Na Godfrey Ismaely
MWALIMU wa Shule ya Msingi Mazengo wilayani Newala Mkoa wa Mtwara, Bi. Fatma Nendakutoa, amekipongeza Chama cha Walimu Tanzania (CWT)kwa
kumfariji tangu akatwe miguu yake kutokana na ugonjwa wa kisukari.
Bi.Nendakutoa ambaye namba yake ya uanachama ni CWT/MTW/MTN/77 alikatwa miguu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ili kunusuru maisha yake.
Alisema CWT kupitia kitengo maalum cha kuwasaidia wanachama wake wenye ulemavu nchini kinachosimamiwa na Bw. Peter Mlimahadala,kilimsaidia kiti cha kutembelea na fedha taslimu sh.125,000.
Akizungumza na Majira katika wodi namba tisa jengo la Kibasila, jana, Bi. Nendakutoa alisema
alifika wodini hapo tangu Agosti 6, mwaka huu akitoa Hospitali ya Ligula (Mtwara) na baadaye Nyagao(Lindi).
"Baada ya kupata uhamisho kutoka hospitali hizo mbili kuja Muhimbili hali yangu kiafya ilikuwa mbaya sana, wakaamua wanikate miguu.
Aliongeza kwamba mara baada ya kukatwa miguu CWT ilimfariji kwa kumpatia kiti hicho.
No comments:
Post a Comment