Na Godfrey Ismaely, Dodoma
KAMBI ya Upinzani Bungeni imelaani kitendo cha serikali kuingia kataba na mwekezaji kutoka Marekani, AGRISOL ENERGY na kumpa ardhi yenye ukubwa wa
ekari 327,755 katika Mkoa wa Ruvuma huku wananchi wakikosa sehemu ya kulima.
Msemaji Mkuu wa kambi hiyo kupitia Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika Bw. Meshark Opulukwa, alieleza hayo jana wakati akiwasilisha hotuba ya kambi hiyo.
Alisema serikali imetoa ardhi hiyo kwa hoja kuwa ataongeza upatikanaji wa chakula na kutengeneza ajira, lakini katika utekelezaji wa suala hilo, wakulima wadogo wapatao 162,000 wataondolewa kwenye maeneo ambayo walikuwa wanalima na kuhamia
kusikoeleweka.
“Kambi ya upinzani hairidhishwi na hoja za uzalishaji chakula na kutengeneza ajira zinazotumiwa na serikali ili kuhalalisha mpango wa kuwapokonya wananchi ardhi yao na kumpa mwekezaji, hoja za kumbeba mwekezaji huyo hazina ukweli wa kutosha;
“Takwimu zilizopo za hali ya chakula zinaonesha kuwa nchi haina tatizo la chakula, ila tatizo kubwa lililopo ni miundombinu mibovu katika maeneo ya uzalishaji mkubwa wa chakula, tatizo la miundombinu ndilo linalosababisha
upungufu wa chakula kwenye maeneo ambayo uzalishaji ni mdogo.
“Hivyo hoja ya serikali kumpa mwekezaji huyo ardhi kwa kisingizio cha kuongeza uzalishaji wa chakula, haina msingi,” alisema Bw. Opulukwa.
Msemaji huyo wa kambi ya upizani alisema iwapo mwekezaji huyo ni muhimu, ingekuwa ni busara akawekeza katika kuimarisha miundombinu mibovu katika mkoa wa Rukwa, ili wakulima na wafanyabiashara waweze kuuza, kununua na kusafirisha
mazao yao kwa urahisi.
Alisema hoja nyingine ya kuongeza mazao yatokanayo na ufugaji inatia shaka, kwani ni dhahiri mwekezaji huyo hajafanya utafiti kuwa Tanzania ni nchi ya tatu kwa kuwa na mifugo mingi na kwamba kuna uwiano kati ya mifugo na idadi ya watu.
Aidha, kambi hiyo imeitaka serikali kuanzisha mamlaka inayojitegema kwa ajili ya kilimo, ili iweze kusimamia sekta hiyo kikamilifu.
Alisema mamlaka hiyo itakuwa na kazi ya kusimamia uzalishaji wa mbegu bora, na za kisasa za kilimo, usimamiaji na usambazaji wa zana za kilimo na kusimamia utumiaji wa teknolojia na zana za kisasa katika kilimo.
Bw.Oporokwa alisema ili kuongeza mchango katika sekta ya kilimo katika uchumi wa nchi, kambi hiyo inaishauri serikali kuwa makini katika kuingia mikataba ya kilimo na wawezekezaji na hasa inayowahusisha wakulima wa mazao.
“Mara nyingi mikataba hiyo inatumiwa vibaya na makampuni na kuwanyima uhuru wakulima kuuza mazao yao eneo lenye bei nzuri,” alisema.
Mheheshimiwa Opokulwa tunaomba usilalamike jambo ambalo hufahamu undani wake: kwanza wananchi waliomo katika eneo ambalo atachukua muwekezaji hawataenda kusikojulikana na wao wanalifahamu hilo, pili hicho chakula unachosema Tanzania kipo kingi kipo wapi? ama umejaza siagi na mafileti kwenye friza zako unadhani kila mtu ndio hivyo? Pia unapenda kuona bei ya vyakula ikipanda kila kukicha? mnapenda kutuona wananchi tukila nyasi msemo wa waheshimiwa wengine? Kwanini asilime mazao yakawa mengi bei za vyakula zikashuka? tafadhali kambi ya upinzani msipende kupinga kila jambo kwa kuwa tu mnaitwa wapinzani, ulizeni TAMISEMI watawaeleza kwa kina na undani wa suala lenyewe na nina imani mtalielewa.
ReplyDeleteNI JAMBO LA KUSIKITISHA KUONA MBUNGE ANAPINGA JAMBO HATA KAMA LINA TIJA ATI KWA KUWA NI MPINZANI. HALAFU KUONGEA BILA KUJUA UNACHOONGELEA NA NI JAMBO LINAHUSU TIJA ZA WANANCHI NI DHAMBI. TANZANIA INA ARDHI KUBWA NA ASILIMIA CHINI YA 25 TU NDIYO INAYOLIMWA. KUNA SOK KUBWA LA CHAKULA NCHI JIRANI NA UTAJIRI WETU UPO KTK KILIMO CHA BAISHARA SI KILIMO CHA KUJIPATIA CHAKULA TU. MAO ALISEMA BILA UATAFITI FUNGA MDOMO WAKO!!
ReplyDeleteKama kuna mtu nafikiri kuwa huyo mwekezaji anakuja kuisaidia nchi juu ya upatikanaji wa chakula basi amepigwa changa la macho. Huyo jamaa anajua kuwa atapata cheap labor tanzania lakini akisha lima kama ni mahindi basi mjue ni kwa ajiuli ya kutengeneza Ethanol! na si kwa ajili ya kuilisha nchi. Kwa kwa bahati mabaya sana nadhani nyie mnaomtetea inawezekana hata mkataba aliofikia na serikali wala hamjui. Kalaga baho!
