MADRID, Hispania
MSEMAJI wa kocha wa timu ya Real Madrid, Jose Mourinho, ameviambia vyombo vya habari vya Hispania, bado hajamwomba radhi kocha aliyemtia kidole
jichoni, wakati wa mechi ya fainali ya Kombe la Supercopa ambayo timu yake ilifungwa na Barcelona.
Alhamisi wiki iliyopita, picha za televisheni na picha zilizopamba kurasa za mbele za magazet,i zilimwonesha kocha huyo mreno, akimtia kidole jichoni msaidizi wa Kocha wa Barcelona, Pep Guardiola, Tito Vilanova wakati wachezaji wa timui hizo mbili wakikwaruzana uwanjani.
Baada ya tukio hilo, picha hizo zilipamba kurasa karibu za magazeti yote na kuzua hali isiyo ya kawaida kwenye vyombo vya habari.
"Jose haombi radhi, yupo wazi kwamba, alikuwa akiitetea timu yake ya Real Madrid," msemaji wa kocha huyo, Eladio Parames, alikaliliwa akilieleza gazeti la dailies El Mundo na AS.
"Hajali ambacho vyombo vya habari vinakieleza, jambo la msingi kwake ni kile ambacho mashabiki wa Real Madrid wanakiwazia," aliongeza msemaji huyo.
Parames aliyaambia magazeti hayo kuwa, Mourinho alikuwa akijibu shutuma na vurugu alizokuwa akifanyiwa kutoka benchi la Barcelona.
Kashikashi hizo kati ya makocha hao, liliibuka mwishoni mwa mechi hiyo iliyofanyika kwenye Uwanja wa Nou Camp, ambapo Barcelona iliibuka na ushindi wa mabao 3-2, yaliyoifanya itwae taji hilo kwa jumla ya mabao 5-4, likiwa kombe la kwanza msimu huu.
Katika rabsharabsha hizo, wachezaji walizozana uwanjani na picha za televisheni zikamwonesha Mourinho akimfuata Vilanova na kumtia kidole jichoni, wakati Mourinho akiondoka, Vilanova akamsukumia kibao kizito mgongoni.
No comments:
Post a Comment