*Juhudi za kumtoa Mbunge Lema mahabusu zakwama
*Mahakama yakataa kumpa dhamana hadi Novemba 14
*Mbowe,Slaa watangaza hali ya hatari hadi kieleweke
Na Waandishi Wetu, Arusha
VIONGOZI, wanachama na wapenzi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) Mkoa wa Arusha wamefungua ukurasa mpya wa kudai kilichodaiwa kuwa ni ukombozi wa taifa kwa kutumia mbinu za kukesha uwanjani baada ya mbinu ya maandamano kushindikana.
Uamuzi huo wa wana CHADEMA kulala uwanjani ulitangazwa jana na Mwenyekiti wa chama hicho Bw. Freeman Mbowe, Katibu Mkuu Bw. Wilibroad Slaa kwa madai kuwa unyanyasaji unaofanywa na serikali na vyombo vyake kama Mahakama, Polisi, Idara ya Usalama wa Taifa umefikia kikomo hivyo kilichobaki ni kujikomboia kiana.
Bw. Mbowe alitangaza uamuzi huo jana katika uwanja wa NMC mjini hapa baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha kukataa kutoa hati ya kudhaminiwa kwa mbugne wa jimbo hilo Bw. Godbless Lema, kwa sababu mbalimbali za kisheria.
Moja ya sababu iliyotajwa na mahakama hiyo jana kukataa kudhaminiwa kwa Bw. Lema ni tarehe ya kufikishwa makamani kwa mwanasiasa huyo kupangwa Novemba 14 mwaka huu na si vinginevyo hivyo kuwataha wadhamini kufika mahakamani siku hiyo.
“Sasa tunatangaza utaratibu wa jinsi ya kudai haki zetu ili kulikomboa
taifa hili na manyanyaso, tumezungumza lugha ya ukombozi wa taifa letu kwa
muda mrefu lakini CCM inaringa na Polisi wake, inaringa na Usalama, inaringa na magereza sasa tumegundua mbinu mpya ya ukombozi wa taifa hili ni kulalala hapa hatuondoki,"alisema Bw. Mbowe na kuongeza.
"Hatuongoipi Polisi, mvua, mabomu, risasi na hata njaa, tutakesha hapa
katika uwanja huu, asisumbuliwe mtu asipigwe mtu, huu ni uwanja wa wakubwa…kila mmoja ampigie simu mke wake alete chai, na kila mmoja ampigia rafiki yake aje tulale hapa,tunaanza na Arusha na kisha Mbeya, Mwanza, Moshi na Dar es Salaam mpo tayari?,”alihoji Bw. Mbowe akihamasisha watu kumuunga mkono.
Kwa upande wake Dkt. Slaa alisema Arusha ni mwanzo wa ukombozi wa taifa
hili na kudai kuwa manyanyaso ya watanzania yamedumu kwa muda mrefu hivyo Bw. Lema aliyemuita kuwa ni shujaa amejitolea hivyo watapigana hadi kulikomboa taifa.
“Tumezaliwa Tanzania, tumekulia Tanzania na sasa tupo Tanzania, Mwalimu
Nyerere asingekuwa mvumilivu tusingepata uhuru wa bendera, uvumilivu sasa
umefika mwisho, leo ni siku ya ukombozi tunafanya maamuzi magumu na siyo
mengine ni kulala hapa hapa uwanja wa NMC Unga Limited,”alisisitza Dkt. Slaa na kuongeza.
“Mapambanao si lazima yawe ya maandamano, kukaa chini pia ni mapambano na ni namna ya kupeleka ujumbe wa wahusika ya madai yetu ya haki wangapi
wapo tayari?,”alihoji.
Alionya kuwa lolote litakaotokea wasilaumiwe na kwamba wako tayati
kwa kitakachotokea bali kila mmoja ahakikishe ameshiba kwa kuwa wapo katika maombolezo ya mbunge wao ambaye ataendelea kuishi rumande hadi Novemba 14 mwaka huu.
Hata hivyo mkutano huo uliingia dosari baada ya kuvurugwa na mvua
zilizonyesha mfululizo kuanzia saa 10.15 jioni dakika 15 tu baada ya
vingozi hao kuingia uwanjani hapo wakitokea mahakamani kulikokuwa kumejaa
wakisubiri mbunge huyo kupata dhamana.
