25 November 2011

Waislamu Dar waihadharisha serikali tishio la Al-Shaabab

Na David John

KAMATI ya Kutetea Haki za Waislamu nchini, imeihadharisha Serikali kutojihusisha na mambo ya kidini hasa yanayohusu kundi la Al-shaabab kwa shinikizo la mataifa
makubwa.

Katibu wa kamati hiyo, Shekhe Ponda Issa Ponda, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Alisema kamati hiyo imemwandikia barua Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Shamsi Vuai Nahodha, kupinga kauli yake aliyowataka Watanzania kuwa makini na wahamiaji haramu ili kudhibiti kundi hilo lisiingie nchini.

Shekhe Ponda alisema ni vyema Serikali ikawa makini na sera za mataifa makubwa ambayo yameingia katika migogoro na baadhi ya nchi za Afrika kwa maslahi binafsi.

“Serikali iache kujiingiza katika migogoro na kundi hili, jambo la msingi ni kuimarisha ulinzi wa mipaka yetu si vinginevyo,” alisema Shekhe Ponda na kuongeza kuwa, si kweli kwamba kundi hilo ni la kigaidi kama alivyosema Bw. Nahodha bali kinachofanywa na kundi hilo ni kulinda mipaka ya nchi yao.

Alisema Bw. Nahodha hapaswi kuwaweka Watanzania katika hofu ya kuvamiwa na kushindwa kusafiri kwa shughuli mbalimbali ambazo ndioz huwapatia kipato na kukuza uchumi wao kutokana na taarifa za upotoshwaji dhidi ya kundi hilo.

“Waziri anapozungumzia kundi hili ni sawa na kudhalilisha Uislamu, mbona hivi karibuni wameingia Wakongo wakiwa na silaha nzito lakini Serikali haikufanya kitu, kwanini Al-Shaabab,” alihoji Shekhe Ponda.

Bw. Ponda alisema kauli iliyotoa Bw. Nahodha, imelenga kuwagawa Watanzania ili waichukie nchi ya Somalia kitu ambacho si sahihi.

Hivi karibuni, Bw. Nahodha alisema kutokana na nchi jirani ya Kenya kukumbwa na vitendo vya uhalifu vinavyofanywa na kundi hilo, umefika wakati wa Watanzania kuwa makini na watu ambao wanaingia nchini kinyemela bila kufuata utaratibu

17 comments:

  1. Ponda ni wakala wa Al-Shaabab kwa Tz nini?

    ReplyDelete
  2. Huyu Sheikh ni mwenda wazimu tena amelipwa na Al Shaabab kuimaliza Tanzania. Muogopeni huyu jamani. Kwani Nahodha siyo muislam? au kwa vile siyo Sheikh kama yeye?

    ReplyDelete
  3. ponda anaishi kwa kazi hizo za propaganda za kiislam ,kwanza yeye ni Murundi anaishi kwa hisani tu ya tangu utawala wa Raisi Mwinyi.alisababisha vurugu za Mwembe chai yeye na Maagezi ni watu hatari, anatetea haki za waIslamu kwani Bwakata haipo!.ni shwetani tu, ila muhimu serikali yetu isingie kichwakichwa na kufanya uadui na Alshaabab, ni hatari kwa nchi ambayo imeliwa na rushwa na hakuna ulinzi na usalama wowote wa maana hapa nchini.

    ReplyDelete
  4. Mhariri unakosea unaposema waislam, ponda na wajinga wenzake hawawezi kuwawakilisha waislam wa Tanzania. Al-shaabab somalia wanauwa wakristu au waislam wenzao, ponda nenda mirembe ukaangalie afya ya akili yako

    ReplyDelete
  5. Imetosha na tumsamehe

    ReplyDelete
  6. Wewe kama huna la kusema bora unyamaze kimya. Sheikh wetu si mwendawazimu, jee wewe utakuwa radhi kutangaziwa mashekhe wenu wanajihushisha na
    biashara ya dawa za kulevya. Ufikiri vizuri kabla ya kutamka. Majaraha yanayosababishwa na Ulimi ni makali kuliko yale yanayosababishwa na upanga. Ukisema Shekhe wa Kiislamu mwendawazimu, manaake unaitukana jamii ya Kiislamu na haya lazima uyajuwe.

