30 September 2011

CUF sasa yairarua CHADEMA Igunga

Mbunge wa Lindi kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Bw. Salum Baruani akihutubia wananchi wa Kijiji cha Ngwamashimba wilayani Igunga wakati wa mkutano wa kampeni za kumnadi mgombea wa chama hicho, Bw. Leopold Mahona jana.
*Yadai haijakomaa kisiasa, si cha kitaifa

Na Peter Mwenda, Igunga

CHAMA cha Wananchi (CUF) kimewataka wananchi wa Igunga kutokipigia kura Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa
kuwa si chama cha kitaifa na hakijakomaa kisiasa.

Hayo yalisemwa na Mbunge wa Wawi, Bw. Hamad Rashid Mohamed, wakati akimnadi mgombea wa ubunge katika uchaguzi mdogo wa Jimbo hilo, Bw. Leopold Mahona katika viwanja vya Barafu mjini hapa.

Mbunge aliwahi kuwa Kiongozi wa Upinzani Bungeni kabla ya Bw. Freeman Mbowe wa CHADEMA kuchukua nafasi hiyo, alidai kuwa chama hicho hakijakomaa kisiasa ndiyo maana kinajihusisha na vitendo vya vurugu ikiwemo kumwaga tindikali, kupiga risasi na mengine na kwamba hiyo inaonesha hakiwezi kuleta maendeleo ya wananchi.

Alisema chama hicho kina ubinafsi, ndiyo maana kilijitenga bungeni na kuunda umoja wa wabunge wa CHADEMA peke yao tofauti na wakati alipokuwa kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni ambapo alishirikisha wabunge wa vyama vyote vya upinzani wakiwemo wa chama hicho bila ubaguzi.

Alidai sera za CHADEMA hazina tofauti za CCM ambao wanagawa madaraka kwa watoto wao, ndugu na jamaa badala ya kufuata utaratibu wa uongozi katika jamii.

Bw. Rashid aliyewasili mjini hapa juzi na helkopta ya CUF kujumuika na wabunge wengine wa chama hicho hivyo kufanya idaid yao kufikia 20, alisema chama chake ni cha kitaifa ambacho kina viongozi pande zote za muungano.

“Makamu wa Rais Zanzibar ni Katibu Mkuu wa CUF, sisi wabunge wa Zanzibar tumekuja kwa gharama zetu kumsaidia mwenzetu aingie bungeni kuwakomboa watu wa Igunga, niambieni CHADEMA  kuna kiongoi gani Zanzibar,” alihoji Bw. Rashid.

Alisema wananchi wa Igunga wakitaka maendeleo ya kweli wamchague, Bw. Mahona kuwa mbunge kwa kuwa wana kila sababu ya kufanya hivyo ili kubadilisha maisha yao.

Naye Meneja Kampeni wa mgombea wa CUF, Bw. Antony Kayange, alisema wapiga kura wasipoteze muda kukipigia kura CCM kuwa wanakumbuka kumleta Waziri wa Ujenzi, Bw. John Magufuli  kuwaongopea.

Alisema anawadaganya kujenga daraja la mto Mbutu ambalo limeahidiwa kujengwa miaka mingi iliyopita bila ahadi hiyo kutimizwa.

“Huyu Magufuli amekuwa madarakani kwa miaka 11 mbona hata siku moja hakufikiria kuja Igunga angalau kuona kero za wananchi, leo anakuja kudanganya kujenga daraja la Mbutu huo ni uongo, msikubali kurubuniwa kupigia kura CCM,” alisema Bw. Kayange.

Naye Naibu Katibu wa CUF Tanzania Visiwani, Bw. Ismail Jussa, alisema wananchi wa Igunga wasikubali kudanganywa na vyama vingine kwa kuwa wataendelea kukabiliana na matatizo waliyonayo bila kupata ufumbuzi.

Alisema katika majimbo ambayo CUF inaongoza yana maendeleo makubwa kutokana na kuwa na uwezo mkubwa kujenga hoja za wananchi na kuziwasilisha serikalini kufanyiwa kazi.

Mgombea ubunge Bw. Mahona akiomba kura kwa wananchi alisema kamwe hatakimbia jimbo lake kama wanavyofanya wabunge wengine bali atatumia muda wake mwingi kuwatumikia wananchi wa Igunga.

22 comments:

  1. walevi hao...cuf hawajakomaa ndio maana wako zaidi kicharacter assacination!

    ReplyDelete
  2. Hii comment ni ya mwnanchi nimeona nitoe huku kwani mwananchi limevamiwa na watoa maoni wa chuki:
    Yes tumendela tanzania, tuna helikopta nadhani tutachuaana na south korea: hebu ona mwang acheni ya ukabila na udini soma haya:Yes nation's chances of economic development are greatly increased if it has more and better educated people:South Korea are prepared to invest over $2billion to revolutionize educational system by converting all paper textbooks into digital versions by 2015. They plan to use SMART phones, table computers, smart TVs and other electronics devises to increase online classes and deliver course curriculum through cloud computing.... I hope we shall reach there. Acheni kujadili maudhi ndugu zangu tujadili maendeleo.

    ReplyDelete
  3. Kweli nyani haoni kundule!Wewe Hamadi rashidi Mohamed nadhani haujui hata unacho kizungumza.Hebu tuelaze kuna sehemu ambayo inaubaguzi wa wananchi kupita Zanzibar na pemba kwa hapa Tanzania?.Wacha kuongopea watu nyinyi CUF ndio wabaguzi wakubwa,Ongea kitu kingine cha maana na sio hio hoja yako ubaguzi isiyokuwa na maana.Unadai chama cheni ni cha kitaifa kwa sababu ya maalim seif,Yeye mwenyewe ameshawasahau wananchi wake kwa sababu sasa hivi anaulaji.Wacha porojo zako.

    ReplyDelete
  4. Kweli nyani haoni kundule!Wewe Hamadi rashidi Mohamed nadhani haujui hata unacho kizungumza.Hebu tuelaze kuna sehemu ambayo inaubaguzi wa wananchi kupita Zanzibar na pemba kwa hapa Tanzania?.Wacha kuongopea watu nyinyi CUF ndio wabaguzi wakubwa,Ongea kitu kingine cha maana na sio hio hoja yako ubaguzi isiyokuwa na maana.Unadai chama cheni ni cha kitaifa kwa sababu ya maalim seif,Yeye mwenyewe ameshawasahau wananchi wake kwa sababu sasa hivi anaulaji.Wacha porojo zako.

    ReplyDelete
  5. Kweli nyani haoni kundule!Wewe Hamadi rashidi Mohamed nadhani haujui hata unacho kizungumza.Hebu tuelaze kuna sehemu ambayo inaubaguzi wa wananchi kupita Zanzibar na pemba kwa hapa Tanzania?.Wacha kuongopea watu nyinyi CUF ndio wabaguzi wakubwa,Ongea kitu kingine cha maana na sio hio hoja yako ubaguzi isiyokuwa na maana.Unadai chama cheni ni cha kitaifa kwa sababu ya maalim seif,Yeye mwenyewe ameshawasahau wananchi wake kwa sababu sasa hivi anaulaji.Wacha porojo zako.

    ReplyDelete
  6. Kweli nyani haoni kundule.Hebu wewe Hamadi rashi mohamed tueleze kuna chama ambacho kina ubaguzi kwa wananchi wake kupita cuf huko Zanzibar na pemba?,Pia unadai chama chenu ni cha kitaifa kwa ajili ya Maalim seif.Cha kwanza kutoka kwa maalim seif hamadi yeye mwenyewe amesha wasahau wananchi wake kwa sababu ya ulaji.Tafathali zungumza kitu cha maana na kama huna bora unyamaze kimya.

    ReplyDelete
  7. Kweli nyani haoni kundule.Hebu wewe Hamadi rashi mohamed tueleze kuna chama ambacho kina ubaguzi kwa wananchi wake kupita cuf huko Zanzibar na pemba?,Pia unadai chama chenu ni cha kitaifa kwa ajili ya Maalim seif.Cha kwanza kutoka kwa maalim seif hamadi yeye mwenyewe amesha wasahau wananchi wake kwa sababu ya ulaji.Tafathali zungumza kitu cha maana na kama huna bora unyamaze kimya.

    ReplyDelete
  8. Kweli nyani haoni kundule.Hebu wewe Hamadi rashi mohamed tueleze kuna chama ambacho kina ubaguzi kwa wananchi wake kupita cuf huko Zanzibar na pemba?,Pia unadai chama chenu ni cha kitaifa kwa ajili ya Maalim seif.Cha kwanza kutoka kwa maalim seif hamadi yeye mwenyewe amesha wasahau wananchi wake kwa sababu ya ulaji.Tafathali zungumza kitu cha maana na kama huna bora unyamaze kimya.

