LONDON, Uingereza
KOCHA Arsene Wenger, ameingia katika soko la kununua wachezaji dakika za mwisho akitaka kuimarisha timu yake ya Arsenal.Wenger ametuma ofa ya pauni
milioni 6.2, ambayo imekubaliwa ili kumpata beki wa kushoto kutoka kutoka Brazil, Andre Santos.
Pia ameingia katika foleni ya kutaka saini ya winga wa Chelsea anayetokea Ufaransa ambaye anauzwa kwa pauni milioni 8, Florent Malouda.
Wenger anataka kuimarisha timu yake ambayo Jumapili ilipata kipigo cha mbwa mwizi cha mabao 8-2, kutoka kwa Manchester United katika Uwanja wa Old Trafford.
Pia ametoa ofa ya pauni milioni 7 kwa ajili ya kupata saini ya beki wa kati wa Chelsea, Alex ambaye anatoka Brazil, ilielezwa juzi huku ikielezwa kuwa pia ana mtamani kiungo Yossi Benayoun.
Huku dirisha la Usajili likifungwa leo usiku, Wenger anaonekana kama amenyoosha mikono kumpata mlinzi wa Bolton, Gary Cahill.
Mkataba uliokubaliwa ni beki wa timu ya Fenerbahce kwa ajili ya Santos mwenye miaka 28, hadi jana alitarajia kupimwa afya.
Chelsea inataka dau la pauni milioni 10 kwa ajili ya Alex mwenye miaka 29, lakini bodi ya Arsenal inaamini kuwa inaweza kumpata kwa dau pungufu.
No comments:
Post a Comment