MILAN, Italia
TIMU ya AC Milan imesema kuwa, itaanza kutetea ubingwa wake wa ligi ya Serie A, bila beki wake wa kushoto, Taye Taiwo, baada ya Mnigeria huyo aliyesajiliwa
msimu huu kutenguka kifundo cha mguu.
Shirika la Habari la Ufaransa (AFP), liliripoti jana kuwa, timu hiyo ilitoa taarifa juzi, ikisema kuwa, Taiwo, ambaye amesajiliwa bila ada baada ya kusota kwa muda wa miaka sita katika klabu ya Marseille ya Ufaransa, alikumbwa na majeraha hayo Jumapili katika mechi ya kuwania Kombe la Berlusconi, iliyowakutanisha na Juventus, atakuwa nje ya uwanja kwa mwezi mmoja.
Kabla ya kukumbwa na majeraha hayo, mchezaji huyo mwenye umri wa wa miaka 26, tayari alionywa na na kocha wake mpya, Massimiliano Allegri, kuwa ajifunze jinsi soka la Italia linavyochezwa.
Katika hatua nyingine, mshambuliaji kutoka Sweden, Zlatan Ibrahimovic yupo shakani kucheza mechi ya kwanza dhidi ya Cagliari itakayofanyika mjini Sardinia, baada ya kuumia kifundo cha mguu wa kushoto.
No comments:
Post a Comment