26 July 2011

Tanesco yakata tamaa

*Yasema hali tete, ratiba ya mgawo yatupwa

Na Benjamin Masese

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema kuwa hali ya mgawo wa umeme nchini kwa sasa ni tete kutokana na uzalishaji wa nishati hiyo kuzidi kupungua
na kufikia hatua za mwisho za kuzimwa kwa mitambo.

Vile vile limesema kwamba halitaweza kufuata ratiba iliyotolewa awali ya mgawo wa umeme na hivyo kuwataka wananchi kukubaliana na hali iliyopo sasa hadi serikali itakapofanikisha mipango yake kuhusu suala hilo.

Hayo yalisemwa na Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Badra Masoud wakati wa mahojiano na gazeti hili kwa njia ya simu kuhusu kutofuatwa kwa ratiba ya mgawo wa umeme iliyotolewa awali ambayo imesababisha malalamiko kwa wananchi.

Bi. Masoud alisema kuwa ratiba hiyo imeshindikan kufuatwa kutokana na kiwango kidogo cha umeme kinachozalishwa ambacho kwa muda mwingine kipanda na kushuka, hivyo kuwapa wakati mgumu wa kuwahudumia wateja wake.

Alisema kuwa hakuna njia mbadala ya kuepusha tatizo hilo, kwa kuwa tayari limeshakuwa kubwa.

Kinachotakiwa sasa, alisema ni uvumilivu na subira wakati serikali ikiwa katika mchakato wa kuepusha nchi isiingie katika giza.

"...kwa hilo ni kweli hatuwezi kufuata ratiba tuliyoitoa awali kwa sababu ya kiwango cha uzalishaji kupungua kila wakati, yaani kinapanda na kushuka...sasa ukisema unafuata ratiba utasababisha migogoro, naomba wananchi watambue kwamba hali ni tete na tukubaliane na hali hii," alisema.

Hivi karibuni, vyombo vya habari vilisema makali ya mgawo wa umeme yameongezeka kutoka saa nane hadi 18 kwa siku katika mikoa mbalimbali ikiwemo Tabora, Kilimanjaro, Arusha na Dar es Salaam.

27 comments:

  1. Kwa kweli huu ni muda wa viongozi kuvua suti na kuvaa kama CHADEMA ili kuonyesha kwa vitendo upiganaji wa kweli wa kutuondloea balaa la kukatika umeme. Tatizo nchi imekosa maono siku nyinggggiii! Tunakazi, Kwaheri mi natumia mshumaa tuko enzi ya mawe, na ujima unakomaa! Asante CCM! TUNASHUKURU SANA!

    ReplyDelete
  2. Wenzetu Senegal wameandamana kupinga mgao wa umeme sisi bongo tunang'aa macho tu. Tufanye maandamano ya kuitoa hii serikali ya kisanii madarakani. Tuweke serikali yenye ubunifu. Siyo hawa wanawaza kupitisha bajeti kwa njia ya rushwa.

    ReplyDelete
  3. Njia ya haraka ilikuwaje Serikali iliweza kuihudumia na kukaa na mitambo ya IPTL kwa zaidi ya miaka 15 ishindwe leo ktk dharura muhimu kama hii? Mitambo ya IPTL imezimwa kabisa na ingeweza kuzalisha Meg 100 itatuwe hii dharura kwa mwezi huu na kama mgao basi wakate Osterbay,masaki kwa wakubwa na mjengoni dodoma sio kuwakatia watu walalahoi hata uwezo wa kibatari hawana wakikatiwa hao wakubwa watajuwa ukubwa wa tatizo tatizo n ngojera tokea 2006 leo wimbo ni huohuo kulikoni?

    ReplyDelete
  4. kwa nchi kama hii yenye vyanzo mbalimbali vya nishati kama solar,wind,hydro,makaa ya mawe,natural gas,uranium na vngnvyo eti nchi inaingia gizani!!!!!!! sh.....t!!!!1

    ReplyDelete
  5. watanzania tungoje nini sasa ikiwa daktari kamkatia tamaa mgonjwa?

    ReplyDelete
  6. Wabunge Chonde chonde, tunawategemea kuliko wakati mwingine wowote katika nchi yetu. Msidanganyike mpaka kieleweke. Nyie ndo mlobaki, Rais , Waziri Mkuu ni kama hawako coz hawana la maana zaidi ya story tu. Tafadhali piganeni kiume japo na wanawake wamo ndani. Tunaomba sana. Tunateseka sana bila sababu ila kuendekeza ujinga.

    ReplyDelete
  7. Tunaambiwa hili ni janga la kitaifa. Kama ukweli ndio huo, tunaiomba serikali iombe misaada haraka nje ya nchi kama inavyokuwa kwa majanga mengine(ya njaa, magonjwa nk)

    ReplyDelete
  8. kama tungejenga mabwawa ya kuhifadhi maji baada ya kuzalisha umeme matatizo yote haya yasingetupata, kipindi kama hiki cha ukame maji yaliyohifadhiwa ndiyo yangetumika kuzalishia umeme na kutumika tena na tena. Hakuna hata kiongozi mmoja mwenye wazo kama hilo badala yake kila mtu anazungumzia kukodi mitambo kwa kuwa hapo ndio kwenye 10%

    ReplyDelete
  9. hii ndio faida ya kudanganywa na t-shirt na kofia, so tuanacholalamika ni nini wakati hii serikali tumeipa ridhaa wenyewe hapo mwaka jana.Tunavuna tulichopanda wakujilaumu ni sisi wenyewe wala sio tanesco, tunadanganywa tunadanganyika hala tunacomplain this our foolish

    ReplyDelete
  10. mgonjwa wa kansa akiambiwa arudi tu nyumbani ni kuwa madaktari wameona mwisho umetimia.tanesco ni siasa tu watu fulani.hawataki kufikiri wanaua taifa.wanakiri taifa linakufa nao wako madarakani.kwa nini wasikimbie?ndo maana wananchi wakataka serikali mseto,ili akl za wengine ziingie kazini.kama ulimsikia pof.lipumba,jinsi tulivyo na vyanzo vingi vya umeme,lakn watu wanataka tu kukodi ili wapate ten paccce.akli za zimechoka zinasubir tu kukinga rushwa.hivi wanatupeleka wapi?huduma nyingi zimekufa kwa ajili ya umeme,sawa tu na kansa na ukimwi,hakuna matarajio,had mvua au ARV!

    ReplyDelete
  11. Sokoine Cousin!
    Acheni ujinga nyinyi! Mliamka wenyewe asubuhi kwenda kupigia kura WADUDU WAAHATIBIFU....!!! Halafu leo mnajifanya kulalamika...acheni upumbavu wananchi!

    Mimi nilipiga kura mara ya mwisho mwaka 1980 mara baada ya VITA YA UGANDA...niliwapigia kura watoto wa mjini (SOKOINE NA NYERERE).....Baada ya hapo siendi mpirani, sina kadi ya CHAMA chochote cha WADUDU WAAHARIBIFU (HUU NI UJUMBE KWA VYAMA VYOTE!!!!!!!!

    ReplyDelete
  12. Sokoine Cousin;

    Kwanza hao wapinzani hawana ADABU PIA! NI NJAA TU INAWASUMBUA.....BADALA YA KUKAA WAFANYE MAMBO YA MAANA... WAMEKALIA UJINGA WA SIASA TU.... NI KUKOSA ADABU KWA NCHI NZIMA NDO MAANA TUMEFIKIA HAPA!!! MKUBALI MSIKUBALI! HUO NDO UKWELI!! NCHI HAINA HATA MFUMO MMOJA COZ YA KUKOSA ADABUUUUU!!!! ELIMU INAZIDI KUSHUKA, KILIMO HAKUNA.. WANAJIFANYA "KILIMO KWANZA KUMBE "UJINGA KWANZA!!!!!
    WATOTO WA MJINI (SOKOINE NA NYERERE) WALISEMA SIASA NI KILIMO NA KILIMO NDO UTI WA MGONGO WETU WA TZ NA KWA UJINGA WENU KAMA HAKUNA ANAE KUMBUKA (KILA MKOA ULIKUWA NA NATIONAL MILLING, VIWANDA VYA KANDA, KAMPUNI ZA USAFIRI WA ABIRIA NA MIZIGO.... NA MIFUMO CHUNGU NZIMA!! KWENYE KILIMO KULIKUWA NA THE BIG FOUR (4) RUKWA, RUVUMA,IRINGA NA MBEYA!!! AKIBA YA CHAKULA HAISHI!!! SASA LEO TUNA VIONGOZI KAMA WAJAWAZITO NA HAWAJIFUNGUI!!!

    ReplyDelete
  13. Mimi nimechoka na nyie watazania mnaomsifia Nyerere, mara Nyrere hiki mara Nyerere kile...Yes nakubali Nyerere hakuwa fisadi, kwa hilo nampongeza. Lakni Tanzania iko hapo ilipo kwa sababu yake, hao viongozi wengi walianza kazi wakati Nyerere. Mbona hakufanya kitu chochote? Nani alikuwa anamjua Benjamini Mkapa kabla ya 1995, na Nyerere ndio alimteua na watanzania mkampigia kura. Na ndio fisadi namba moja...

    ReplyDelete
  14. poleni sana watanzania wenzagu.kila kitu hakuna uhakika nacho.umeme shida,maji shida ,hospitali hakuna, elimu mbovu,hebu wananchi tufanyeni kitu kimoja.tufanye michango ya wazi kama alivyofanya katibu mkuu wa nishati na madini JAIRO katika wizara zote harafu tupate mitambo mipya wakati tunasubiri maji.

    ReplyDelete
  15. tuweke mikakati ya kuwakatia nao umeme hakuna kutibiwa india,hakuna safari za nje kwa viongozi.na manunuzi ya magari ya kifahari kwa serikali.lakini pia wanapoenda huko nje hujifunnza nini?mbona huko hawako kama sisi?la kikwete hata wakere wenzio wanakuponda.wapwani wenzio wamezoea hata umpe shilingi 10 atakusifia sasa watu wa bara hawataki pwapwa zako

    ReplyDelete
  16. Mi nadhani tufurahie tu maana tumewachagua juzi tu na tulikuwa tunawajua kuwa hawana jipya. Sasa kelele za nini. Hureeeee ccm endeleeni kutekeleza sera zenu za kunufaisha wateule.

    ReplyDelete
  17. WaTanzania wenzangu poleni na giza, kusema ukweli inasikitisha sana. Lakini naona tunapopata matatizo vile vile tunapata akili za kutatua shida zetu.Na mie namsuport jamaa hapo juu, Simon, anaposema kutatua tatizo letu inabidi tuwatupe Tanesco na serikali. Tutumie solar,wind,hydro,makaa ya mawe,natural gas,uranium. Jua na upepo hupo tele bongo.

    ReplyDelete
  18. Sokoine Cousin:

    Kwa taarifa yenu nyie wananchi msio na ADABU..... hii ni kwa WA TZ wenye ADABU TU ndio wanaelewa.... NYERERE NA SOKOINE WALIKUWA NA KITU KINAITWA "UNDERSTANDING OF DISCIPLINE WITH GOOD PERSONALITY".....MWINYI, MKAPA,BONGO FLAVOR (MRISHO) hawana na UNDERSTANDING OF DISCIPLINE WITH GOOD PERSONALITY!!!!!

