Na Godfrey Ismaely
KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bw.Nape Nnauye, ameunga mkono kauli iliyotolewa na Makamu Mwenyekiti wa
CCM, Bw. Pius Msekwa, kuwa chama hicho kimepoteza mvuto mbele ya wananchi na kuwashangaa watu wanaojiita makada kumpinga.
Bw. Nnauye alitoa kauli hiyo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu. Bw. Nnauye alisema kauli zilizotolewa na baadhi ya watu waliojiita makada wa CCM mkoani Mwanza wakipinga kauli iliyotolewa na Bw. Msekwa kwenye vyombo vya habari kuwa CCM imepoteza mvuto, hawatambuliki.
Bw. Msekwa alikaririwa juzi na vyombo mbalimbali vya habari akisema CCM imepoteza imani kwa baadhi ya wananchi, ndiyo maana chama hicho kimefikia uamuzi mgumu wa kuanza kujivua gamba.
Bw. Nnauye alisema kwamba Bw. Msekwa hakutamka jambo lolote mbaya, hivyo maneno yanayoendelea ni uzushi wa vyombo vya habari.
Alisema kama kuna makada wanaosema kiongozi huyo wa chama alikosema mbona majina yao hajayaona kwenye vyombo vya habari?
"Tuwe wawazi kwani kama hoja hizo zingekuwa na ukweli wowote hatua zaidi zingechukuliwa na chama au wewe ulimsikia kama ulimsikia tuelezane ili tufahamu hatua ambazo zitachukuliwa, hayo yanayosemwa ninadhani siyo ya kweli," alisema Bw. Nnauye akipinga kauli habari zilizoandikwa vyombo vya habari zikinuu makada hao.
No comments:
Post a Comment