wanavyoona.Tuwaombee isije ikawa kama Somalia,Afghanistan au Iraq
ReplyDeleteNakupongeza sana uliyetoa maoni yako kuhusu kuuawa kwa Kanali Mummar Ghaddafi, hakika hakuna asiye mwema na vilevile hakuna asiye na makosa hivyo kumhukumu Kanali kwa makosa peke yake si kumtendea haki kwa Mwenyezi Mungu yote tumwachie Mungu na tumwombe aiweke roho yake mahala pema peponi. Aamin.
ReplyDeleteInalilahi wainal ilaihi raajun - Amin! Bado Mugabe na Museveni on list!
ReplyDeleteThe hero has fallen like Mkwawa did. We shall never forget you after successfully had safeguarded Libyan people resources. In Africa only Mugabe remains.America wants leaders who can go bow reguesting for small things like mosquito nets.
ReplyDeleteGhadafi ni shujaa wa Afrika tutamuenzi tutamkumbuka kwa kuisaidia Afrika na waafrika kwa ujumla na kutaka afirka iwe moja sitegemei kama kutajitokeza kiongozi wa kutaka Afrika iwe moja kama marehemu huyu.
ReplyDeletesisi sote ni wa Mwenyezi Mungu na kwake lazima turejee.
Huu ni wakati muhimu kwa viongozi wa kiafrika kujifunza. Urais si wa familia na ukitaka kuufanya wa familia matokeo yake ni kutoa maamuzi yasiyo sahihi na udikteta. Vile vile kusababisha maafa makubwa kwa wanafamilia. Gadafi amekwenda na familia yake karibu yote na waliobaki wanatafutwa hii hatari. Kung'ang'ania madaraka kwa muda mrefu matokeo yake huwa ni kuangushwa kwa nguvu(mapinduzi). pamoja na uzuri wake wote mpiganaji Gadaffi alichokwa na wananchi anaowaongoza. Au IWAOMBE Mugabe na Mseveni waondoke haraka kabla hayajawakuta ya muhamed Gadaffi. CCM na nyinyi mjifunze.
ReplyDeletehakuna hasara yoyote alioipata kanali kwa sababu,kufa ni kitu cha kawaida na hakuna atakae ishi milele, lazima mtu ufikilie wapi tunaelekea, kama ulizaliwa basi jua utakufa tu, na wala sioni sababu ya kushangilia kifo cha mwingine wakati hatma yetu bado hatuijui, jiulize je yangu mimi na ww ni lini? na tumemfanyia mazuri magapi mungu? niko tayari hata akiniitaji sasa hivi? tujiulize kwanza kabla hatujashangilia kifo cha mwenzetu, mungu atufanyie wepesi duniani na kesho akhera. mungu ailaze roho ya gadafi mahali pema peponi amin
ReplyDeleteSiyo huyo tu kuna viongozi amabao wameng'ang'ania madaraka kwa muda mrefu angalia Museveni yeye amaifanya Uganda kama nchi yake na familia yake angalia nachokifanya Prof. Bingu wa Mutharika amethubut hata kuwateua mkewe na kaka yake kuwa mawaziri wa serikali yake,lakini watu wamemsahau Eduardo dos Santos wa Angola amekuwa madarakani tangu 1978 baada ya kifo cha aliyekuwa Rais wa kwanza wa nchi hiyo Agustino Neto,Mugabe nae anataka kufia madarakani CCM nayo inapaswa ijifunze mwenzako akinyolewa wewe unapaswa kutia maji.
ReplyDeleteGaddafi aliishi kwa upanga (tangia mapinduzi na utawala wake). Amekufa kwa Upanga, what goes around comes around.
ReplyDeleteThis should be a lesson to other African dictators!
NTC HAWAKUWA NA HAKI YA KUMUUA GADHAFI
ReplyDeleteHUKUMU WANGEIACHA MIKONONI MWA MAHAKAMA ZILIZO HURU.
