Na Rehema Maigala na Anneth Kagenda
MAKAMU wa pili wa Rais wa Zanzibar Bw. Seif Ally Iddi, amepokea wa sh.mili 5.3 na vitu mbalimbali kwa ajili ya kusaidia waathirika wa ajali ya meli ya Mv Spice Islander.Misaada
hiyo ilitolewa na Jumuiya ya Wanawake wa Kiislam Tanzania (JUWAKITA), Jumuiya ya Wanawake wa Kiislamu Mkoa wa Dar es Salaam, Radio Uauti ya Quran na Jumuiya ya Maendeleo ya Watumasalamu Tanzania wakati wa dua ya pamoja iliyosomwa na jumuiya hizo jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa kusoma dua hiyo, Mwenyekiti wa JUWAKITA Bi. Shamimu Khan, alisema lengo la dua hiyo ni kuwaombea waliokufa na wale walionusurika katika ajali hiyo.
"Ajali hii imewaathiri watu wengi ndiyo maana tunaomba dua kwa wale walipoteza maisha yao na tunachangishana vitu mbalimbali kwa ajili ya kuwapelekea wale waliopoteza wazazi wao na ndugu," alisema.
Naye, Makamu wa Rais Bw. Ally Idd ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa dua hiyo, alisem amefurahishwa na misaada aliyoipokea kwa ajili ya kuwasaidia wale wote walioathirika na ajali iliyotokea.
Alisema misaada aliyoipokea ni kwa ajili ya wale wote walioathrika katika ajali hiyo na si kwa ajili ya mambo mengine.
"Nitahakikisha pesa hizi zitamfikia kila mlengwa aliyepatwa na ajali au yule aliondokewa na wazazi wake au ndugu zake," alisema Bw.Idd.
Wakati huo huo vilio na simanzi imetawala jana katika ukumbi wa Korea wakati wa swala maalum ya kuwaombea watu waliokufa kwenye ajali ya meli ya Mv Spice Islanders iliyotokea hivi karibuni.
Baada ya mshereheshaji kutangaza kwamba kwenye ibada hiyo kwamba kulikuwa na baadhi ya walionusurika, ndipo alipomsimamisha Bi. Asha Issa Mussa (29) mkazi wa Uwanja wa Ndege.
Bi. Mussa aliyeookolewa kesho yake na waokoaji alisema alikutwa Mombasa hakiwa hajiwezi na badaye kupelekwa katika hospitali kwa ajili ya matibatu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati swala hiyo ikiendelea, Imamu Mkuu wa Msikiti wa Idrisa Shekh Ally Abasaleh, alisema huu ni muda muafaka kwa serikali kuhakikisha inakuwa na vyombo vya usafiri ambavyo ni imara.
“Visiwa vya Pemba na Unguja vina mkondo unaoitwa Nungwi, mkondo huu hauitaji meli zisizo na nguvu na ikiwa meli hiyo ni zile zinazolega lega ikifika pale lazima ipasuke tu,”alisema.
“Sasa ziwepo meli kama ilivyokuwa Mv Mapinduzi, Mkondo ni kubwa,” alisema Shekhe Abasaleh.
No comments:
Post a Comment