    ReplyDelete
  7. USHEHE NI TUNU TU NA HAINA MAANA KWAMBA MTU AKIWA SHEHE BASI HAWEZI KUWA MGONJWA WA AKILI. SIONI HATA MOJA LINALOFANYWA NA ELISHAABABU LINALOSTAHILI SIFA.WALE WASHENZI WANAUA WATU WASIOKUWA NAHATIA SIJUI KAMA HILO LINAKUBALIKA KATIKA DINI YA UISLAM.ANAYEWATETEA NI HAYAWANI USHEHE WAKE NI WA BANDIA NA HANA THAMANI KATIKA DUNIA YA WATU TIMAMU. NA ALAANIWE

    ReplyDelete
  8. wakristo acheni chuki zenu, mnataka kuendeleza MFUMO KRISTO SASA TUMEWASOMA, HAKI ITAPATIKANA TU. KUNA WAUAJI AU MAGAIDI DUNIANI KAMA WAKIRISTO WAMAREKANI. HAYU NI MAWOZO YA KIJINGA SANA. SH PONDA YUKO SAHIHI.MBONA SISI TUMEKAA NA WAKIRISTO MUDA MREFU TENA MKITUNYONYA NA BABA WENU WA TAIFA MBONA HATUJA WAUA. NA ALIE ANZISHA UGAIDI NI MAREKAN TATIZO LENU WAKIRISTO NI KUWATHAMINI WAZUNGU SASA WATAKUJA KUWAOA NA HIVI WANATAKA USHOGA.
    KWANZA CHEO CHA BABA NI KANISANI INAKUWAJE RAIS MSITAAFU ANAITWA CHEO CHA KANISANI, SAINT BABA..,HUU NI WIZI MTUPU.
    SOMENI HISTORIA YA NCHI HII MPATE UKWELI JUU YA WAISLAM, HUYO NAHODHA NA WENZAKE NI MFUMO KRISTO TU, WAISLAM POA

    ReplyDelete
    Replies
    1. INAVYOONEKANA WEWE NI MJINGA MAANA COMMENT UNAZOTOA ZINADHIHIRISHA. ACHA UKWELI UWE UKWELI.KAMA HAMKUSOMA SHAURI YENU MAANA WAARABU WALIKAZANIA BIASHARA TU.KUMUITA BABA WA TAIFA NI VILE ALIYELETA UHURU NA SI VINGINE.NYIE MNAPENDA SHARI ONA BOKO HARAMU (NIGERIA),ALSHABAB(SOMALIA) NA ALPONDA MNATAKA KUWA NYIE.

      Delete
  9. Said utakuwa umeishia madrasa, na kwa ujinga huo utaendelea kutawaliwa kifrikra. Marekani na ukristu ni vitu viwili tofauti ndugu yangu.
    juzi mahujaji wamekwama Saud Arabia ulisikia shida waliyopata?, au wakristu wale au kule kuna mfumo kristu?
    Ala shaabab wanauwa waislam wenzao somalia. ila kwa mjinga kama wewe unaona sawa, au dini inavyokufundisha, Syria wanakufa wakriso, misri je? mbona husemi kuhusu hao, nenda shule kama una vigezo ili usitawaliwe

    ReplyDelete
  10. Ponda akili zake hazina akili na nafikiri ana ajenda ya siri na hao al-shabab.

