16 January 2012

Ferguson akoshwa na Scholes

LONDON, Uingereza

KOCHA Alex Ferguson amempongeza mchezaji mkongwe Paul Scholes aliyemrejesha katika kikosi cha Manchester United kwa kucheza vizuri na kufunga bao la kwanza katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Bolton juzi.

Mchezaji huyo mwenye miaka 37 alifunga bao la kwanza ikiwa ni wiki moja tangu arejee uwanjani baada ya kutangaza kustaafu soka baada ya kuisha msimu uliopita.

Kwa mujibu wa The Sun, hilo lilikuwa ni ni bao la 151 kwa Scholes katika timu ya United, lilikuwa ni bao zuri, awali kocha alimpatia maelekezo ya kukaa zaidi katika sehemu ya kiungo cha ulinzi.

Kocha wa United  alisema: "Ilikuwa ni kitu cha kushangaza kumwona akiwa mbele.

"Katika umri wake na kwa kuzingatia ukweli kuwa alikuwa amerejea muda mfupi tulitarajia angekaa sehemu ya katikati ya kiungo,  kitu ambacho alifanya pia.

Alimsifu mchezaji huyo kuwa ni mzuri na alionesha hilo katika mechi ya Jumamosi na kueleza kuwa ni mmoja kati ya wachezaji wazuri zaidi wa United.

United ilikuwa imebanwa hadi pale Scholes alipofunga bao muda mfupi kabla ya mapumziko huku Wayne Rooney akikosa penalti.

Zat Knight alimchezea faulo Danny Welbeck kwenye eneo la hatari na kuonesha kadi ya njano kitu ambazo Fergie alikilalamikia.

 Vincent Kompany wa City alitolewa wiki iliyopita kwa kwa kucheza rafu ya miguu miwili, lakini  Glen Johnson wa Liverpool alicheza rafu kama hiyo na kisha Joleon Lescott siku tatu baadaye lakini hawakuadhibiwa.

Alisema baadhi ya waamuzi wamekuwa hawafuati sheria katika kutoa maamuzi yao.

Fergie  alisema kuwa Welbeck alitolewa kwa kuwa aliumia enka lakini atakuwa fiti wakati wa mchezo dhidi ya Arsenal kwenye uwanja wa Emirates Jumapili.

Kocha wa Bolton, Owen Coyle naye alisifu bao lililofungwa na Scholes.

No comments:

Post a Comment