28 July 2011

Madiwani watano Arusha waomba radhi

Na Flora Amon

MADIWANI tano kati ya 10 wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutoka Arusha wameandika barua ya kuomba radhi baada yakutakiwa kufanya
hivyo na chama hicho.

Hayo yamebainisha jana na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dkt. Willibrod Slaa kuwa mpaka sasa amepokea barua za madiwani tano ambao wameomba msamaha kama ilivyotakiwa katika barua walizoandikiwa.

Alisema kuwa madiwani hao wote waliandikiwa barua mbili kila mmoja, moja ikiwa ya kujiuzulu na nyingine ya kuomba radhi.

Aliongeza kuwa kilichokuwepo si kwamba madiwani wote walitakiwa kujiuzulu, isipokuwa wale watatu walioingia kwenye maridhiano batili ndio kutakiwa kuachia nafasi hizo.

Kwa mujibu wa Dkt. Slaa kati ya madiwani 11, mmoja aligoma kuingia muafaka wakati wenzake 10 walikubali na watatu kati yao kupewa nyazifa, hivyo kutakiwa kuziachia nyazifa hizo kwani muafaka haukutambuliwa na chama hicho.

Alisema kuwa kuna gazeti moja liliandika kuwa madiwani hao wanatuhumiwa kwa rushwa, jambo ambalo amekanusha na kusema siyo kweli.

"Mimi sielewi nyie waandishi wa habari mna ajenda gani na Chadema kwa sababu hili swala la madiwani sisi kwetu siyo kubwa lakini nashangaa linakuzwa mkitegemea Chadema itasambaratika. Haitatokea, haitowezekana kwani Chadema tunaongozwa na katiba," alisema.

"Mnafuatilia suala la Arusha wakati wabunge wanatajwa kuwa wala rushwa, hayo ndiyo mambo muhimu ya kufuatilia na siyo mgogoro wa madiwani kila siku," aliongeza.

6 comments:

  1. tatizo walikufa watu lazima tufuatilie

    ReplyDelete
  2. Safi sana huo ndo uzalendo ukijua umefanya kosa kubali then tubu big up kwa hao madiwani waliokubali makosa yao ni mfano wa kuigwa

    ReplyDelete
  3. wasenge tu hawa wanatuzingua slaa hana lakufanya sasa hivi mbowe ashamchinjia baharini anatuletea ukumakuma wake aondoe kelele, hao waliopkubali wote makuma tu kama slaa mmwenyewe

    ReplyDelete
  4. huyu anayetumia lugha ya matusi kwakweli hasitahili kabisa ktk jamii ya Ktz.lakini kama jamii hatushangai sana maana serikal ya ccm inaundwa na watu wanamna hiyo ni wajinga wajinga tu.sasa la kujiuliza hv huyu naye anafamilia na watoto?Nina wasiwasi na HISA ya akili yake maana hata tahira hawezi kuongea maneno yanamna hiyo.Atoe maneno ya kujenga na siyo huo upumbavu wake.

    ReplyDelete
  5. Hao ni CCM tu kwani wanaonyesha jinsi wanavyoteseka kwa ndani na PEOPLES`S POWER.
    Wangojee Igunga waone nani zaidi.

    ReplyDelete
  6. inakuaje site ya gazeti kama hili tena linaheshimika na jamii ya kitanzania mtu anaandika matusi na mnayaachia jamii iendelee kuyasoma...tafuteni means ya kuzuia uchafu km huo

    ReplyDelete