25 November 2011

TBS yanasa mabati bandia, yapigwa mafuruku sokoni

Na Mwandishi Wetu

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limepiga marufuku uzaaji wa mabati yanayouzwa na kampuni ya Kamaka CO LTD, iliyopo Barabara ya Mandela, jijini Dar es Salaam, baada ya
kubainika hayakidhi matakwa ya viwango.

Hatua hiyo ilifikiwa Dar es Salaam jana baada ya maofisa wa shirika hilo, kujiridhisha kuwa mabati hayo hayana ubora wala anuani ya mtengenezaji.

Kwa msingi huo TBS imewataka wananchi wasinunua mabati hayo wakati hatua zingine za kisheria zikiendelea kufanyiwa kazi dhidi ya wahusika, waliohusika kuyaingiza kwenye soko.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Ofisa Masoko wa TBS, Bw. Daud Mbaga,alisema  wananchi hawatakiwi kununua mabati hayo baada ya shirika lake kujiridhisha kuwa hayana ubora.

Alisema sheria mpya Namba 2 ya mwaka 2009 inaipa TBS meno ya kuharibu bidhaa ambazo zinaingizwa kwenye soko bila kuwa na viwango au kurudishwa kule zilikotoka kwa gharama za mhusika.

Alisema TBS ifatilia ili kujua ni nani aliyehusika kuingiza mabati hayo nchi, ili na yeye aweze kusaidia shirika ni wapi yalipotola. Alisema walizungumza na Meneja Mauzo wa Kamaka, Bw. Idrisa Coptecin, ambaye alisema na wao mabati hayo waliyanunua kwa mtu mwingine.

Akizungumza na waandishi wa habari, Bw. Coptecin, alisema halikuwa hajui kama mabati hayo hayana viwango, kwa hiyo hakuwa anayauza kwa makusudi.

Alisema bando moja ya mabati hayo imekuwa ikiuzwa sh. 250,000 na tayari alikuwa amebakia na mabati kama 3,000 kwenye ghala lake. Aliahidi kutoa  ushirikiano kwa TBS katika kushughulikia suala hilo.

TBS imekuwa ikifanya ukaguzi wa mara kwa mara na kuchukua sampuli za  bidhaa tofauti na kwenye kuzipima kwenye maabara zake ili kujua kama zinakidhi matakwa ya ubora.

No comments:

Post a Comment