Mbunge Lema alienda rumende Novemba mosi mwaka huu baada ya kukataa
dhamana kwa kile alichodai kuwa ni kwenda kutafuta ukombozi grerzaji na kueleza kuwa ni eneo bora kwa kazi hiyo huku wenzake 18 wakidhamaniwa na ndugu zao na kuachiwa huru.
Imeandaliwa na Said Njuki, Pamela Mollel na Queen Lema, Arusha
Saa ya ukombozi ni hii. Mkombozi wa mwananchi wa TZ ni yeye mwenyewe. Si siri Polisi nao wamezidi jamani kuwa vibaraka wa wakubwa. Hakuna cha Mahakama hapa ni unyanyasaji tu. Na Arusha kuna hawa Magesa wawili - Hakimu na Mkuu mpya wa Mkoa ambaye ameingia mji huu kwa mbwembwe. Ndugu Mkuu wa Mkoa tahadhari kabla ya hatari tuonavyo sisi wana-Arusha wewe utaleta uvunjifu wa amani wenzako wamepita wengi hapa lakini walikwaa kisiki nakushauri tumia busara zaidi ya ubabe. Hutafanikiwa kwani umeingia kwa matambo mno na kusema hadharani ulipoonana na watumishi wa CCM Wilaya kwamba kazi yako ni moja tu kutokomeza CHADEMA. Je ndicho kilichokuleta Arusha? Kama ndivyo pole Mkuu.
ReplyDeleteChadema nao na Lema wao wamezidi jamani! Yaani hata sheria za mahakama hawajali wanachojali ni kupata madaraka tu. Sasa Arusha pekee yake haiwezi kuwapa urais. Sisi tunaona Chadema ni chama makini lakini tunakokwenda wataishia pabaya kama CUF! Sasa jaziba za nini? Kwanini hamtaki kufuata sheria za nchi? Je ninyi mkiwa na rais ndo mtaafuata utawala wa sheria? Kila kukicha ni maandamano mpaka lini?
ReplyDeleteSerikali ya Tanzania tunaelekea wapi sasa?kwani ni wakati wa kuangalia mambo ya msingi hasa haki ya kila mtu. Ni ukweli usiopingika kuwa Tanzania ni nchi ya unyanyasaji sana hasa jeshi la polisi ,ole wao ninasema, Mungu anawaona mnayoyafanya, hizo drama hatutaki, Halafu Rais amekaa kimya kama hayupo vileeeeeeeeeeeeee. Hakuna rais makini Bongo
ReplyDeleteWe unayesema eti Chadema na Lema wamezidi mawazo yako ni mafinyu mno,we sijui kabila gani,hata huna wazo hata moja.We unaona nchi inakwenda sawa au we fisadi na wenzio hao???Waswahili walisema sikio la kufa halisikii dawa,kweli kabisa sertikali na viongozi walioko madarakani hawafanyi haki ni wachache sana kama vile Dr Mwakiembe.Haki yako unanyanganywa bado unashingilia eti chadema na Lema wamezidi,tunakushangaa sana chadema hawako peke yao nasi tuko nje ya nchi,pamoja mi ccm lakini serikali yetu imechosha watu,pia manyanyaso kwa raia si tu vyama vya upinzani,rushwa,porisi kila pembe rushwa.Si Arusha tu yaweza kuwapa Urais si tuko nje tunaungana na chadema Lema anasingiziwa kwa shinikizo la serikali na porisi wasiofanyakazi kwa maadili.Sijui we kabila gani,akili finyu,iko ndani imefichwa kama kiungo chako chako kinachotabaanisha kuwa we ni mke au mme.We kaa ndani kama mawazo yako yaliyo ndani.Sadam Hussein,Gadafi na wengineo wako wapiii?? ccm ikitoka nchi itaneemeka tuna vyanzo vingi vya utajiri,lakini watu waliomadarakani wanafinyanga tu mambo.Subiri 2015.
ReplyDeleteMimi nafikiri serikari inalake jambo, wote walio magerezani si wakosefu, Mzee Mandela alikaa gerezani na wengine wengi kwa kudai haki na uhuru wa walio wengi. Naungana na wanachadema wote katika maamzi magumu watakayo yatoa.
