19 August 2011

TPA yakabidhi alama za walemavu barabarani

Na Willbroad Mathias

MAMLAKA ya Bandari  Tanzania (TPA), imekabidhi msaada wa alama mpya za usalama barabarani, ili kuwasaidia watu wenye ulemavu mbalimbali nchini kukabiliana na
ajali.

Msaada huo wenye thamani ya sh.milioni 4.5 ulikabidhiwa Dar es Salaam jana na Ofisa Mawasiliano Mkuu wa TPA,Bi.Janeth Ruzangi kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Usalama barabarani ya Watu wenye Ulemavu (NCPDRS),Bw. Jutoram Kabatelle, katika hafla fupi iliyofanyika makao makuu ya mamlaka hiyo.

Akikabidhi msaada huo ,Bi. Ruzangi alisema wamefikiwa uamuzi huo, baada ya kuombwa na NCPDRS ili waweze kuondokana na adha wanazokumbana nazo wakati wa kuvuka barabara.

"Sisi kama TPA baada ya kupokea maombi ya kamati tumeamua kurudi katika kazi yetu ya kuisaidia jamii,"alisema Bi. Ruzangi.

Alisema alama hizo zinahusisha walemavu wa aina zote. Alisema pamoja na msaada huo, mahitaji bado ni mengi na kuwa msaada huo  hauwezi kutosheleza wilaya tatu za Mkoa wa Dar es Salaam. Alitoa  mwito kwa  mashirika na taasisi nyingine kujitokeza kutoa msaada wa aina hiyo.

Kwa upande wake mbunufu wa alama hizo, Bw.Kabatele, aliishukuru TPA kwa msaada huo.

Alisema wana imani alama hizo zitaheshimiwa pindi zitakapozinduliwa  mwezi ujao, kutokana na kuwa tayari zilishapitishwa bunge tangu mwaka jana.
   


No comments:

Post a Comment