04 July 2011

Mgambo, Polisi watimuliwa kwa mawe Mpanda

Na Sammy Kisika, Mpanda

ASKARI Mgambo wa Halmashauri ya Mji wa Mpanda mkoani Rukwa, pamoja na askari Polisi wilayani
humo, wamenusurika kuuawa kwa kupigwa mawe na wananchi baada ya
kuzuka tafrani baina yao na Wafanyabiashara wa soko la Mpanda Hotel.

Askari hao walinusurika kufa wakati  wakiendesha operesheni ya kukusanya ushuru wa soko hilo kutokana na baadhi yao kutolipa ushuru kwa wakati.

Tukio hili lilitokea juzi saa 4. 00 asubuhi  sokoni hapo mtaa wa Majengo ‘B’ mjini hapa baada ya msafara wa mgambo hao kuwasilia eneo hilo wakiwa na mmoja wa mawakala waliopewa zabuni ya kukusanya ushuru katika soko hilo.

Baada ya kuwasili katika eneo hilo  wafanyabiashara hao walianza kuwarushia maneno makali kisha kuwashambulia kwa mawe askari hao waliokuwa wamefuatana na Polisi Koplo Musa na Mzabuni huyo wa kukusanya ushuru.

Wakati wakiwashambulia askari hao wafanyabiashara hao walikuwa wakipinga ongezeko la ushuru uliotangazwa kupanda kuanzia Julai Mosi mwaka juu.

Ushuru huo umepanda kutoka sh. 200 hadi 300 kwa wauza mboga na sh. 200 hadi 800 kwa wafanyabiashara wengine wakiwamo wauza mitumba wa soko hilo.

Awali wafanyabiashara hao waliwaambia askari hao kuwa hawako tayari kulipa viwango hivyo vipya na kuwataka waondoke katika eneo hilo la soko mara moja kabla hawajatangaza hali ya hatari kwao. 

Pamoja na tishio hilo askari hao waliendelea kuwasihi kulipa ushuru huo hatua ambayo iliwafanya wafanyabiashara hao waanze kuwashambulia kwa mawe hivyo kuwalazimu Mgambo na polisi huyo kutimua mbio na kupoteana.

Wakati wakitimua mbio kila mmoja alifuata njia yake wakisindikizwa na kelele za kuzomewa kutoka kwa wafanyabiashara wa soko hilo

Awali kabla ya kuponea chupuchupu askari hao walishindwa kufanikisha ukusanyaji ushuru katika soko kuku la mijini Mpanda walipogomewa na wafanyabiashara wa soko hilo ndipo
walipoamua kwenda kwenye soko la Mpanda hotel.

Akizungumza baada ya tafrani hiyo Katibu wa wafanya biashara wa soko kuu la Mji wa
Mpanda Bw. Amani Mahela, alisema wafanya
hawako tayari kulipa viwango vipya vya ushuru kwa kile alichokieleza kuwa ni kutoshirikishwa.

Alisema ameshangazwa na uamuzi wa Halmashauri ya Mji wa Mpanda kupanga viwango vipya vya ushuru bila kutoa taarifa kwa wafanyabiashara kama walivyokuwa wamekubaliana katika vikao vyao vya awali.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mpanda Bw. Enock Gwambasa, alisema
ameshangazwa na hatua ya wafanyabiashara hao kugomea kulipa ushuru wakati walishirikishwa katika mchakato wa kupanga viwango hivo vipya na kuhoji ni vipi wakatae kulipa.

“Nimeshangazwa nahao nduguzangu kwani mara yakwanza tulipangaushuru ufikeshilingi elfu moja wakapinga, na tukawaita hatimaye tukakubaliana kiwango kipungue kutoka elfu
mojahadishilingi mia nane kwa wafanyabishara wengine, wakati wale wauza mboga ulipungua kutoka penderkerzo laawali lashilingi mia tano hadi mia tatu, sasa wanafabnyafujo za nini kama sio matatizo !” alihoji Bw. Gwambasa.

Alisema yeye binafsi anaamini kuna shinikizo la baadhi ya watu ambao hakuwataja mara moja wanaopita chini kwa chini kuwashawishi Wafanyabiashara hao kugomea viwango hivyo vipya vya ushuru kwa maslahi yao binafsi.

“Kwa ufupi naweza kusema haya mambo ni mashinikizo ya kisiasa, kuna wanasiasa
wanataka kupata umarufu kupitia hii migogoro kwa kuwashawishi hawa wafanyabiashara kutolipa ushuru na sisi tunatarajia kukutana hii leo (jana) kulizungumzia suala hilo,” alisema.

2 comments:

  1. Halmashauri ikae na wafanyabiashara na kufikia muafaka kabla ya kutangaza bei mpya na pia waache kusingizia wanasiasa sio kweli huwezi kupandisha ushuru kwa asilimia mia nne toka 200 hadi 800. waache kuwaburuza wananchi watu wametulia wao wanaanza kuwataka kuleta vurugu mimi naona hawa halmashauri ndio wana nia ya kuchafua hali ya hewa

    ReplyDelete
  2. Hapo poa hao polisi ni njaa tuu zinawasumbua mbwa nyie kazi yenu kutumwa tuu, angalieni ndugu zenu wanakufa njaa mbona hamuwakamati viongozi mafisadi na wanao kula rushwa. Nenda Moshi ukaine askari wamebinafishisha barabara gari lina nunua njia wanajua makonda wa daladala watawaambia mimi askari akipigwa nafrahi maana hawana huruma hawa ni mbwa sana.
    safi sana wananchi kuthubutu

    ReplyDelete