23 August 2011

'Serikali iunde chombo kisimamie mauzo ya sanaa'

Na Humphrey Shao

MASHIRIKISHO ya Sanaa nchini yameitaka serikali kuunda chombo kitakachopewa mamlaka ya kusimamia shughuli za mauzo ya kazi za sanaa kama
ilivyo katika biashara zingine.

Hayo yameelezwa na viongozi hao ambao waliofika katika Jukwaa la Sanaa kuchambua kiasi cha fedha kilichotengwa kwa ajili ya maendeleo ya sanaa hapa nchini kutokana na bajeti ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa mwaka 2011/12.


Mmoja viongozi hao kutoka Shirikisho la Sanaa za Ufundi, Adrian Nyangamale alisema serikali haijajipanga katika kupanga na kuendeleza michezo na sanaa chini .

"Wizara ya Habari , Vijana na Michezo imetengewa  sh. bilioni 18 kati ya hizo sh. bilioni 14 zinatumika kwa ajili ya mishahara na posho huku sh. milioni tatu kwa ajili ya maendeleo, huu ni utani kwani wizara hii ina idara kubwa nne na mashirika ya umma 12 bado wasanii hakuna maendeleo hapa,'' Nyangamale.

Mtoa mada mwingine kutoka shirikisho la muziki, Chemundu Gwao alisema kitendo hicho cha kupitisha bajeti finyu kimetokana na uelewa mdogo wa wabunge wa bunge letu juu ya umuhimu wa sanaa na michezo hapa nchini.

Alisema hii imejidhihirisha pale tulipo kutana na wabunge mbalimbali na kukiri wazi kuwa hawatambui hali halisi ya mchango wa sanaa katika taifa kutokana na kutopewa elimu sahihi juu ya mapato ya sanaa katika taifa hili.

"Tulikutana na waziri mkuu tukakaa naye chini kwa takribani muda wa saa manne ndio alipoelewa kuwa sanaa ni zao ambalo linaweza kuleta mabadilko kwa taifa hili hali iliyopelekea waziri mkuu kuagiza tuandae kongamano la kuwaeleimisha watendaji wote wa serikali kuu umhimu wa sanaa katika kuongeza pato la taifa" Alisema Chemundu.

Alisema kuwa serikali aina dhamira ya dhati ya kuweka mfumo wa mauzo katika hali nzuri na wasaniikulalamika wananyonywa lasivyo wanatakiwa kuhiamisha Cosota kutoka wizara ya viwanda na biashara hadi wizara ya inayo husika na wasanii moja kwamoja.

Alisema sh. bilioni tatu zilizotengwa kwa maendeleo ya michezo na sanaa nchini ni kichekesho kwani fedha hizo zinafaa kwa watu wa utamaduni peke yake hapo bado ujagusa kundi la vijana.

Alisema wizara hiyo ina kundi la vijana amabalo ndio idadi kubwaya nguvu kazi ya taifa hili lakini fedha za maendeleo ambazo zimetengwa kwa maendeleo kwa shughuli zote ni sawa na kumtumbukiza tembo katika mtungi wakati aenei.

No comments:

Post a Comment