28 July 2011

Uuzwaji wa UDA watinga mahakamani

Na Rachel Balama

KAMPUNI ya Simon Group imefungua kesi ya madai dhidi ya Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) na Consolidated Holding Coorporation kupinga kukatishwa mkakaba
baina yake na mdaiwa wa kwanza.

Kesi hiyo ambayo imefunguliwa katika Mahakama Kuu ya Biashara iliahirishwa jana ili kuona kama kuna uwezekano wa suala hilo kumalizwa nje ya mahakama.

Juzi, Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dkt. Didas Masaburi alitangaza kuvunja Bodi ya UDA na kusimamisha uongozi wake kutokana na ubadhirifu wa mamilioni ya fedha, huku akiunda Kamati kuchunguza mkataba wa kuuziana hisa kati ya shirika hilo na kampuni hiyo.

Kesi hiyo inayosikilizwa na Jaji wa Mahakama Kuu ya Bishara, Bi. Agnes Bukuku, ilitajwa jana na kupangiwa tarehe nyingine  ya kutajwa, Septemba 7, mwaka huu.

Baada ya kusikiliza pande zote mbili, Mahakama iliahirisha kesi hiyo ili kuona kama suala hilo linaweza kumalizwa nje ya mahakama kati ya mdai na wadaiwa.

Kampuni ya Simon Group imefungua kesi mahakamani ikiomba itamke kuwa yeye anastahili kumiliki hisa zote ambazo hazijatolewa za UDA na kuwa kukatishwa kwa mkataba baina yao ni kosa kisheria.

2 comments:

  1. wizi huu wa mali za umma utaisha lini?

    ReplyDelete
  2. Kwani hamjui kama mmiliki wa Simon group ni mtandao wa mtoto wa Kiketwe Ridhiwan? someni alama za zanyati.

    ReplyDelete