22 August 2011

Wenger akana kuitema Arsenal

LONDON, England

KOCHA Arsene Wenger amesisitiza kuwa, hakuna nafasi yoyote itakayomfanya akiteme kibarua chake cha kuifundisha timu ya Arsenal.Shirika la Habari la Ufaransa
liliripoti jana kuwa, kipigo cha mabao 2-0 ambacho timu yake ilikipata kutoka Liverpool, ikiwa nyumbani kwenye Uwanja wa Emirates, kilifanya kundi la mashabiki kumtaka Wenger atumie fedha kabla ya kuacha kumuunga mkono, huenda ikamfanya aikimbie timu hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mchezo wa wiki hii, ambapo Arsenal itasafiri kuikabili Udinese katika mechi ya kuwania kufuzu fainali za Klabu Bingwa Ulaya na mtanange dhidi ya  Manchester United katika Ligi Kuu England, Wenger alisema kuwa, hakuna jambo kama hilo.

"Hakuna kitu chochote kitakachonifanya niondoke. Nilijibu swali hilo jana (juzi), nitaendelea kujaribu kufanya kila niwezalo kwa klabu," alisema.

"Kushindwa ni uharibifu au tetemeko la ardhi katika kazi hii. Tumefadhaika kwamba, leo tumefungwa. Najisikia kama tumepata pigo kubwa, lakini maamuzi ya kutolewa nje  mchezaji wetu na bao la kuotea," alisema Wenger.

Alisema kuwa, kwa upande wao jambo la muhimu ni kuwapa molari wachezaji kwa ajili ya mechi ya Jumatano dhidi ya Udinese na baadaye, watakapokutana na Manchester United.

No comments:

Post a Comment