16 January 2012

Kocha Zambia atamba kuwa na kikosi kizuri

LUSAKA,Zambia

KOCHA wa timu ya Taifa ya Zambia, Herve Renard, amesema kuwa uwezo wa kikosi chake hauwezi kupimwa kwa matokeo ya sare ya bao  1-1 dhidi ya Afrika Kusini katika mtanange uliofanyika Jumatano mjini Johannesburg.

Renard  alisema watu wanapaswa kuwa na matumaini makubwa na timu hiyo katika fanaili za Kombe la Mataifa ya Afrika  zitakazofanyika Jumamosi ijayo katika nchi za Guinea ya Ikweta na Gabon.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Daily Mail ya Zambia, ilisema kwamba Balozi wa Zambia mjini Pretoria, Patson Chilemba,  alieleza kuwa raia wa nchi hiyo watashuhudia  Chipolopolo tofauti wakati fainali hizo zitakapoanza kutimua vumbi.

"Wakati sisi tunafanya maandalizi ya timu kwa muda wa wiki tatu, baada ya wiki mbili sisi hatukuwa tayari," alisema.

Renard alisema morali waliokuwa nao wachezaji wakati wakicheza dhidi ya Bafana Bafana na timu B ulikuwa tofauti kutokana na kwamba wachezaji wengi walihofia kuumia.

Katika hatua nyingine, Mganga Mkuu wa timu hiyo, Joseph Kabungo,alisema majeraha yanayomkabili beki wa timu hiyo, Stopilla Sunzu, siyo mabaya kiasi cha kumfanya akose fainali hizo.

Kwa sasa mchezaji huyo anakabiliwa na matatizo ya nyama za paja hali ambayo inatia hofu kuwa huenda akaikosa michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment