28 July 2011

Mlimali wamuaga Profesa Mushi

Na Tumaini Makene

VIONGOZI mbalimbali wa kitaifa, wanazuoni, familia, ndugu na marafiki jana walishindwa kujizuia kuonesha masikitiko na wengine kuangua kilio wakati waliokuwa wakitoa
heshima za mwisho wakati wa kuuaga mwili wa Profesa Samuel Mushi.

Katika heshima hizo zilizoongozwa na Makamu wa Rais, Dkt. Ghalib Mohamed Bilal, Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa, Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye, Prof. Mushi alielezewa kuwa mmoja wataalam wazalendo wa mwanzo kabisa kujiunga na UDSM, mwaka 1967.

Ilielezwa kuwa kwa muda wote aliokitumikia chuo hicho katika
nafasi mbalimbali za kitaaluma na kiutawala, alikuwa mtu aliyetumia uwezo wake wote kuonesha kwa vitendo kuwa wasomi wanapaswa kutumikia jamii.

Prof. Mushi, ambaye ameacha mjane, Mama Felister Mushi, watoto saba na wajukuu 13, alizaliwa Desemba 24, 1939, huko Machame, Kilimanjaro, akijiunga na UDSM tangu mwaka
1967, ambapo alikitumikia kwa utumishi uliotukuka mpaka mauti yalipomkuta Julai 23, mwaka huu, baada ya kupatwa na ugonjwa wa kiharusi.

Akisoma wasifu wake wa hayati, Prof. Gasper Munishi, alisema kuwa hayati Prof. Mushi atabakia kuwa mmoja wa wasomi wachache ambaye waliobaki wanapaswa kujivunia na kujifunza kutoka kwake.

"Siwezi kusoma kila kitu kilichoko katika wasifu wake itachukua muda mrefu maana ni kurasa kumi na nne. Hivyo nimefanya kufupisha...Prof. Mushi atabaki kuwa mmoja wa
wasomi wachache ambao kwa kweli tunakiri kujivunia kutokana na umahiri wake wa hali ya juu," alisema Prof. Munishi.

Mwili wa Hayati Prof. Samuel Stephen Mushi ulilazwa katika makazi yake ya milele huko Bunju, Dar es Salaam, baada ya kupewa heshima za mwisho katika ukumbi wa Nkrumah chuoni hapo.

3 comments:

  1. BARUA YA WAZI KWA WAZIRI WA MAMBO YA NJE:UWEPO WA ASKARI WA JWTZ KATIKA KULINDA AMANI NCHINI LEBANON/DARFUL-SUDAN HAUNA FAIDA.
    NDUGU MHARIRI SISI WANAJESHI WA JWTZ WAKULINDA AMANI NCHINI LEBANON NA DARFUL-SUDAN TUNANYANYASIKA YAPATA MIEZI SITA HATUJALIPWA MISHAHALA YETU TUKIULIZA WAKUU WETU TULIONAO KWENYE OPERESHENI WANATUAMBIA UN HAWANA PESA WAKATI HUOHUO KUNAWANAJESHI WA JWTZ WANAFANYAKAZI YA OBSERVER NCHINI LEBANON NA DARFUL WANALIPWA KILA MWISHO WA MWEZI DOLA 2000 KAMA UN HAINA HELA HIZO ZINAPATIKANA WAPI? PIA TUMEFUNGULIWA AKAUNTI CRDB BANK KWALAZIMA PESA ZETU WANAFANYIA BIASHARA KWANI KILA ASKALI ANALIPWA NA UN DOLA 5000KWA MWEZI LAKINI CHA AJABU NCHI INATULIPA DOLA 800 TU KWAMWEZI.
    JE HII NI HALALI AU DHULUMA? WATANZANI ONENI TUNAVYO DHURUMIWA NA LUTENI GENERALI ABDURAHMAN SHIMBO PAMOJA NA SELIKARI YA TANZANIA. TUNATEGEMEA ASKARI AKIENDA KULINDA AMANI KIDOGO ATAKUWA NA UNAFUU WA MAISHA KAMA MAJESHI YA WENZETU LAKINI TUKIRUDI TUNARUDI NA NJAA.BORA TANZANIA IONDOLEWE KWENYE KULINDA AMANI LEBANON/SUDAN.
    SISI WANAJESHI WA KULINDA AMANI LEBANON NA DARFUL-SUDANI.

    ReplyDelete
  2. BARUA YA WAZI KWA WAZIRI WA ULINZI NA MKUU WA MAJESHI YA ULINZI (JWTZ).

    UWEPO WA ASKARI WA JWTZ KATIKA KULINDA AMANI NCHINI LEBANON/DARFUL-SUDAN HAUNA FAIDA.
    NDUGU MHARIRI SISI WANAJESHI WA JWTZ WAKULINDA AMANI NCHINI LEBANON NA DARFUL-SUDAN TUNANYANYASIKA YAPATA MIEZI SITA HATUJALIPWA MISHAHALA YETU TUKIULIZA WAKUU WETU TULIONAO KWENYE OPERESHENI WANATUAMBIA UN HAWANA PESA WAKATI HUOHUO KUNAWANAJESHI WA JWTZ WANAFANYAKAZI YA OBSERVER NCHINI LEBANON NA DARFUL WANALIPWA KILA MWISHO WA MWEZI DOLA 2000 KAMA UN HAINA HELA HIZO ZINAPATIKANA WAPI? PIA TUMEFUNGULIWA AKAUNTI CRDB BANK KWALAZIMA PESA ZETU WANAFANYIA BIASHARA KWANI KILA ASKALI ANALIPWA NA UN DOLA 5000KWA MWEZI LAKINI CHA AJABU NCHI INATULIPA DOLA 800 TU KWAMWEZI.
    JE HII NI HALALI AU DHULUMA? WATANZANI ONENI TUNAVYO DHURUMIWA NA LUTENI GENERALI ABDURAHMAN SHIMBO PAMOJA NA SELIKARI YA TANZANIA. TUNATEGEMEA ASKARI AKIENDA KULINDA AMANI KIDOGO ATAKUWA NA UNAFUU WA MAISHA KAMA MAJESHI YA WENZETU LAKINI TUKIRUDI TUNARUDI NA NJAA.BORA TANZANIA IONDOLEWE KWENYE KULINDA AMANI LEBANON/SUDAN.
    SISI WANAJESHI WA KULINDA AMANI LEBANON NA DARFUL-SUDANI.

    ReplyDelete
  3. nchi ikiongozwa na manyang'anyau matokeo yake ni manyanyaso kila sekta poleni sana askari wetu . ccm haioni dhuluma hizi kwasababu hatimaye yenyewe ndio inayofaidika na mfumo huu dhalimu wa kuwekana madarakani. njia bora naya uhakika ni sanduku la kura na kuzilinda hadi inag'oka

    ReplyDelete