*Ni kuhusu madiwani waliofukuzwa CHADEMA
*Tendwa: Diwani akiishafukuzwa ndio kikomo
*Mwanasheria: Mkuchika sasa amekiuka katiba
Na Gladness Mboma
WATENDAJI wa juu ndani ya serikali ya Rais Jakaya Kikwete wamezidi kutofautiana vikali na
kutoa misimamo inayokinzana, safari hii ikiwa ni zamu ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Bw. John Tendwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (TAMISEMI), Bw. George Mkuchika kuhusu sakata la madiwani wa CHADEMA waliofukuzwa uanachama mkoani Arusha.
Wakati Bw. Mkuchika akiruhusu madiwani watano waliofukuzwa na CHADEMA kuruhusiwa kuendelea kuhudhuria vikao vya baraza na kutakiwa kulipwa stahili zao zote, Bw. Tendwa ameshangazwa na uamuzi huo na kusema kuwa serikali haiwezi kutengua uamuzi wa chama.
Akizungumza na gazeti hili jana, Bw.Tendwa alisema kuwa alishangazwa na uamuzi huo wa Bw. Mkuchika na kusema kuwa Bunge au diwani akiishafukuzwa uanachama ndio kikomo cha uongozi na ili kurudishia uongozi ni lazima hoja itenguliwe na mahakama.
"Serikali haiwezi kutengua uamuzi wa chama, haiwezekani hata kidogo, na kama mtu siyo mwanachama hawezi kuwa na wadhifa wa kubunge au diwani ni nafasi za siasa," alisisitiza.
Bw. Tendwa alitofautiana na Bw. Mkuchika kwa uamuzi wake wa kuandika barua kwa Meya wa Manispaa ya Arusha Bw. Gaudence Lyimo kuhusu hatima ya madiwani ya kutaka waendelee kuhudhuria vikao vyote vya baraza na kulipwa stahili zote hadi mahakama itakapotoa uamuzi.
Alisema kuwa yeye mpaka sasa haamini kama kweli Bw. Mkuchika ameamuru madiwani hao waendelee na kuhudhuria vikao vyote vya baraza huku wakiwa wamevuliwa uanachama na kwamba ameingilia uhuru wa mahakama.
"Huwezi kutengua lolote la mahakama, kwa kuwa kufanya hivyo utakuwa umeingilia uhuru wa mahakama," alisema.
Alisema kuwa hata Meya wa Arusha alitakiwa kuangalia sheria zinasemaje badala ya kukubali kupelekwapelekwa, kwa kuwa kesi hiyo iko mahakamani walichotakiwa kusubiri ni uamuzi wa mahakama pekee, ambao ndio yenye mamlaka ya kuwarejeshea uanachama au la.
Hivi karibuni, Bw. Mkuchika alidaiwa kukiuka Katiba ya nchi kutokana na kuandika barua ya kuruhusu madiwani watano waliofukuzwa na CHADEMA kuruhusiwa kuendelea kuhudhuria vikao vya baraza na kutakiwa kulipwa stahili zao zote.
Akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki baada ya kuahirishwa kwa kesi ya viongozi wa chama hicho katika Mahakama Kuu Mwanasheria, Bw. Method Kimomogolo alitoa kauli hiyo baada ya Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Willibrod Slaa kuonyesha nakala ya barua iliyotoka kwa Bw. MKuchika yenye kumb Na. HA 23/235/01/16 ya Agosti 23 mwaka huu iliyotumwa kwa Meya wa Manispaa ya Arusha, Bw. Lyimo kuhusu hatima ya madiwani hao.
Nakala ya barua hiyo ambayo ilibeba kichwa cha habari kisemacho: "Kuvuliwa uanachama hivyo kukosa sifa ya kuwa diwani huku mwisho wa barua hiyo ikisema kuwa 'kutokana na na madiwani hao watano kufungua kesi na kuiomba mahakama kuwarejesha uanachama wataendelea kuhudhuria vikao vyote vya baraza na kulipwa stahili yote hadi mahakama itakapotoa uamuzi'.
Bw. Kimomogolo alisema maamuzi yaliyofikiwa na Bw. MKuchika yalikiuka Katiba ya Muungano kwa vile mtu anayehitaji kugombea uongozi katika nafasi yoyote ni lazima awe na dhamana ya chama.
Alisema kuwa vipengele vingine vinaweka bayana kuwa katika suala la urais, ubunge na udiwani utakoma pindi chama kilichomwekea dhamana kitaondoa dhamana yake na kusema kwa kuwa tayari CHADEMA ilikwishaindoa dhamana kwa madiwani hao sasa hawana sifa.
Bw. Kimomogolo alisema kuwa inashangaza kuona serikali iliyopinga mgombea binafsi mahakamani na kushinda kesi, inakuja kuwatambua madiwani ambao mdhamini wao wamekwishawafukuza ambaye ni CHADEMA.