    ReplyDelete
    Replies
    1. SIJAPATA KUMWINA MPUMBAVU KAMA WEWE NA NAMWOMBA MUNGU ANIEPUSHIE MPUMBAVU KAMA WEWE MPAKA NAKUFA NAKUOMBA UMWOMBE RADHI SHEIKH WANGU PONDA ISA PONDA KWANI INAWEZEKANA KAMA HUNA WENDAWAZIMU BASI UMETOROKA MIREMBE MDA SI MREFU KWA UTUMBO ULIOUELEZA HAPO JUU.

      Delete
  11. Ponda ni mwendawazimu, wala hilo sio swala la kujadili! Hajui hata anachosema kuhusu wacongo waliokamatwa, hajui hatua za serikali, uhamiaji au jeshi kule Kigoma, au alitaka vita ianze na Congo? Hiyo peke yake inaonesha kiasi cha ujinga na ushabiki tu. Al-Shabaab ni wendawazimu kabisaa! Ukiangalia documentary moja ilirekodiwa na kurushwa Aljazeera, utaona uongozi wa hawa wehu unavyotenda dhambi zisizosameheka kwa kutumia mgongo wa uislamu! Waislamu wa Tanzania tusikubali wehu huu ambao unaleta maafa kwa watu kama kina mama na watoto ambao hawahusiki na lolote!!

    ReplyDelete
  12. Kusema ukweli, si busara kutukana watu hasa viongozi wa dini wanaosimamia miongozo ya dini zao, Kwa mtu makini ukusikia jambo lichunguze kwanza,Si vyema kuonesha jazba,chuki za kidini, Me ni mkristo, nakereka sana na nyinyi wakristo wenzangu mnaotukana humu, Leo kaandikwa sheikh tumetukana, kesho akiandikwa Askofu,Padri, na wenzetu wakitukana, hautafika mbali,Kwani hakuna mtu aliyekuwa mkamilifu mbele Bwana, Maaskofu wangapi wanaongea pumba! kuna njia nzuri ya kusema, sio matusi, ndugu zangu,

    ReplyDelete
  13. Hivi Ponda ni wakili wa Al-shabaab Tanzania? mbona kauli yake haina mashiko. wahamiaji haramu toka Somalia maana yake ni waislam? Mbona nchi ile wote ni waislaam hata majambazi wa kisomali?

    Acheni hisia zisizo na maana!!!

    ReplyDelete
  14. Vita dhidi ya Al Shababi kamwe sio na haviwezi kuwa vita vya kidini. Hiki ni kikundi cha kigaidi na hakistahiki sifa yoyote. Sheikh anaposema makini itumike, ni vema ila huwezi kufanya urafiki na gaidi kwa kunyamaza. Akifungiwa mirija ya mapato kwingineko kunyamaza kwako hatokuona kama hisani. Ni sawa na kumfunika nyoka chini ya kitanda eti wamwogopa, itaja siku ya kukukabili. Tanzania na Afrika Mashariki itakuwa bora zaidi na salama Al Shabab wakiwa hawapo kuhatarisha usalama. Wala kutulia hakuihakikishii Tz usalama wake dhidi ya magaidi hawa.

    ReplyDelete
  15. vyombo vya usalama police,jwtz,jkt,magereza,uhamiaji,etc,hawana net work inayowaunganisha na hii ni hatari kwa nchi km ya kwetu,wanakamatwa wahalifu wa ngazi tofauti hivi vyombo vingekuwa na mawasiliano na kuona ni chombo kipi ,cha kushuhulikia tatizo husika,ukiwa kwenye viwanja vya ndege,bandari,mahakama,na mipakani ndipo utakapo ona hatari ilivyo kubwa,watu wana angalia rushwa badala ya usalama wa nchi,Malawi wana ulinzi wakuigwa ,nimefanya biashara Malawi,nimejifunza mengi,na wanafikiri kila anaye ingia nchini basi ni mtalii aheshimiwe ndio lakini usalama wetu kwanza,lazima kila mtu akaguliwe,hata km ni nani au ametoka taifa gani,km mataifa makubwa wanavyofanya,lasivyo vijana wetu hawata pona kutokana na madawa ya kulevya.

    ReplyDelete