PIA NI FUNZO KWA 'MAKANJANJA' WA UTAWALA KATIKA AFRIKA YETU HII.HATA HAPO TANZANIA KWETU WATAWALA NDANI YA CCM DHAHIRI WAMEUGEUZA UONGOZI WA NCHI KUWA WA FAMILIA ZAO KWA NAMNA WANAVYOJITAHIDI KUWARITHISHA WATOTO WAO NAFASI ZA UONGOZI CHAMANI NA SERIKALINI NA MIFANO NI DHAHIRI
TUNAPOSEMA SI VIZURI KUMUHUKUMU MTU INANISHANGAZA SANA KWANI SS WATANZANIA TUNAWAHUKUMU NDUGU ZETU VIJANA WTU KWA KUWACHOMA MOTO HIVI HII SIO HUKUMU AU KWA HAPA KWETU JAMBO HILI LIMEALALISHWA,
ReplyDeleteTUNAMSIKITIKIA GADHAF KWA KIFO CHAKE LAKINI SIO KUTOLEWA MADARAKANI KWANI KAMA NI KIONGOZI ALIYEFAA ASINGEWEZA KUNG'ANG'ANIA MADARAKA HADI WAKATI WA MAPINDUZI YA KIJESHI CHINI YA NTC ANAAMURU WANAWAKE NA KINA DADA KUBAKWA NA WATU WENGINE HASA WATOTO WADOGO KUWEKWA JUU YA MAGARI YA MAJESHI YAKE WAWE KAMA NGAO NA KAMA NI KUSHAMBULIWA WAUWAWE WAO HUO SI UBINADAMU, NDIO SABABU KIFO CHAKE KUNAWAFURAHISHA WATU WENGI. ILA TU, TUSIKITIKE KATUTOKA BINADAMU MWENZETU NA PIA NI WAJIBU WA MWENYEZI MUNGU KUMUITA KILA MMOJA WETU ANAPOMUHITAJI. KAZI YAKE HAINA MAKONA JAPO NI KWA MKONO WA MWANADAMU. MUAMAR GADHAFF APUMZIKE KWA AMANI ATAKOPANGIWA NA MWENYEZI MUNGU AMINA.
ReplyDeleteHUWA TUNAJIFUNZA KUTOKANA NA MAKOSA.HIVYO VIONGOZI WAJIANGALIE KWA MAKIN.HEBU JIULIZE LICHA YA UBAYA NI MANGAPI GADAFI KAIFANYIA LIBYA?LAKINI ONA HATIMA YAKE.JIULIZE SASA KWA TZ MIAKA 50 TANGU UHURU MAJI HAKUNA UMEME HAKUNA,JE?TUTAFIKA?RASILIMALI NYINGI LAKINI BADO MASIKIN.VIONGOZI KUTUKUZA WAZUNGU,WATAALAM NA WASOMI WENGI LAKINI HAWATHAMINIWI.JAPO ITACHUKUA MUDA LAKIN IPO SIKU ITABAKI HISTORIA YA CCM.MUNGU AMLAZE PEMA AMEN
ReplyDeleteSikupenda kuuawa kwake. Maadamu alikamatwa akiwa hai sikuona sababu kwa nini hakusimamishwa kizimbani kujibu tuhuma dhidi yake kama wanavyomtuhumu. Ingeijengea serikali ya mpito sifa kwa kujali utawala wa sheria.Kutokana na kitendo cha kumuua inaonesha dhahiri hawakuwa na cha kumshitaki nacho!Maana kama kiu yao ilikuwa ni kumuua wangemtia hatiani mahakamani kisha wamuue kama ilivyokuwa kwa Saddam Husein
ReplyDeletekila binadamu ni mkosaji si vema sana kumhukumu Gadafi! alipaswa kusikilizwa jamani,
ReplyDeleteGadafi ameua wengi bila huruma wala kujali haki. Hivyo kumwonea huruma ni upuuzi mtupu
ReplyDeletewatanzania tumejaa unafiki sijui tunapenda nini! na tunachukia nini! si ndio huyo aliungana na amin kutuua?atakaaje madarakani miaka 42 yeye nani?kaua wangapi ? sikitikeni maisha ya bongo magumu uchumi unazidi kushuku.ni jana tu ndugu zetu Dom wanatupiwa na risasi.CCm imewabana mbavu.huyo chizi gaddafi hakuwa mzalendo wala nini?hiyo afrika aaliyotaka iungane angeongaza nani?dictator.wote tutakufa ndio but he deserved that i think took to long to finish him.we believe in freedom of choice,speech,and safety .tuache unafiki people.tuwaache wa libya wachugue mtu wanaye mtaka but not one stupid monkey controlling every one for 42yrs
ReplyDeleteWATANZANIA NI WATU WA KUJIPENDEKEZA SANA TUNAJIFANYA KUMLILIA GADDAFI MNAFAHAMU MADHAMBI YAKE KWANI WALIBYA NI WAJINGA KUMKATAA KIONGOZI ANAYE WALETEA NEEMA,ACHENI UNAFIKI NHATA MSIPO WATAMBUA WAASI HAMNA LA KUWASAIDIA WALIBYA
