25 January 2012

Vijana 1600 kupata ajira Namtumbo

Na Muhidini Amri
Ruvuma

KAMPUNI inayojishughulisha na uchimbaji wa madini ya Uran ya Mantra Tanzania Ltd iliyopo Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma  imesema itatoa ajira kwa vijana 1600 kutoka vijiji mbalimbali baada ya kupatiwa kibali cha kuanza kazi ya uchimbaji.


Hayo yamebainishwa hivi karibuni na Mjeolojia Mkuu   kampuni hiyo Bw. Emanuel Nyamsika wakati alipokuwa akitoa taarifa mbalimbali kwa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Ruvuma chini ya mwenyekiti wake Mkuu wa Mkoa huo Bw.Said Mwambungu waliotembelea eneo la mgodi wa madini hayo kwa lengo la kujiridhisha baada ya kupata malalamiko kutoka vijijini vilivyo jirani mgodi huo.


Alisema,licha ya kutoa ajira hizo kwa vijana,kampuni hiyo imeshaanza kutekeleza kwa vitendo agizo la serikali ya awamu ya nne kwa kuwahamisha wakazi wa vijiji jirani na mgodi huo kuanzisha vikundi vya kiuchumi na tayari imeshaanza kutoa fedha za
kuwawezesha wanavikundi hao kuifanya shughuli za maendeleo kama ufugaji wa kuku wa mayai na nyama.

Alisema,lengo la kufanya hivyo ni kutaka wananchi hao kunufaika na uwepo wa mgodi huo na pia kuunga mkono juhudi za serikali.

Alisema, mpaka sasa bado wanaendelea na kazi ya utafiti kwa eneo lote lilokusudiwa ambalo ni km za mraba 332,lakini wameshindwa kufanya utafiti wao kwa
eneo lote ilo kwa sasa na kufanikiwa kufanya utafiti wao kwa km za mraba 100.

"Tunategemea kuendelea na utafiti katika maeneo yaliyobaki baada ya kupata kibali cha kazi ya
uchimbaji,lengo letu ni kutaka kuyafikia maeneo yote ya mradi huu,hata kuongeza ukubwa wa eneo kwani tunaamini pori ili lina hazina kubwa ya madini ya
Uran,"alisema,

Pia ameiomba serikali,kusaidia upatikaji wa kibali cha uchimbaji ili waanze kutekeleza baadhi ya mipango yake ikiwemo ya ujenzi wa nyumba za watumishi katika
vijiji jirani na eneo la mgodi kwakuwa hairuhusiwi mtumshi kuishi kambini na familia yake.

Akizungumzia kuhusu uharibifu wa mazingira, Bw.Nyamsika aliwatoa shaka wajumbe wa kamati ya ulinzi na kusema kuwa watakuwa na utaratibu wa kufukia mashimo hayo ,na kupanda nyasi na baadhi ya mimea itakayosaidia kurudisha maeneo hayo katika hali yake ya
kawaida.

No comments:

Post a Comment