ReplyDeleteKikwete anaona ni fahari kula hadharani kutulingishia watanzania, tumejifunza nini watanzania kuonyeshwa watu wakila hapo nje wakati watu wengine wakiwa na shida nyingi na taifa likiwa na matatizo mengi yanayolikabili! hapo tumeliwa,Mzungu huyo amekuja kuvuna na si vinginevyo baada ya Muda atapewa ardhi yetu, kama si ardhi atapewa sehemu ya kuchimba rasilimali zetu, na kama si hayo kuna kupewa nyara zetu, hiyo ilikuwa ni biashara.Watanzania tumeliwa! Saa ya ukombozi ni sasa, Ningefurahi kama angeu BINAFISHA URAIS kwanza kwani hapo kuna mapungufu Makubwa ya Maamuzi, Vinginevyo tutaendelea kuliwa.Jamani Tuamkeni, ukiona polisi anayetetea matatizo kama ya Arusha ana masirahi binafsi au si mwadirifu katika kazi zake analinda au anaficha makosa yake kwa kupitia CCM,Mimi binafsi nimechoka je wee?
chadema hakuna kulala hadi kieleweke.ukiona giza nene ujue asubuhi inakaribia
ReplyDeletekwa huko uwanja wa Unga Limited kesheni,mlale huko hata mwezi huku sehemu zingine tuachieni wenyewe,kwanza itakuwa nafuu sana kwetu maana uwizi utapungua maana vibaka wote ni sapota wa Lema.
ReplyDelete2. Lema ameitaka jela mwenyewe kwani dhamana ilikuwa wazi,sasa mnatuletea fujo za nini Arusha,subirini hadi tarehe ya mahakama ikifika mumuwekee dhamana kwani iko wazi lakini si kwa siku au saa umnayotaka nyie.
3. Jeshi la Polisi,Mahakama na Serikali hii ni changamoto kwenu na mkiwa dhaifu mtashindwa kufanya kazi zenu. mliweka wazi dhamana bwana mkubwa kwa kupenda sifa na umaarufu alikataa au pengine alienda kuonana na vijana wake wezi wa magari na kupanga mikakati ya kuwatoa.
4. Waarusha sasa ni wakati muhimu kuamka na kukataa makabila mengine zaidi ya Wameru,Waarusha na Wamasai kuwa wabunge katika majimbo yetu hasa ya Arusha mjini. Hawa Wachaga kwao hawakubali mtu mwingine awe mbunge lakini hapa kwetu Arusha wanaona wana haki ati tu kwa sababu ni haki yao lakini kule Moshi ni wachaga tu. Tulikataeni hili hata wakisema mbona bungeni kuna wahindi na wasomali tuwaambie wawape hao wahindi na wasomali umbunge jimboni kwao,sio wawape wachaga tu
USHAURI mi naona Chadema kama kuna tatizo bora kuchugua kikundi cha watu kama 8-10 kuwa wakilisha kuliko kwenda kwa mlolongo namna hiyo inakuwa ni fujo ustaarabu kama mnavyodai mko kwa amani mngefanya hivyo, na wangine kusubiri kwenye office zenu mletewe salamu nafikiri hata hakimu angewafikiria, kwa namna hiyo matakuwa mnaoneshana ubabe na serikali.
ReplyDeletefggfe
ReplyDeleteSlaa na Mbowe mna lenu. mnataka serikali iingilie uhuru wa mahakama? Hivi ninyi mkipewa sarekali ndivyo mtakavyo fanya? Nina wasi wasi na ninyi. Mkipewa nchi Mtaingilia bunge na mahakama. Tulisha waamini sasa mmeanza kutukatisha tamaa. achani hizo
ReplyDeletenyie polisi mngewaacha hao chadema walale uwanjani hata mwezi. wakiwa huko mji unakua na amani. vibaka wote ambao ndio masapota wa lema nao wanaua huko. tunalala kwa amani. WAAZHENI WALALE HUKO SISI TUPATE USINGIZI
ReplyDeletewatanzania tunahitaji elimu ya uraia lakini je tutaipata wapi ikiwa serikali yenyewe haiitambui elimu hiyo? ndugu zanu watanzania tusiwe tunakuwa washabi wa au wanasiasa wa hiari.tunapozungumzia umaskini kuna watu wanasema hakuna umasikini kisa kuna watu wanaamkia baa,wanaendesha magari ya kifahari na wanapata kila wanachohitaji na anayesema hivyo anakula mlo mmoja kwa siku lakini anashindwa kujenga hoja kwa kujiangalia mwenyewe.
ReplyDeleteTulichukulie suala la lema kama la kitafa na sio la chama.Hivi yakipatikana matunda mazuri au mabadiliko kupitia kwake kuna atakaemnyoshea kidole?
