28 July 2011

Pinda anusuru bajeti Kilimo

Na Godfrey Ismaely, Dodoma

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda juzi aliinusuru Bajeti ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika baada ya asilimia kubwa ya wabunge wa CCM na vyama vya upinzani
kushikilia msimamo wa kutoikubali kwa madai kuwa hailengi kumkomboa mkulima wala kulitendea haki zao la pamba.

Msimamo huo wa kuikataa bajeti hiyo ulifikiwa na baadhi ya wabunge baada ya Mbunge wa Nzega, Dkt. Hamis Kigwangalla (CCM) kutoa hoja ya kuondoa shilingi katika mshahara wa waziri kwa kuwa serikali imekuwa haitoi bei ya kuridhisha kwa zao hilo kila mwaka huku wafanyabiashara wakinufaika kwa kujipangia bei.

Baada ya wabunge kusimama na kuonesha msimamo wao wa kutaka kauli ya serikali ni lini bei ya pamba itatangazwa kufikia sh. 1,000 hadi 1,500 kwa kilo, ndipo Bw. Pinda alilazimika kusimama na kutoa ufafanuzi juu ya hoja hiyo.

Alisema zao hilo ni kama mazao mengine ya biashara na kuongeza kuwa wakulima wote ni muhimu ila bei zinashuka kutegemeana na soko la dunia.

“Wadau mlipokutana Mwanza bei ilikuwa nzuri sh. 1,100 na sisi hatupangi bei, lakini katika kipindi kifupi ukweli umejitokeza. Mnataka serikali iseme nini? .

“Waziri Maghembe amesema serikali itajitahidi bei ya pamba isishuke chini ya sh 800. Tupeni nafasi serikali na wadau kushauriane katika hili tuone tunamaliza tatizo hili,” alisema Pinda

1 comment:

  1. Mh. Pinda naona sasa kauli zako haziashirii kuwa mtoto wa mkulima. Stand critically like Chavez of Venezuela Please!

    ReplyDelete