04 July 2011

Tutaanika mafanikio yote ya CCM Julai 7- NAPE

Na Benjamin Masese

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimejipanga kujibu mapigo kwa kuanika mafanikio yake yote tangu kuundwa kwake Julai 7 mwaka 1977, katika maadhimisho ya miaka 34 ya
chama hicho Julai 7, mwaka huu ili kuondoa kauli potofu kuwa  hakuna kilichofanywa na utawala wake.

Akizungumza na wandishi wa habari Dar es Salaam jana, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi (NEC) Bw. Nape Nnauye, alisema CCM itafanya hivyo kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania Bara.

Alisema baadhi ya watu wamekuwa wakipotosha ukweli na kuwadanganya watanzania kuwa katika miaka hiyo 50 hakuna kizuri kilichofanywa na CCM iliyotokana na Chama cha Tanzania Afrika National Union (TANU) iliyounda mwaka 1954.

Alisema CCM imeamua kufanya shughuli hizo kwa kutumia kauli mbiu ya 'uhuri na kazi' iliyowahi kutolewa na Hayati baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere, siku ya mkesha wa uhuru wa Tanganyika mwaka 1961.

Alisema kauli hiyo iliwataka wananchi kujiandaa kufanya kazi kwa bidii ili kujiletea maendeleo yao wenyewe na nchi kwa ujumla na kwamba CCM inaendelea kufanya shughuli za jamii hadi siku hiyo ya maadhimisho.

Bw. Nnauye alisema, maadhimisho hayo ya mwaka huu yatafanyika nchi nzima kuanzia ngazi ya matawi hadi mkoa na kufanya shughuli mbalimbali kama usafi wa mazingira, kusaidia ujenzi, kupanda miti na kutembelea wagonjwa hospitalini.

Alisema usiku wa kuamkia Julai 7, vijana wa CCM nchi nzima watakutana maeneo mbalimbali kufanya shamrashamra za kuashiria kuzaliwa kwa TANU ambapo asubuhi watashiriki katika matamasha na kujadili masuala yenye faida kwa kata, wilaya, mkoa na kitaifa kwa ujumla.

Alisema katika majadiliano hayo watakumbushana mafanikio yaliyopatikana ndani ya kipindi cha miaka 50 kwa kila wilaya na mkoa.

"Sherehe hizi zitaanza usiku wa Julai 6 kwa vijana wa CCM kutoka sehemu mbalimbali kukutana na kusherehekea ikiwa ni pamoja na kufyatua mafataki saa sita usiku kama ishara ya kuzaliwa TANU.

Lakini kwa mkoa wa Dar es Salaam Rais Jakaya Kikwete, atashirikiana na vijana na asubuhi yake atakutana na mabalozi wa nyumba 10 na kuzungumza nao,"alisema.

Alisema watu wanaobeza kuwa hakuna mabadiliko ndani ya miaka ya uhuru wa Tanzania 50 wanatakiwa kufikiria kwanza na kusoma historia kabla ya kuzungumza kwa kuwa historia itawahukumu.

Alisema wanatakiwa kujadili hali iliyokwepo wakati nchi inapata uhuru na kufananisha hali ilivyo sasa katika sekta za barabara hususan za lami, vyuo vikuu, hospitali, viwanda, maendeleo, nyumba, elimu na vitu vingine.

Alisema Julai 7, itakuwa mwisho wa kauli za watu hao kwa kuwa mafanikio yote yataelezwa kwa kila wilaya, mkoa na taifa kwa ujumla.

5 comments:

  1. MOJA YA MAFANIKIO MAKUBWA YA CCM NI KUZALISHA MAFISADI WENGI AMBAO WAMEWEZA KUJILIMBIKIZIA MALI NA KUINGIA MIKATABA MIBOVU NA WAWEKEZAJI.

    ReplyDelete
  2. Mafanikio makubwa ya CCM katika Miaka 50 ya kupata UHURU ni kufanikiwa kwako kutuweka GIZANI katika karne hii ya sayansi na teknolojia. Hongereni sana CCM.

    ReplyDelete
  3. Shamrashamra zitaanza usiku wa manae? Gizani! Ni mafanikio ya CCM kuwa gizani kwa miaka 50?

    ReplyDelete
  4. barabara, shule, viwanda, mnamiliki magari, tv, mnavaa vizuri, nini mnataka na bado tunamikakati yakinifu ya kuwaletea wananchi maendeleo, program ya kilimo kwanza, tunajali wakulima na wafanyakazi, ni mamabo mengi tunafanya jaribuni kuona na hayo.

    ReplyDelete
  5. mafanikio makubwa ni mfumo kristo kushtadi Tanzania, ubalozi wa papa, tume ya majeshi ya kikatoliki, chama cha kanisa na ilani ya uchaguzi ya kanisa, waumini sumbawanga kufukuzwa dini kwa kuchagua ccm.
    Waisla miaka 50 ya ccm ni ibra kwetu kuwakumbuka wazee wetu waliojitoa muhanga kuuping mfumo kristo tangu jihad ya majimaji mpaka tukapata uhuru.Nyerere amevalishwa suruali ya kwanza na waislam lkn akaja kuwageuka someni kitabu cha dokta John Sivalon kanisa katoliki na siasa Tanzania kama kweli Nyerere ni baba wa taifa nasi kanisa. leo wazalendo wameachwa hawatajwi tena tunataka historia sahihi ya uhuru iandikwe sio hii ya kanisa.
    WANAHISTORIA INABIDI KUTAFUTA HISTORIA SAHIHI YA TANZANIA VINGINEVYO UKWELI UKIJA DHIHIRIKA ITAKUWA AIBU SANA. KUMBE HATA MKWAWA ALIKUWA MUISLAM, USTADH SONGEA, HASAN CHIBRUMA, BUSHRI BIN SULTAN N.K WALITOA MUELEKEO WA KUPAMBANA NA MADHALIMU WA KIKOLONI. KAMA UNABISHA MUULZE JOHN RUPIA WALIKUW WAKRISTO WANGAPI KWENYE TANU WAKATI WAKUDAI UHURU WA TANGANYIKA?

    ReplyDelete