Na Addolph Bruno
BENDI kongwe ya muziki wa dansi nchini, Msondo Ngoma Music, imeshinda tuzo ya wimbo bora wa rhumba Afrika Mashariki na Kati katika mashindano yaliyofanyika
mjini Nairobi, Kenya mwishoni mwa wiki.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Msemaji wa bendi hiyo, Rajabu Mhamila 'Super D', alisema ushindi huo umetokana na kazi nzuri ya wimbo wa Kalunde ulioimbwa na aliyekuwa mwanamziki wa bendi hiyo, marehemu Tx Moshi Wiliam.
Alisema katika shindano hilo bendi, mbalimbali kutoka Afrika Mashariki na Kati, zilishiriki, ambapo ushindi wao ulishuhudiwa na Mkurugenzi wa bendi hiyo, Said Kibiriti na mwanamuziki Roman Mng'ande.
Alisema bendi nyingine zilizoshiriki ni Akudo Impact kutoka Tanzania kupitia wimbo wake wa Yako wapi Mapenzi na TP OK Jazz kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Alisema mashindano hayo yaliandaliwa na taasisi inayojihusisha na masuala ya muziki ya nchini Kenya na kuongeza kuwa, bendi yao imeanza mazoezi jana kuandaa nyimbo zao mpya na kuzirekebisha baadhi za zamani.
No comments:
Post a Comment