Hivi hata uhuru tulionao japo tunaweza kuuita wa bendera asingekua mwalimu Nyerere na watuwachache waliokua na uchungu na nchi yao tungeupata? au kwa sababu hakuna ambaye alikatwa mikono kwa kukataa kulima kwenye shamba la mkolono? au kukataa kubalishwa na mkufu au shanga kwenda kwenye mashamba ya miwa marekani?
watanzania tujaribu kuondokana na imani za kuachia kila kitu kwa serikali kwani serikali sio rais wala mbunge bali ni sisi wenyewe kwanini rais na wabunge wasifanye kile tulichowaagiza?
hata katika vitabu vitakatifu vimeandika kwamba mtu usiozaa matunda unakatwa na kuondolewa. hii ni mifano lakini hata katika maisha yetu ya kila siku mmea usio zaa matunda unaondole kwani uongo?
niwaombe watanzania wenzangu tuache kunyosheana vidole tushikamane kuuondoa unyanyasaji na dhuluma.hivi kuna anayependa kununua sukali kwa 2500-3000/= au lita ya petrol kwa 5000/= au nauli ya daladala kwa 500-100/=? unaweza ukashangaa lakini ndiko tunakoelekea. jaribu kuangalia rate ya kubalishia pesa ya kitanzania na pesa ya nchi nyingine kama kenya na zingine. tubadilike.tuwe watanzania na sio CCM, CHADEMA, CUF, NCCR na vingine.
"TANZANIA NI YETU NA SISI NDIO WATANZANIA"
Hivi ni nani ameiroga CCM? Au ni laana ya mwasisi wao Hayati Mzee Nyerere waliyemwaibisha kwa kuyaacha mema yote aliyowausia?
ReplyDeleteNi Nyerere aliyewaonya juu ya rushwa, ukabila, udini na ufisadi lakini sasa wao ndiyo "makuhani" wakuu wa yote hayo! Na kama kwamba hiyo haitoshi sasa wanahangaika na kuwapa umaarufu ikiwa ni pamoja na kuwanadi kwa wananchi CHADEMA! Wanadhani kuwanyanyasa kwa kutumia Polisi na Mahakama (ambazo kwa hali inavyojionyesha zinafanya kazi kama vitengo vya CCM) watauzima moto wa ukombozi!
Nadhani saa ya ukombozi imewadia na CCM inayoenda kamagari lililokata usukani inaelekea shimoni itakakotumbukia na kubaki kwa miango kadhaa huko!
Je, hakuna mwenye akili ndani ya CCM atakayeweza kuwaonya juu ya hatari iliyo mbele yao? Sipendi kuamini kwamba woote wamelewa mvinyo wa ufisadi ulioongezwa ladha na siasa za udini, ubaguzi na u-matabaka! Wanasahau kwamba wanaanzisha mtindo utakaotumiwa na vyama vingine pia vitakapoingia madarakani, mtindo wa kugandamiza upinzani ambao wao hawako mbali na muda wa kubadilishana majina na wanaoitwa wapinzani sasa. Labda niwakumbushe tu ili wachache wenye akili watafakari na wachukue hatua. Aliyekuwa mtawala wa Southern Rhodesia (Sasa Zimbabwe)Ian Smith alitunga sheria nyingi za kuwabana wapinzani ikiwa ni pamoja na ya kuwaweka kizuizini wapinzani bila mashtaka hadi mkuu wa nchi atakapoamua. Muda haukupita nchi ilipata Uhuru na Mugabe,kwa kutumia sheria ileile alimweka kizuizini na kuzua mtafaruku toka nchi za magharibi waliolalama hatendewi haki. Walifunga midomo walipothibitishiwa ilikuwa ni kwa mujibu wa sheria zilizoasisiwa na Smith mwenyewe! Nina mashaka kama CCM hawatatumbukia kwenye shimo wanalolichimba. Mungu ibariki Tanzania.