"Kwenye kesi aliyofungua Mchungaji Christopher Mtikila, ambapo mahakama imeamua hakuna mgombea binafsi, hivyo maamuzi yanayofanywa na madiwani hao kwenye kwenye vikao vya baraza nayo ni batili na posho wanazopokea ni wizi na anayewapa atawajibika kuzilipa,"alisema.
Naye Dkt. Slaa alisema kuwa alishangazwa na maamuzi hayo kwa kuwa madiwani hao walikwishavuliwa uanachama na kupelekea kukimbilia mahakamani ili kurejeshewa uanachama wao hivyo iwapo waziri ataendelea kuwatambua wakati chama hicho kiliondoa dhamana ni kukiuka taratibu za sheria.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo,Bw. Estomii Chang'a alikiri kuipata barua hiyo na kwamba anachokitekeleza ni maamuzi hayo yaliyotoka ngazi za juu.
Madiwani waliofukuzwa CHADEMA baada ya kukaidi maamuzi ya Kamati Kuu yaliyowataka kujivua nyadhifa walizopata kupitia muafaka walioingia bila baraka za chama hicho na kata zao kwenye mabano ni Naibu Meya Bw. Estomii Mallah (Kimandoli),Bw. Charles Mpanda (Kaloleni),Bw. Ruben Ngowi (Themi) na Bibi. Rehema Mohamed (Viti Maalum).
urais, ubunge na udiwani utakoma pindi chama kilichomwekea dhamana kitaondoa dhamana yake na kusema kwa kuwa tayari CHADEMA ilikwishaindoa dhamana kwa madiwani hao sasa hawana sifa.
ReplyDeleteHICHO KIFUNGU KIONDOLEWE KATIKA KATIBA. MBUNGE AKISHACHAGULIWA ANAKUA MBUNGE WA WANANCHI WOTE KATIKA JIMBO NA SIO MBUNGE WA CHAMA KILICHOMWEKEA DHAMANA. HIVO AENDELEE KUWA MBUNGE AU DIWANI HADI MWISHO WA KIPINDI CHAKE CHA UCHAGUZI
NI VIZURI KUIGA MIFANO NA NCHI ZINAZOONGOZA KWA DEMOKRASIA
mtoa maoni kama unataka kifungu hicho kiondolewe tulilie tupate katiba mpya.Kwa katiba ya sasa tuliyo nayo ndiyo iliyotufikisha hapa.Serikali ndo ya kwanza kuvunja sheria pale inapoona ina maslahi yake.Kama walikataa mgombea binafsi je Rais,mbunge au madiwani wakivuliwa uanachama watasimama kwa dhamana ya chama kipi cha siasa???????????????
ReplyDeleteTuombe ufahamu wa kuelewa na kusimamia yale tunayoamini kwa kufuata sheria vinginevyo tutaendelea kusikia na kuona mengi yakuchefua maendeleo ya nchi na wananchi wake
Hii ni sheria iliyopo kama huna back up ya chama unawakilisha wanachama wa chama gani. Hatuwatambui hao madiwani na kama mnawapa pesa jiandaeni kulipa na viboko juu. Stop politicizing legal issue!
ReplyDeleteHii ni manifistation nyingine tena inayozidi kuonyesha arrogance na ignorance ya baadhi ya mawaziri wa CCM. Nashangaa kwa nini huyu Rais wetu asimfukuze kazi Waziri Mkuchika kwa kuikuka katiba ya nchi? Katika kiapo chake, nadhani aliapa kuilinda katiba ya nchi. Haya anayoyafanya sasa ni kuidharau katiba aliyoiapia kuilinda. Kwa msingi huu, Mkuchika hafai kuendelea kuwa Waziri. I think its high time our President became serious in handling and conducting his office according to the Constitution. Hii biashara ya Rais kuongoza nchi kiswahiliswahili na kienyeji bora sasa isimame kwa heshima ya Ofisi yake na nchi kwa ujumla. Mhe JK, kumbuka Urais ni taasisi na sio wa kwao binasfi. Wake up and play your part!
ReplyDeleteHuu ukweli unajulikana hata mkuchika mwenyewe anajua sana tu, ila kuna mchezo mchafu wa kisiasa unaochzwa hapa, Chadema ilisha wafukuza uanachama, na ni mahakama ndio yenye uwezo wa kutengua huo uamuzi siyo mkuchika, hii inadhihirisha kuwa uasi wa hawa madiwani uliasisiwa na CCM, na wanapewa maagiza yote toka CCM.
ReplyDeleteNi kweli hakuna Rais, mbunge wala diwani atakayechakuduliwa bila kuwa na chama kinachomwakilisha kwa mujibu wa katiba ya nchi. na shangaa kuona blaa balaa zinapata nafasi, eti wataendelea kuwakilisha wananchi wakati wameshatupwa na chama walichokuwa wakikiwakilisha.
ReplyDeleteinashangaza zaidi pale Waziri mwenye dhamana, tena mwenye uzoefu wa kiuongozi kwa muda mrefu kufanya mambo kama kiini macho...huenda hajui anachokifanya kama walivyo viongozi wengi nchini, wanaomwaharibia Rais JK uongozi wake na kuonekana hawezi, kumbe vichwa vyao ndiyo tatizo.