ReplyDeleteni kweli watanzania wanafiki tena mno u njua bwana mzee gadafi aliwasidia pesa ya uchaguzi ndio mana waziri mzima membe anaongea hadharani kumtetea gadafi kweli tumeishiwa sera ya kwetu yanatushinda unaangalia ya mwenzio na bado viongozi wa afrika mjifunnze sana kwanza waliomua ni waarabui wenzie nyie kinawawasha nini je mnaridhika na vitendo vinavyofanyika srya watu eleweni dunia imebadilika hata nyie viongozi wetu msipokuwa wema mnawatakia watoto wenu mtakaowaacha duniani watateseka sana na dhambi zenu watanzania acheni unafiki kabisa tena mkubwa ndio huyo membe anataka uraisi 20015 hatapata tumeshamwona hana upeo wa mbali ni kibaraka huyo gadafi wala hakuwa mzalendo mngejua vitendo vibaya alivyofanya sijui nadhani pia kitu kingine habari nyingi watanzania zinawapita hamwoni sababu ya tatizo la umeme hivyo kama hujui ulimwengu unakwendaje kaaa kimya n atutaendelea kuteseka wenzio hao viongozi waliletewa masanduku ya pesa ya uchaguzi bwana nyie vipi watanzania kumbuka wakati wa vita vya amini alileta majeshi yake kwetu labda yangeuwa familia yako yote pamoja na mkeo na watoto sidhani kama leo membe angeongea hizo pumba mdomoni kwake hafai huyo membe tena shetani huyo inawezekana ni alkaida wa tanzania
ReplyDeletetena usemayo ngd mtanzania ni kweli tena huyo membe aije akajitokeza hadharani ktegemea uraisi kwa kauli zake hizi tumemaind hana sifa hata ya kuwa diplomasia anaongea pumba pumba kwanza sisi watanzania tusipowatambua hao waasi wana shida gani na sisi na wewe membe ulikuwa wapi kwenda kumbebembeleza gadafi aje aishi kwako usiwe mnafiki bwana tunakushangaa usomi wako mwisho hapo jamani aibu watanzania acheni unafiki jamani haswa wewe membe
ReplyDeleteWaziri Membe wala hajakosea hata kidogo. Ningependa mjiulize ninyi mnaomkashifu Membe. Kati ya Wazir Membe na ninyi na amesoma zaidi?, Pia nani amekaa serikalini zaidi na nani anayejua siri za serikali zaidi.Msiwe mnaropoka tuuu alafu ukija kufuatilia kumbe hata huyo Membe hamumjui. Kuhusu Gadafi kuleta askari wake kwa Amin ili watuangamize ilikua ni sawa tu kutokana na ujinga wa baba yenu wa taifa. Mnavyojua ninyi basi kwamba vita ya TZ na Uganda ni suala la mipaka!! Si hivyo basi niwachane live leo. "Kuna mambo baba yenu wa taifa aliyafanya kwa baadhi ya watu humu TZ, suala ambalo Gadafi na Amini(Mtu na shemeji yake) ambao ni wapenda amani na haki liliwachukiza ndio maana wakaamua kufanya hivyo. Mmwzugwa na mambo ya mpaka ndo maana mnamwona Gadafi mbaya. Mwenzenu Mh.Membe anayajua na anapenda haki ndo maana yupo upande wa Gadafi. Someni historia ya TZ kiundani ndugu zangu mtaelewa tu,msipelekwepelekwe.
ReplyDeletehivi wewe ngd ni mtanzania au mkimbizi sijui unaongea nini leo hii unadiriki kusema baba wa taifa nyerere ni mjinga sikuelewi hata kidogo jamani leo hii nyerere anaitwa mjinga kweli hii comenti lazima nimrushie makongoro na familia yake aibu wewe mtanzania sijui unatoka wapi nadhani wewe ni alkaidas wa bongo yetu haya bwana endelea
ReplyDeleteDah tumshkuru Mungu but alikua gaidi sana so God decided to suspend him may his soul be fairly judged
ReplyDeleteJamani Membe ni mwanasiasa kama wengine, na kawaida yao wengi si wakweli. Halafu Membe ni Ex-shushushu ambae amekulia kwenye system ya unafiki na uongo. Kwa hiyo nadhani ni vyema tumuelewe halafu tumdharau na mizaha yake.
