25 January 2012

Uchumi kwa waathirika wa vipodozi kushuka

                           
Na Esther Macha,
Mbeya

MKURUGENZI Mkuu Mamlaka ya chakula na dawa nchini (TFDA )Kanda ya Nyanda za Juu  Kusini na Bw.Paul Sonda amesema  mbali na  athari za matumizi ya vipodozi vilivyopigwa marufuku kuna hatari ya uchumi kushuka kwa waathirika kutokana na gharama kubwa za matibabu
na wengine kupoteza maisha.


Alisema kuwa pia kuna hatari wengine kupata ulemavu wa maisha kwani hatua hiyo imekuja baada ya utafiti kuonesha bado baadhi ya wafanyabiashara wanavipitisha kwa njia ya panya.


Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi huyo katika Mkutano Mkuu wa Madaktari wa Hospitali na Zahanati binafsi uliofanyika jiji hapa.

Bw.Sonda alisema kuwa watu wanaotumia vipodozi hivyo wanahatari kubwa ya kukumbwa na magonjwa ya kupoteza fahamu, kansa ya damu, kansa ya ini, ubongo, pia kwa akina mama wajawazito kujifungua watoto wenye
mtindio wa ubongo, muwasho mwilini na kunenepa kupita kiasi.
Hata hivyo Bw.Sonda amesikitishwa na kitendo cha wakazi  wa Songwe ambapo vipodozi hivyo viliteketezwa baada ya kuchukua masalia ya vipodozi hivyo na kuvitumia.

Hivi karibuni Mamlaka ya Chakula na Dawa kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato nchini waliteketeza vipodozi vyenye thamani ya sh.mil.129.






 

No comments:

Post a Comment