    Omary Kapera( Nyerere) alipomkosa Omary Chogo (SOKOINE) ambae alikuwa very 1st choice, akamwomba Salim Ahmed Salim awe Rais wa TZ but to no avail coz of high-stupidity ya upemba na uunguja! then, akaona bora achukue SCRAPPER (mwinyi) na 1995 wakati Nyerere(Omary Kapera) yu hai aliwakataa MZINZI (MALECHELA) MWIZI(LOWASSA)NA BUM(MRISHO)akamchukuwa his former student (Mkapa) but refer the above statement u boy!!! alisema huyu kijana sio mkamilifu but atawasaidia!


    u BOY UKIWA understanding utanielewa why every disciplined tznian shud n't 4get Omary Kapera (Nyerere) na Sokoine(Omary Chogo)

    but KAMA NYERERE alishiriki ktk kifo cha Omary Chogo (Sokoine) BASI hii dhambi kubwa kuliko hata dhambi ya ASILI (this only for Christians esp. RC's) kila M-TZ anaiishi!!

    Sorry, kama ulikuwa uelewi vitu hivyi!

    And 4 ur information....

    Kama Omary Chogo (SOKOINE) angekuwa hai.....i can tell u....Usingemsikia REJECT (MWINYI),WATER MELON(MKAPA)WALA BUM (MRISHO)....... na tusingekutana na huu UPUMBAVU wa sasa... nadhani nimekusaidia kuhusu (Omary Kapera(Nyerere na Omary Chogo (SOKOINE)

    uLIZA SWALI JINGINE...!!! BUT USISAHAU KUWAONESHA WENZAKO MANENO HAYA if at ol they can afford to...... they are very, very expensive....cost yake exceeds that of space shuttle Atlantis -sts-135...hahahahhaaa cheersss boooy!!!

    ReplyDelete
  19. sokoine cousin? cjakupata what? Nyerere alishiriki kumuua Soikoine? how? wakati wewe mwenyewe umesema that Sokoine was Nyerere's No1 choice, iweje tena amuue? come again bro

    ReplyDelete
  20. Sokoine Cousin:

    Huwezi kunipata coz bado unakwenda mpirani, unashabikia ligi ya wajawazito ya UK...Ulipiga kura....siasa zilikuwa kabla ya Omary Kapera (Nyerere) haja ng'atuka (1985) na kabla hatujampoteza Omary Chogo (SOKOINE) na mpira uliisha rasmi 1975 (Mseto bingwa) wakati huo Aluu Ally, Hussein Ngulungu, Omary Hussein, Ndululu, mnyepe, shilingi, shiwa lyambiko wanacheza...... ndo wewe na watz wenzako hamuezi kunipata!! Ngumu sana kunipata mimi.....unaenda kupiga kuchagua ngadu au nge wakuongoze? unaende mpirani kuona bongo flavor? Tulikwenda mpirani, kupiga kura coz tulikuwa na furaha ya Nyerere na Sokoine.... hivi unajua kwamba msafara wa Sokoine ulipokuwa ukikaribia bungeni mawaziri wote na wabunge wote wanakimbilia ndani kama watoto wa chekechea????

    Sorry u'll never get along wt me!!! Mpira hauko UK kwenye timu za wajawazito (lIVERPUL,CHELSEA,ARSENAL,MANCHESTER) ungepata kuangalia ligi za uturuki, russia, bundesliga(real human being) paraguay, uruguay, mexico, colombia, chile......na mpira wa TZ wa miaka ya 1960's - 1970's.....USINGEPOTEZA muda wako M-TZ!!!! WAT's more boy??

    ReplyDelete
  21. Unajua ukiona mitoto ilikosa adabu ndo maana walishindwa kumsaidia nyerere.....we engineer wa UDSM amesomeshwa abroad miaka 5 hadi 7...anakuja kutengeneza mashine ya kienyeji ya matofali na juice? wazima hao watoto? unataka Omary Kapera(Nyerere) na Omary Chogo(Sokoine) wafanyaje???? mashine za matofali na juice zipo gerezani nzuri zaidi ya zile za wadudu waaribifu(UDSM) .....
    SOKOINE COUSIN:


    Nakuomba uelewe tu kwamba TZ imebaki yatima kwa hiyo ile mikaka yetu mikubwa (mwizi-Lowassa, nnge-Chenge, bum-mrisho, tikiti-maji-mkapa, scrapper-mwinyi....ndo wametufisha hapa tulipo... kama huwezi kunielewa hapo.......i can tell you HAUTAMUELEWA MTU YEYOTE YULE!!