ReplyDeleteMimi binafsi nimekuwa nafuatilia sana malumbano ya Membe kwenye luninga na nimekuja ku-establish kuwa ni mtu mjanja mjanja asiyekuwa na substance kichwani. I think he happens to be a self opiniated person with a lowest level of thinking capacity. Most of his arguments are based on a lowest denominator point! Nashangaa hata huyo JK aliyemteua kwenye huo uwaziri? I think he is also problematic. Ndio maana kuna dalili za wazi kuwa nchi imemshinda kutawala!
KUNA JITU ZEZETA KWELI HATUZUNGUMZII NYERERE HAPA PUMBUFU.MEMBE AMESOMA OR MAEMBE AMESOMA SO STUPID COMMENT EVER HAPPEN.KAMA KASOMEA DEGREE YA KUOKOTA MAEMBE LAZIMA AWE CHIZI.SO FAR WHO CARE ABOUT HIS EDUCATION ?AND HOW MUCH IS HELPING OUR SOCIETY ? KUMSIFIA GADDAFI NA AMINI NI UJUHA .HATUTAKI KUJUA CHANZO CHA AMINI TUNACHOJUA NYERERE KATUSAVE LIFE HUO UJINGA MWINGINE KAA NAO MWENYEWE.TATIZO MNASOMEA PRIMARY MBOZI,SECONDAR YOTE MBOZI CHUO TUMAINI MBEYA NA WEWE NA HUYO MAEMBE WAKO MNAJIDAI MMESOMA HIVYO.TEMBEA DUNIAN UONE WATU TUMETEMBEA DOGO NI MWENDO WAKUBADILSHA NDEGE SOUTH TO NORTH WEST TO EAST EVERY TIME TUNAIJUA DUNIA WEE KAA SUBIRIA UMEME WA MGAO HUO WENZIO TWALA LIFE DUNIANI.PUMBUFU USIMSEME NYERERE TENA .WE LOVE HIM NO MATTER WHAT PEOPLE SAY.
ReplyDeleteIdiot!
ReplyDeletehuyo anayemsema nyerere ana harufu ya al-shabab.
ReplyDeleteHata Tanzania viongozi na chama chao wanaong'ang'ania uongozi kiama hakipo mbali juu yao,maana Polisi na wafuasi wa ccm wakubwa watanguka muda si mwingi tumechoka na ccm,tuwape CHADEMA waongoze.
ReplyDeletendugu wa tz ilo nalo neno couz yasijekutukutaa kama yaliyotokea libya kwa kuogopa kuwachana live hawa ccm wanaotaka kufia ikulu next time watoke tawaweke chadema.pia tusisahau kumuombea zittokabwe apone haraka na kurejea home salama
ReplyDeletekwa watu wasio na akili huwa wanakimbilia kuhoji mabaya ya mtu yale mazuri wanayapuuza.gaddafi kafanya mambo mangapi mazuri Afrika mpaka asisifiwe.ok yeye mwadai kaua wengi na hao NATO wameua wachache si ndio.kuweni waelewa na msiwe wakurupukaji .ok fine kamsaidia uganda kuipiga TZ kwani uingereza si ilimsaidia Tz kuipiga Uganda.
ReplyDeletejamani muacheni baba yetu nyerere apumzike, kwa amani. hakuna mwingine tena kama nyenyere,ila Baba wa mbinguni.
ReplyDeletejamani tumechoka kutawaliwa na ccm, hicho chama kilikuwa kizuri enzi za BABA YETU NYERERE: sasa hakitufai tena, watanzania tumeshakikinai chama hicho.
ReplyDeletematatizo ya umeme, tatizo la mabarabara hasa za vijijini, watu wa libya achaneni nao jamani tuwaze ya kwetu. libya ahijawahi kuwa na tatizo la umeme kama tanzania, kinatuuma sana.
ni kweli tuwaze ya kwetu na kuyatafutia ufumbuzi, tanzania kuna rasili mali nyingi wala tusingekuwa na haja ya kwenda kuomba misaada kwa wenzetu, Mlima kilimanjaro, mbuga za wanyama, migodo ya kuchimba madini, mashamba ya kulimo, wasomi ni wengi , ukiangalia kodi ni za juu, mijihela yooooooooooooote hiyo hatujui huwa zinafanyaga nini, jamani tujifikirie, na pia tusaidiane mawazo, tusiishie kuyaongelea ya walibya. ya walibya waachieni.
ReplyDeletehakuna marefu yasiyokua na ncha mungu ailaze roho ya marehemu gaddafi mahala pema peponi ameni utakumbukwa kwa mema yote uliyo fanya libya ila naamini mungu ndio muweza wa kila kitu wewe umetangulia nasi tunakuja
ReplyDelete