26 July 2011

Mbunge akerwa Zanzibar kufananishwa na wilaya

Na Godfrey Ismaely, Dodoma

MBUNGE wa Ole Rajab Mbarouk Mohammed (CUF), amemjia juu mbunge wa Geita, Bw. Donald Max (CCM) kwa kuifananisha Zanzibar na wilaya.Wakati akichangia
hotuba ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Bw. Max alisema kuwa wilaya ya Geita ina ofisa kilimo mmoja, wakati wilaya hiyo ni kubwa kuliko Kilwa na Zanzibar.

Baada ya mbunge kumaliza kuchangia hotuba hiyo, Bw. Mohammed, aliomba kutoa taarifa kwa Mwenyekiti wa bunge, Jenista Mhagama akisema kuwa mbunge aliyemaliza kuchangia ameitaja Zanzibar kama wilaya.

“Mheshimiwa Mwenyekiti naomba kutoa taarifa, mchangiaji aliyemaliza ameitaja Zanzibar kama wilaya.

“Naommba kumpa taarifa kuwa Zanzibar ni nchi, ina rais wake, katiba yake na bendera yake…tunataka hili suala likome,” alisema Mohammed.

Akijibu hoja hiyo, Mhangama alisema kuwa taarifa hiyo imezingatiwa na itaingia kwenye hansard kwani inafahamika kuwa Zanzibar ni nchi.

9 comments:

  1. Sawa Zanzibar ni nchi, ila ukubwa wake wa eneo ni ndogo kuliko wilaya iliyotajwa au kufananishwa nayo. Wala siyo kosa kusema hivyo kama kuna sababu ya kupeleka ujumbe ueleweke vyema. Sioni kuna sababu ya kung'aaka kwa kudhania ni kudhalilisha Zanzibar kwani ukweli utabaki vile vile.

    ReplyDelete
  2. ukweli utabaki hiyvo hivyo kuwa zanzibar ni nchi hata mkizalilisha vipi na kama mnajiamini mbona mnang'aga'na kuwa nayo kama vipi nanyi wabara undeni serikali yenu roho mbovu ndo inawasumbuwa

    ReplyDelete
  3. Lugha aliyoitoa mbunge dhidi ya yule aliyesema zanzibar ni sawa na wilaya ninzito na inaonyesha kuna makubwa zaidi ambayo alishindwa kuyasema. Wakati umefika wa kuwa wazi zaidi kuhusu mwungano huu. Watu wote wanajua kinachoendelea lakini hakuna mwenye uwezo wakusema let us be serious on this issue. G55 waliwahi kusema lakini dola ikawadhibiti wako wapi hao? Iokoeni Tanganyika

    ReplyDelete
  4. Nyie nini..hamjui hata historia yenu ..
    Mabaki ya watumwa kutoka bara ndio nyinyi.
    Hao waarabu wa kupepea mnawaona miungu !1
    Vichekesho..nchi haina jeshi wala polisi wake ,,kweli nyie hamna hata haya.. (( mimi mzanzibar bwana )) amkeni wajinga ninyi.Mnayo hela yenu ,,au wabunge wenu wajingawajinga hawadai kuwa na hela ya kizanzibari. wanaona Geita tu ???

    ReplyDelete
  5. bara mnaikalia kimabavu znz kama israel wanavyoikalia kimabavu palestin... kama znz ndogo vunjeni muungano basi mukaungane na kenya au uganda wao ni nchi kubwa, bila znz hamuwezi kujiendesha mafala nyinyi.

    ReplyDelete
  6. hata iwe vipi,hata tukipima kwa tape measure, hata zanzibar ikiwa na rais, pesa yake, majeshi yake, na kila kitu chake, bado itakuwa na udogo wa eneo kuliko wilaya ya Geita! that is a point, huyo mbunge aliyeomba mwongozo hana hoja ila alitaka aonekane kuwa aliomba muongozo

    ReplyDelete
  7. Mh! hili joto limezidi sasa, isitajwe Znz basi ni dhambi, kama vile kuitoa udhu! bora muungano unvunjwe joto liishe

    ReplyDelete
  8. Du.. znz kazi ipo.
    Naomba kuwauliza hawa wajinga wajinga..
    Hivi siku hizi wana(((( PASSPORT))))) za kizanzibari NIELIMISHENI.
    HUENDA NASEMA WAJINGA WAJINGA KUMBE WANASAFIRI KWA PASS ZA UNGUJA.
    WENU: MTOTO WA YESU NA MTUME.

    ReplyDelete
  9. hivi hao wamanga wa znz wamewafanyia nini kikubwa au kwa vile ni waarabu tusiongee !!
    mnajivuna wamewajengea misikiti..mbona basi hawawawekii angalau viti mkaswali kwa raha.

    ReplyDelete