    ReplyDelete
  22. KHA SOKUINE COUSIN umeongea maneno mazito sana lakini hamna namna...ni vyema CHUPI ikaendelea kuitwa CHUPI na sio NGUO YA NDANI....hapa ndio dawa itapatikana na sio kuremba remba...

    Tanzania ilipoteza dira miaka hiyo tangia succession toka kwa nyerere...... na hii ni kwamba alifikiri kuwa kundi lake tu ndio sahihi kuliko kila mtu....akakabidhi nchi kwa WAMELO ..... kweli hapa tulipofika ni SOO!! tushatafakati sasa tuchukue hatua.....

    ReplyDelete
  23. Umenikumbusha mbali Mjomba SOKOINE COUSIN sasa tunafungwa magoli ya penalt, penalt ya kwaza Giza, hizo penalts zingine nini? na huku tanasherekea miaka Hamsini ya uhuru. sasa kamampigaji ni SEMBULI nyavu zitapona kweli?

    ReplyDelete
  24. Sokoine Cousin;

    Mayb 4 ur information tu.....kuwa wakati PM - SOKOINE (kassin mwabuda -six ya mkoa wa Tanga) alitoa order ya kumweka into custody waziri wa fedha by then, mwizi mshenzi -Cleopa Msuya.....ilibidi Nyerere amdanganye Sokine na Sokoine alichukia sana, alitaka kuresign......So I can comply wt me kwamba hakuwa mtu kucheze-chezea hivi......LEO HII Msuya akisikia Sokoine amerudi ATAKUFA NA PRESHA HAPO HAPO!!!! AU SOKOINE AJE AANGALIE IKULU PAKOJE SIKU HIZI.... WOTE AKINA BUM (MRISHO) WATAKIMBILIA KIGAMBONI BILA KUJIJUA WAMEVUKAJE PALE FERRY!!!!..... .Tz ilishawahi kuwa na Prime Minister mmoja tu....(EDWARD MORINGE SOKOINE- ONE AND ONLY...!!!!)Ukioondoa wakati Tanganyika ilipokuwa CHINI ya uangalizi wa wazungu pori na wababaishaji (BRITISH).....laiti WAZUNGU WENYEWE -ORIGINAL (THE GERMANS WANGESHINDA THE WORLD WAR -II TUNGEKUWA MBALI MNOOO KIMAENDELEO.... !!!

    Now mayb tuna retired PM's wawili tu (JOSEPH SINDE WARIOBA NA SALIM AHMED SALIM)...Sasa huwezi hata siku moja kuni-convice Cleopa Msuya,Sumaye na mporaji na mwizi mashuhuri (LOWASSA); eti ni retired PM's....a very, very BIG NO-NO-NO-NOOOO!!!!!!

    Well, cna cha kufanya zaidi ya kuwakumbuka these very, very smart guys!! For watever expense!!


    mmmhhhhh...kama ni wewe kweli mshabiki wa mpira huwezi kumsahau "mpiga penati mashuhuri wa Mseto ya Morogoro(KIWANDA CHA WACHEZA MPIRA) SHIWA LYAMBIKO...Shiwa alipokuwa anapiga penati uwanja mzima walikuwa wanatazama nje ili wasiione mpira unavotinga wavuni....

    Sasa tukirudi kwenye nidhamu SITAACHA KUWATAJA SOKOINE NA NYERERE...... Sokoine ni kama kipa wa zamani wa simba (Hassani Mlapakolo na Nyerere kipa wa zamani wa Yanga (Muhidini Fadhili) au six ya Yanga Abrahman Juma (Nyerere) na Khalid Abeid (Sokoine) six ya Simba!!!