Tunahitaji umakini, uwajibikaji na uweledi katika uongozi siyo masuala ya kutenda bila kujua unachokitenda. kipindi cha 'funika kombe mwanaharamu apite' kimepitwa na wakati, tujihadhari nacho. Njuki
Ni kweli tunaona wazi kuwa suala zima liliasisiwa na CCM, ndio maana lazima wawabebe sasa ila kosa wanasahau sheria na katiba ya nchi inasema nini? Huwa hawapitii vitabu ni wavivu kusoma hao, Serikali yenye mkingamano wa Maamuzi ya Viongozi ni hatari kwa ustawi wa taifa, Angalia , Luhanjo, Mkuchika na Msekwa wanavyotoa kauli tofauti, SAsa ni wakati ambao Rais inabidi aonyeshe makali kumtoa waziri kafara kwa kutoa kauli Pingana, na chanyifu
ReplyDeleteIt seems Tanzanians are not serious! Huyu anayekiuka katiba ya nchi anastahili awajibishwe. Utawala wa sheria uko wapi? Kwa nini tusimchape viboko Hadharani? Katiba si kitu cha kuchezeachezea.
ReplyDeleteHakuna cha Rais wala mbunge, wote mbumbumbu wa katba! Kama unabisha, huyo jk anayejiita dkt, kasema nn juu ya mkuchika? tba! Kama unabisha, huyo jk anayejiita dkt, kasema nn juu ya mkuchika?
ReplyDeletemimi naona George Huruma Mkuchika anataka wananchi waanze kumchunguza kwa maamuzi yake ambayo amekuwa akiyatoa kwa watendaji wake wa Halmashauri nchini. katika siku za hivi karibuni amekuwa akitoa maamuzi mazito mno kama yeye ni Rais wa nchi hii. hii ikiwa pamoja kuwasimamisha wakururugenzi bila kufuata utaratibu na hii ya kuwarudisha madiwani wa CHADEMA bila kufuata kanuni sheria na taratibu kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kinachoshangaza madiwani wale ni wa Chama mbadala ambapo kwa kawaida katika siasa ushindani angechukua uamuzi huo kuwa nifaida kwa chama chake na angechukua hiyo nafasi kuanza angalau kuwashawishi waingie kwenye chama chake kama anaona wanauzika. misimamo mikali ya chama ilikuwa inaonyeshwa tu wakati wa chama kimoja ambapo kulikuwa na uhakika kuwa idadi kubwa ya wananchi walioiweka serikali wanatoka chama tawala. naomba nimwonye Mkuchika wananchi wa Tanzania hatutaki mauaji yaliyotokea arusha yatokee tena, damu ya watu watatu waliokufa Arusha bado inakulilia mkuchika. usishangae kuona wote waliohusika na sakata hilo wakiwa hai au wamekufa wanajibu tuhuma hizo. watanzania wako tayari kufukua makaburi yao ili iwe adhabu ya ufedhuli walioufanya.
ReplyDeletenamkumbuka Jobu lusinde aliyetaka wabunge wapimwe akili nadhani alikuwa anamaana mawaziri wapimwe kwa sababu kichaa kina mwanzo na kingine kinafuatana na umri. mimi nadhani ndugu yetu mkuchika akapimwe haraka sana vunginevyo ataleta maafa. Mheshimiwa Jakaya Mlisho Kikwete Umepewa penalti ipige funga goli kwa kuliondoa jitu linalofanya mambo ambayo wewe binafsi naamini unayasimamia, unayapenda na unayaamini ili asikupake matope.
CHADEMA chapa mwendo mmetake advantage ya constitution iliyopo hongereni.
huyu mzee kawa kama Makamba sasa kwani anajiona na yeye ni kama yuko juu ya sheria na hii ni uzembe wa raisi wetu kwenye kusimamia majukumu yake na kuwawajibisha wale wasiotekeleza wajibu wao ipasavyo kama Mkuchika.
ReplyDeletehapa tukisema mawaziri huwa wanakurupuka tuaambiwa tunaibeza serikali na kusahau memngine, kwenye hili hata kama niko CCM acha wanitoe kwenye uanachama Mkuchika kachemsha na anapaswa awajibishwe ikiwezekana atolewe uwaziri kwani tulipopinga mgombea binafsi CCM ndiyo tulikuwa agenda zetu kumpinga Mtikila na yeye Mkuchika alimbeza sana Mtikila leo kajisahau, huyu hana maana kama Msekwa.Uchafu ulioutema unaumeza tena.
ReplyDeleteKikwete rais wetu mbona umelala?nchi inaenda wapi?unakuwa kama haupo?hao marafiki zako uliowajaza kwenye baraza la mawaziri ndio wanaokuangusha.na kwa sababu ni machamalee hauna ubavu wa kuwakemea!haya endelea utaona matunda ya kukaa kwako kimya!
ReplyDelete