Na Heri Shaaban
SERIKALI kupitia kitengo cha maafa Ofisi ya Waziri Mkuu itagharamia chakula cha wiki moja kwa ajili ya wakazi walioathirika na kimbunga kilichoezua mapaa ya nyumba
maeneo ya Mbagala, Dar es Salaam.
Hayo yalismwa Dar es Salaam jana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa (TAMISEMI).Bw.George Mkuchika, alipofanya ziara ya kutembelea waathirika hao.
Bw.Mkuchika alisema chakula hicho kinatarajiwa kutolewa leo ili kusadia familia hizo katika kipindi hiki kigumu.
"Waathirika wapo wa aina mbili kati yao watano watapewa bati kwa ajili ya kujenga upya nyumba zao na watu 630 watapewa chakula cha wiki moja," alisema,Bw.Mkuchika.
Alisema kitengo cha maafa kinafahamu mlo wa siku wa kila mtu, hivyo baada kufanya tathimini na kuwafahamu wananchi walioathirika itajua itoe chakula kiasi gani.
Aliziagiza kamati za maafa za mtaa kata, wilaya na Mmkoa kuendelea kuomba msaada ili kuzisaidia familia hizo.
No comments:
Post a Comment