16 January 2012

Ndoa ya Kobe Bryant hatarini kusambaratika

NEW York Marekani
MCHEZAJI nyota wa mpira wa kikapu, Kobe Bryant na mkewe Vanessa wako mbioni kutengana.

Hiyo imetokana na baada ya kutambulika kuwa Kobe tayari amefanya taratibu kuandikisha nyumba mbili kwa jina la mkewe ambaye atatengana naye siku zijazo.

Mtandao unaooandika habari za wasanii nyota Hollywood, umefanya uchunguzi na kugundua kuwa Januari 5, Kobe aliachia nyumba mbili kwa Vanessa na pia katika siku hiyo Vanessa aliamua kuiachia nyumba ya tatu kwa Kobe.

Chanzo kimesema kuwa sasa  Vanessa ni mmiliki wa nyumba ambayo alikuwa akiishi na  Kobe  iliyo Newport Coast huku nyumba ya pili ambayo ataimilimili  jumla ni ya karibu ambayo alikuwa akiishi mama yake.

Awali mtanda wa TMZ  uliandika stori Desemba 16 kuwa Vanessa amefungua mashitaka akidai talaka kutoka kwa Kobe.

Ingawa kulikuwa na habari kuhusu kuwepo hali ya kumaliza tofauti zao, lakini hali ya kugawana mali iliyoaonekana imeonesha kuwa talaka iko karibuni kati yao.

Mwakilishi wa Kobe, Michael Sitrick,  alisema kuwa hana cha kueleza kuhusu jambo hilo.

No comments:

Post a Comment