    ReplyDelete
  9. Huyu Hamad nani kampa kuongea upuuzi wake huu hapo Igunga? maana hawa sasa hatuwataki waende zao umewachoka yaani hajui hata ukabila, maana yeye na chama chake kwa siasa kali za kujilipua hazioni mpaka aone siasa za ccm na chadema kichwa chake kweli siyo kizuri maana zanzibar ndio lango la madawa ya kulevya akamatwe akaguliwe kama polisi hawatakuta kete kadhaa

    ReplyDelete
  10. Hamad amechafua gazeti hili sana leo, arudi zanzibar akajilipue na mabomu

    ReplyDelete
  11. CUF badala ya kupambana na CCM wanapambana na CHADEMA hivi wanaakili sawa sawa hawa magaidi?

    ReplyDelete
  12. wazanzibar msifikiri mtakuja pata nafasi aliyopata mwinyi kuongoza nchi hii

    ReplyDelete
  13. tatizo la cuf wao ni ccm "B"

    ReplyDelete
  14. Hizi ndizo chuki za kunyimwa uongozi kwenye kambi ya upinzani bungeni, sasa kila mtu keshaona rangi zake, akae pembeni aache wenye hoja wanene

    ReplyDelete
  15. CUF ilipokuwa inaongoza kambi ya upinzani ilishirikisha vyama vote vya upinzani..hii si kweli?

    ReplyDelete
  16. Chadema hakina mjumbe yeyote Zenj si chama cha Kitaifa...na hii nayo si kweli?

    ReplyDelete
  17. Badala ya acid alimwagiwa maji...si kweli acid hakuna Igunga!

    ReplyDelete
  18. CUF milio bungeni shukuruni tu kuwa mmepata hata nafasi ya kujua bara ikoje. Hivi CHDM wangekuja Pemba ninyi CUF Wapemba mungewapokea kama milivyo jaa hiana ya ubaguzi. Ajali ya meli mwezi jana IMEDHIHIRISHA JINSI CUF MLIVYO. Kama ninyi si wabaguzi zilitakaje KAULI ZA KUDAI KUWA WAPEMBA HAWATENDEWI HAKI pale tu hata JAMBO LA HERI LILIPOAMULIWA NA MAMLAKA YA USALAMA. Nisameheni kusema WAPEMBA lakini hii ni kwa maana PEMBA SI CHO CHOTE BALI NI CUF NA HAMADI RSH NA WENZAKE NI WA HUKO HUKO

    ReplyDelete
  19. hao cuf wamechemsha chadema inatambulika kama sivyo tendwa angeifuta.hongera makamanda wa chadema kwa kuisaidia tanzania,igungatutashinda!

    ReplyDelete
  20. pasua jibu baba cufu inatisha

    ReplyDelete
  21. Hamadi Rashidi amepoteza mwelekeo na mvuto pia,siasa imemshinda.Ni kilaza, asome alama za nyakati, CHADEMA ni mwisho wa matatizo kimebeba matarajio ya wananchi hususan vijana.SIASA ZAKO ZA KITOTO AENDE NAZO HUKOHUKO ZANZIBAR.

    ReplyDelete
  22. hahahaha! CUF wananiacha hoi sana na falsafa yao ya "tukose wote" ns wivu wao wa kitoto. Angalia sasa matokeo yake mnaambulia kura 2000! Aibu kwa "chama cha kitaifa" kama chenu. Hivi kale kamtaji cha kura 11000 mlichokuwa mnaringa nacho kamepotelea wapu? au mlizipata kwakuwa mwaka 2010 CHADEMA waliweka jiwe?

    Acheni utoto, someni alama za nyakati, sisi vijana hatuingiwi na sumu za ukabila,udini au ubaguzi wowote ule, hayo siyo mahitaji yetu. tunataka mabadiliko ya kweli na tunawaunga mkono CHADEMA kwa kuwa wamethibitisha kuwa wako serious , wana ujasiri wa kufikiri na kubuni nje na zaidi ya mfumo uleule ambao CCM wameutumia kwa miaka 50 kuendesha nchi bila mafanikio pamoja na kuwa na rasilimali lukuki.

    ReplyDelete