Na Amina Athumani
MICHUANO ya Chalenji mchezo wa gofu, inatarajia kuanza Novemba 8 hadi 11 mwaka huu katika viwanja vya
Klabu Gymkhana, Arusha.
Katika michuano hiyo, Tanzania itawakilishwa na wachezaji wanane, ambao wataunda timu ya taifa yenye wachezaji kutoka mikoa mbalimbali inayocheza mchezo huo.
Wachezaji hao watapatikana katika michuano ya Dar es Salaam Open Golf, ambayo itafanyika Oktoba 29 hadi 30 mwaka huu.
Kutokana na michuano hiyo ya Chalenji, aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Gofu Tanzania (TGU) Dioniz Malinzi, amemtaka kocha wa taifa wa mchezo huo kuhakikisha timu hiyo inatwaa ubingwa huo.
Malinzi ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa Taifa (BMT) alimtaka kocha huyo kuhakikisha Tanzania inatwaa ubingwa huo, ambao mara ya mwisho kuupata ilikuwa mwaka 2002 katika mashindano yaliyofanyika Arusha.
"Naanza utekelezaji wangu kama nilivyoagiza, hivyo nitaanza na watu wa gofu endapo watafanya vibaya nitachukua hatua ya kumtimua kocha," alisema Malinzi.
Michuano hiyo ya chalenji, itashirikisha nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na itafanyika kwa siku nne mfululizo.
No comments:
Post a Comment