19 August 2011

Watano wafa ajalini Moro

Na Ramadhan Libenanga, Morogoro

WATU watano wamekufa na mwingine kujeruhiwa baada ya magari mawili waliyokuwa wakisafiria kugongana mkoani hapa. Kaimu Kamanda wa Polisi
mkoani hapa, Bw. Joseph Rugila alisema tukio hilo lilitokea Agosti 18, mwaka huu saa 8 usiku huko eneo la Lubungo Tarafa ya Mikese, Barabra ya Morogoro - Dar es Salaam. 
 
Magari yaliyohusika katika ajali hiyo ni T 845 BSD aina ya Canter likiendeshwa na Chipengwa Yaona (22) Mkazi wa Tegeta Dar es Salaam,  ikitokea Dar kwenda Morogoro lililogongana na lori lenye namba za usajili T 880 ADF lililokuwa likiendeshwa na Fadhiri Hussein (32) mkazi wa Arusha ambapo gari aliyekuwa akitoka Mbeya kwenda Dar.
 
Kamanda Rugila aliwataja waliofariki dunia katika ajali hiyo kuwa ni pamoja na madereva wa magari yote mawili, Ofisa Maliasili wa Wizara ya
Maliasili na Utalii, Mbwana Mkiboga, Ali Yona (38) mkazi wa Dar es Salaam, pamoja na mwanaume mmoja ambaye jina lake bado halijafahamika.
 
Katika ajali hiyo, Bw. Hussen Makame (35) mkazi wa Tanga alijeruhiwa na kulazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro.


No comments:

Post a Comment