Na Mwandishi Wetu, Igunga
MBUNGE wa Igunga Dkt. Peter Kafumu, (CCM), ametoa onyo kali kwa watumishi wa Halmashauli ya wilaya kuwajibika na kuwataka wenye tabia ya kula fedha zinazotolewa na serikali kwa ajili ya miradi ya maendeleo kuacha mara moja kabla ya kufikiwa.
Amesema wakati wa kampeni alipokea malalamiko mengi na kwamba karibu kila sehemu alikokipita kuangalia utekelezaji wa miradi ya maendeleo wananchi wanamwezeleza kuwa fedha nyingi zinazotolewa na serikali kuu zinaliwa na wajanja wachache na kusababisha wao kukosa imani na serikali yao.
Akizungumza katika kikao chake cha kwanza na Madiwani baada ya kuapishwa wiki iliyopita mjini Dodoma mbunge huyo aliliambia Baraza la Madiwani ya wilaya hiyo kuwa hategemei tena kuona hali hiyo kwa watumsihi wa umma na kuwaomba viongozi bao kumpa ushirikiano wa karibu juu ya kero hiyo.
kuhusu utekelezaji wa ahadi za CCM wakati wa uchaguzi huo mdogo alisema anategemea kuchimba bwawa kubwa kwa lengo la kuondoa adha ya maji jimboni – Igunga na kuwaomba madiwani wote kumpa ushirikiano kufanikisha mradi huo mkubwa.
Katika hatua nyingine Baraza la Madiwani wilayani Igunga kimelaani vikali kitendo kilichofanywa na baadhi ya wananchi wa Kata ya Mwashiku cha kumchoma moto hadi kufa aliyekuwa Mkuu wa shule ya Sekondari Mwashiku, Mwalimu Charles Medady kwa tuhuma za wizi wa saruji.
Awali Mwenyekiti wa Halmashauri ya Igunga Bw. Abubakari Shaban, akimkaribisha rasmi Dkt. Kafumu katika baraza la madiwani aliwaomba wajumbe kusimama kwa dakika tatu kumwombea marehemu.
Kwa upande wake Dkt. Kafumu aliahidi kwenda katika eneo hilo kutoa elimu maalum kuwawezesha wananchi hao kutochukua sheria mkononi badala yake watumie njia za kisheria kushughulikia matatizo na vitendo kama hivyo.
Hawezi kuchukuwa hatua maana hata yeye amekwapua za semina huko Dodoma soma ripoti ya bunge ya Injinia Ramo.Thubutu huyo yeye ni fisadi kuliko Rostam
ReplyDelete