19 August 2011

Wahadhiri 21 watimuliwa Ustawi

Na Mwandishi Wetu

BODI ya Magavana inayosimamia Chuo cha Ustawi wa Jamii Jijini Dar es Salaam, imesitisha ajira za wahadhiri 21, kati ya 22 waliokuwa katika mgomo uliosababisha
serikali kukifunga kwa muda usiojulikana.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Kaimu Mkuu wa Taasisi hiyo, Mlwande Madihi, imesema hatua hiyo imeanza kutekelezwa kuanzia Agosti 17 mwaka huu, na kwamba imechukua uamuzi huo kutokana na kuendesha mgomo usio halali na kukaidi maagizo ya mamlaka za juu.

Kikao kilichofanya maamuzi hayo kilikuwa chini ya uongozi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Magavana ya Chuo hicho, Profesa Lucian Msambichaka.

Taarifa hiyo imewataja wahadhiri hao kuwa ni Bw. Faustine Nzigu, Bw. Rindstone Ezekiel, Bi. Mariana Makuu, Bi. Aziel  Elinipenda, Bw. Deodatus Mkumbe, Bw. Daudi Chanila na Bw. Viscal Kihongo.

Wahadhiri wengine ambao ajira zao zimesitishwa ni Bi. Elizabeth Bitegela, Bw. Joseph Sunguya, Bw. Constantin Njalambaya, Bi. Mwajuma Hussein, Bi. Rita Minga, Bi. Caroline Mutagwaba, Bw. Elia Kasalile, Bw. Marwa Maridadi Phanuel na Bi. Adrophina Salvatory.

Wengine ni Bw. Kinswemi Malingo, Bi. Suzana Nyanda, Bw. Machumbana Michereli, Bw. Warioba Nyamoni na Bw. Yassin Masyaga Mwita, na kwamba hatua hizo zimetaanza mara moja, huku wahusika wakizuiwa kujihusisha na lolote linalohusiana na taasisi hiyo na ulinzi mkali umewekwa ili kuwazuia wasiingie chuoni hapo.


4 comments:

  1. huu ni ulevi. management za namna hii za fukuza fukuza zinatakiwa kuangaliwa upya kwani zinaliingiza taifa hasarani time and finances...

    wahadhiri mliofukuzwa, msiogope, mlichofanya ni sahihi.....nendeni mahakamani mchukue mapesa mnunue prado za kutosha ...hakikisheni mnanunua engine za 1 kz

    ReplyDelete
  2. Mi nafikiri Serikali yetu haina uongozi kwa sasa!! Kuanzia kwa Rais hadi mjumbe wa nyumba kumi kumi!! Ninachokiona mimi ni kuwa kila mtu akiamka asubuhi anafanya anachojua hata kama hajui hilo swala linaingiza hasara kiasi gani kwa Taifa!! Haiwezekani wahadhiri 21 wakawa na matatizo au wanachosimamia hadi kugoma hakina tija!! hapo waangaliwe hao wanaojiita Management !! Serikali wanaacha watu wachache wakuu wa Taasisi za Uma wanakuwa miungu watu a matokeo yake kila siku Nchi ina matatizo yasiyokuwa na nafuu!!! Rais uko wapi, Waziri Mkuu unafanya nini na hao mawaziri je wana kazi gani???? Bongo kweli inafurahisha. Wenzetu wanatucheka eti. Mdau ughaibuni

    ReplyDelete
  3. siamini 21 wote wakawa na matatizo management fanyeni utafiti

    ReplyDelete
  4. hizo ni chuki na hira za viongozi wa chuo cha ustawi wa jamii. mimi siamini hata kidogo kuna mtu kama Mchomvu ana historia mbaya tangu anafundisha Chuo cha Ualimu Kigurunyembe, pia Madihi pampja na huyo mama yao mwenye roho kama shetani. hivi ni haki kufukuza watu kama kuku? ila naamini hapana mwenye kutenda haki isipokuwa mungu pekee maana ukweli na aibu zinawakaribia. laana za watanzania zinakuja.

    ReplyDelete