Jela Lema kataka mwenyewe halafu mnasumbua watu. Weldone jeshi la polisi msitawaliwe na vipanya tekelezeni wajibu wenu
ReplyDeleteUNAFIKI WA CHADEMA HUU HAPA. HAYA SASA MFUKUZENI HUYO MCHAGA NA MMBULU. KILA SIKU TUNAWAAMBIA WAJINGA NYIE NI LINI MCHAGA AKAKUA HAKI YEYE WAZO LAKE NI PESA TU. HATA NDUGU ZAO WANALALAMIKA SUKARI SUKARI KUMBE HAOHAO MATAJIRI WANAOFADHILI CHADEMA WAKO TAYARI NDUGU ZAO WAKOSE HIYO BIDHAA MUHIMU WAPELEKE KENYA WAPATE MAPESA. ATI LEO TUMPE MBOWE HAZINA YA NCHI KAMWEEEEEEEEEEEEEEEE. UNAFIKI WAO WA BUNGENI HUU HAPA:-
ReplyDeleteKiwango cha mshahara tunaolipwa sasa kiliwekwa muda mrefu na inawezekana wakati huo kilikuwa kikitosheleza, lakini kimebakia hapo kwa muda mrefu licha ya watumishi wengine viwango vyao kubadilika, sasa tunadhani ni wakati mwafaka jambo hili kufikiriwa,” alisema mmoja wa wabunge aliyehudhuria kikao hicho.
Mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini, alinukuliwa akisema uwakilishi umekuwa mzigo, kwani wakati mwingine amekuwa akitumia fedha anazozipata kwenye vyanzo vyake binafsi kuwatumikia wananchi.
“Hapa nina mialiko 26 ya kwenda kuchangia ujenzi wa shule na shughuli nyingine za maendeleo kule Rombo, zote hizi zinanihitaji kama mbunge nitoe fedha, sasa jamani fedha hizi zinatoka wapi,?” chanzo chetu kilimnukuu mbunge huyo akihoji na kuungwa mkono na wabunge wengi.
Chanzo hicho kilisema Selasini alieleza jinsi ambavyo wabunge hukutana na kero ya wananchi kuomba fedha ili wakatatue matatizo yao mbalimbali nakwamba ni vigumu kukwepa jukumu hilo kutokana na hali ya maisha ilivyo sasa nchini.
Wabunge wengine waliochangia suala hilo ni Mbunge wa Mbulu (Chadema), Mustafa Akunaay, ambaye alimuunga mkono Selasini akisema malipo ya mbunge hayalingani na wajibu wake kwa umma.
Mbunge huyo alinukuliwa akisema wabunge ambao wamekuwa wakipinga posho wanazopewa huenda wana vyanzo vingine vya fedha ambavyo wanavitegemea.
Hongera sana Serikali,fanyeni kazi ipasavyo,uchaguzi umeshaisha tunahitaji amani,utulivu na maendeleo,chapeni kazi kwa mujibu wa sheria,siwashangai sana hawa wachaga,maana wachaga wengi sheria hawazijui,wao wanachojua ni biashara na jinsi ya kutafuta mali na fedha,wengi hawajaenda shule,leo wanajidai wanatafuta haki za watanzania kwa kuingia magerezani wenyewe,ni haki gani inatafutwa kwa kuvunja sheria za nchi,hao ni wanjanja wanataka madaraka kwa ajili ya mali,
ReplyDeleteWITO KWA WATANZANIA:tusidandanyike,hakuna nchi inayoongozwa na malaika,matatizo ya kiutawala yako nchi zote na yanatatulika,hawa Chadema wasijione kuwa hao ndio malaika hawatakuwa na dhambi,hao ndio tuwaogope kama ukoma maana wana asili ya Uchaga,wachaga si mnawajua kwa hela.
CHADEMA NAWASHAURI:
ReplyDeletelema ni Waziri Kivuli wa mambo ya ndani,ameamua kwenda gerezani kikazi zaidi ili asiwe anasimuliwa akiwa bungeni,hivyo muacheni yuko kikazi zaidi,anaonja ugali wa dona na maharage, na anakojolea ndoo,ndio akili yake imemtuma aende huko,sasa mbona mna haribu amani ya nchi wakati mwenzenu yuko kazini,msubirini hadi tarehe 14 mtamuona ili awasimulie aliyoyaona huko. CHADEMA HACHENI UJINGA.
Je Mbunge akimlawiti mwanao ni mpaka Spika apewe taarifa ili ukamatwe? polisi hili msilikubali mbunge akifanya kosa kamata akanyie ndoo jela. msisumbuliwe na hawa PANYA
ReplyDeletenadhani Chadema wanapitwa na wakati. ule uongo tuliodhani ni kweli sasa ni dhahiri uongo,. hapa sio libya, misri, tunisia. walidhani falsafa yao ya NCHI HAITATAWALIKA ITATIMIA wajue sasa watanzania tumechoshwa na vurugu zao , lema sio watanzania, lema sio, suluhisho la matatizo ya watanzania. watuache tuijenge nchi yetu toka umaskini.
ReplyDelete