    Kwa umakini zaidi six ya mkoa wa Tanga enzi hizo (KASSIM MWABUDA-SOKOINE) na six ya mkoa wa Dar es salaam (Khalid Abeid)

    kuna wengine wengine tuu Gilbert Mahinya, Mbaraka Jingalao, Hassan Gobbos, Mohamed Msomali (exceptional -COACH), John Lyimo (TPC-MOSHI)......Unajua wakati mwingine tunamwangalia huyu bongo flavor, BUM (Mrisho) then, tunaishia kusema....well, some guys, then unatingisha kichwa tu....!!!I wish tuonane nikueleze mambo ambayo pengine huyajui ama hujawahi kukutana na M-TZ akakueleza real things!!!! enjoy ur day boy!!

    ReplyDelete
  25. Sokoine Cousin;

    Sio KWA SABABU SOKOINE ni my uncle tu..!!Cjui kama umeshapata habari zake vizuri hivyo....Mjomba wangu Sokoine alipofariki chumbani kwake tulikuta kaunda SUTI MBILI (2) zisizo na kola (i.e. kama zile north korea au uchina), misale mbili (2) za waumini(4 christians) ama misaa-afu miwili(2) 4 muslims!! na safari buti boot 2 pairs only!

    Sio kwamba Sokoine alikuwa hajipendi NO u're mistaken boy...!!! Sokoine alikuwa na kitu kinaitwa "SELF-DETACHMENT" (UKINAIFU NA ROHO.....Spirituality..... hahahahaha......nitafute siku moja tuongee boy!!!!!! and in fact Sokoine waz runing beyond Nyerere.....!!!!

    Pengine unapata taabu kunielewa kidogo....mayb let me give a break on this......nakumbuka vizuri Mwenyekiti wa Simba by then, Said El-Maamry na mjumbe FIFA NA CAF alipata wakatu mgumu mnamo mwaka 1973 wakati CAF ilipohitaji kupata majina mawili ya wachezaji wa TZ ambao walitakiwa kujiunga na wenzao kwenye kombaini ya timu ya Africa kwenye mashindano ya mabara. CAF iliitaka TZ one wakati huo OMARY MAHADH BIN JABIR (Kwa kipa kulikuwa hakuna mjadala, Mahadh waz mwaaaah!!! sasa inside ten (no 10) ndo ilikuwa noma....simba kulikuwa na Abdallah Kibaden -Mputa(Nyerere) na Yanga -Maulid Dilunga (Sokoine). Kwa kweli wote ni wazuri sana. Sasa Said El Maamry kwa kuwa alikuwa M/kiti wa Simba akapeleka jina la Kibaden kule CAF-Misri na lile la kipa la Omary Mahadh Bin Jabir;

    kumbuka kwa kipa CAF walinyoosha mikono kwa Omary Mahadh Bin Jabir......sasa CAF waliipoona jina la inside ten (no. 10) sio wanalolitaka ilibidi watafute jezi ya rangi ya njano na kijani wakaipiga picha, then wakaituma TZ kwa FAT....kwenye picha hiyo wakaonesha tunamtaka mchezaji anaechezea timu yenye rangi hizi....njano na kijani (i.e. Yanga) ambae ni MAULID DILLUNGA (SOKOINE) na sio ABDALLAH KIBADEN (NYERERE)......So boy Nyerere na Sokoine wote walikuwa smart-guyz but Sokoine the greatest of both!!!
    hahahaha....just find sometimez to luk for me SOKOINE COUSIN nikueleze vitu ambavyo hujawahi kuvisikia hapa TZ....

    Have a great day boy!!

    ReplyDelete
  26. Tatizo wananchi wa Tanzania hawaonyeshi kama wako katika janga la kitaifa, nasi tubadilike na sherehe zisizo za lazima huo ubadhirifu na israfu mkipewa madaraka mtafanya kama wenzenu maana hulka inaanzia chini angalia sehemu uliko una uadilifu kiasi gani kama kutwa kukicha watu wamejazana baa pesa za kunywa na kutanua wanapata wapi?

    ReplyDelete
  27. sisi kafara hatuna lakusema baba mwizi sembuse mtoto wizi una anzia serikalini mpaka mitaani ngazi ya chini sisi hatuna la kusema la msingi tuuze nchi

    ReplyDelete