Na Mwali Ibrahim
KAMPUNI ya Simu ya Airtel, leo inatarajia kukabidhi msaada wa vitabu kwa shule tano za mkoa wa Morogoro, ikiwa ni mkakati wake wa kusaidia sekta ya
elimu.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Meneja wa Huduma za Jamii wa Airtel, Bi.Tunu Kavishe, alisema kila shule itapata vitabu vyenye thamani ya sh. 1,000,000.
Alisema msaada huo ni mwendelezo wa kampuni hiyo kusaidiaka sekta ya elimu ambapo mpango endelevu huku. "Kwa sasa tumeangalia mikoa ya Morogoro, Arusha, Mtwara, Mwanza na Dar es Salaam," alisema.
Bi.Tunu alisema tayari wameishaanza kutoa vifaa mbalimbali katika shule 800 za Tanzania Bara na Visiwani, ambapo sambamba na kugawa vitabu wamekuwa wakitoa misaada ya madawati kwa lengo la kuweka mazingira mazuri ya wanafunzi kujifunzia.
"Si kwamba tumebagua maeneo ya kutoa msaada huu, bali tulikaa na serikali wakatushauri maeneo ya kuanzia kuwa ni hayo, lakini sisi tuna mpango wa kufika mbali zaidi ili mpango huu ufike katika mikoa yote," alisema
Sambamba na kutoa msaada huo alisema Airtel imelenga kuwakomboa wanawake kwa kutoa elimu kuanzia ngazi ya chini, ambapo wameangalia zaidi Mkoa wa Mtwara, ambao unaonekana kuwa na idadi kubwa ya vijana wa kike wanaopata ujauzito na kushindwa kuendelea na masomo.
No comments:
Post a Comment