ReplyDeleteKalagabaho mwenyewe!! wewe ndiye mbinafsi kwelikweli!! hiyo cheap labor tulikuwa nayo? au wewe ni mtoto wa kigogo na kwamba unakusanyaga kodi za walalahoi na kujilimbikizia hivyo huoni tabu ya kukosekana kwa ajira Tanzania. Hiyo ardhi akiitumia muwekezaji na asipoitumia wewe kama wewe utapata nini!! si bora apime kwa wingi chakula kiwepo kwa wingi!!?? na ajira unazoziita cheap labor zikapatikana? tumia akili wewe!!kalagabaho!!
ReplyDeleteAfu wee kalagabaho hujui jinsi viongozi wetu wengi wamejigawia hii nchi yote na wameipiga tu fensi na hawaifanyii chochote bali ni tamaa tuu!!nenda Dodoma Bagamoyo hata Kagera wanamiliki maelfu ya ekari kwa kutumia nyadhifa zao!! bora muwekezaji alime tupate chakula na ajira!!
ReplyDeleteWe mjinga kweli.
ReplyDeleteAnalima na anasafirisha ulaya na marekani auze kwa DOLA. Mjinga wewe--upate chakula toka kwa mzungu ?? una wazimu.Waulize waethiopia .. nao walifanya hivyo miaka iliyopita ,,leo je ? au unarukuia mambo tu ??
we mjinga sawa tu na viongozi wako.
si bora wangekuwa wananunua ardhi, hao wapewa bure mjinga wewe.. na kama ana hela aanze na kuwajengea wanaoishi huko nyumba then awahamishe kwa gharama zake. akifanya hayo.basi uongozane naye makalime hayo mahindi mjinga wewe. huna kwenu ?? mkimbizi nini ?? mbuzi kabisa, bado mtumwa wa hawa nguruwe,,pole mjinga wewe,
wadanganyika ngoja niwakumbushe kitu kimoja muhimu watu kila siku wanaongezeka lakini ardhi haiongezeki leo hii mnaona kuwa mna ardhi kubwa lakini kiukweli baada ya muda fulani ardhi haitotosha jifunzeni kwa nchi zingine nendeni nchi za ulaya mkajionee. ardhi ni kitu cha mwisho duniani kuuziwa wageni maana ndio urithi wa nchi na wana wake, Ni nchi zenye viongozi wajinga na wasioona mbali ndio wanaweza kuuza maziwa ya mama yao kwa vipande vya fedha.
ReplyDeleteTusaidiane kuwaelewesha hawa ngumbalu..
ReplyDeleteWe mtanzaia omba serikali ikupatie hata kiwanja cha banda la kuku ujionee !!
Akawekeze kwa mama yake-- alikotoka hakuna ardhi ..
aende zake huko mjinga tu..mwafrica si yule wa 1780 !! Na shuleni tukafundishwa ujinga eti wavumbuzi wa africa Vasco dagama na wasenge wenzake walikuja kutafuta viungo !!
shiiit, viungo kweli ???
Ujinga unaudhi,
Kuna jamaa hapo juu nilikuwa nahisi ni muendawazimu lakini sasa hivi kwa kusoma hoja zake ndio nimehakikisha kwamba anahitaji msaada wa kufikishwa milembe dodoma kwa ajili ya matibabu ya kichwa, tena anahitaji huduma ya haraka sana kabla hajaanza kula mavi na kuokota majalalani makombo na vichaa wenzake, nasema hivi kwa sababu yeye tangu jana akilini mwake kunatoka maneno yafuatayo: kalagabaho, mjinga,nguruwe, mtumwa sijui na mengineyo!! kweli kama sio kichaa kabisa huyo unaweza kwenda kwenye cafe kwa ajili ya kwenda kuudhihirisha ukichaa wako mana kichwani pamejaa hayohayo!! pole kaka bora andika namba yako ya simu na akaunti namba watanzaia tukuchangie ukatibiwe kama waginjwa wengine wa kansa, uvimbe, nk.pole sana kwa ugonjwa kaka yetu.
ReplyDeleteNdugu mhariri hawa wanaolaumu mbunge wa Cahdema hawajui wanalozungumza. Mimi ni mtanzania ambaye nipo Ulaya. nimekuwa huku Ujerumani hata wakulima wadogo wanalalamika kwa hilo yanapoingia makampuni makubwa yanaua kabisa wakulima wadogo wadogo wanabaki kama manamba. Hawa wanaotetea mwekezaji hawana uzoefu wowote. Subiri mruhusu huyo mkulima aingie mtaona. Wengi wa watanzania wanashabikia mambo wasiyo yajua au wengine tayari ni mafisadi. Subiri mtakumbuka kauli na Upeo wa Wabunge wa CHADEMA. Wakulima wanaotoka nje wakuja kufanya kitu kinachoitwa Superprofit, nimesoma matatizo ya Uwekezaji haya yameleta shida katika nchi ya Ecuador, Meksico, Brazil na Guatemala. Hawa wanaopinga hoja ya Mbunge wa CHADEMA wanamifano hipi. Nao hawa waliingiza makampuni ya Kigeni wakidhani yataleta neema lakini wengi wamekuwa wakilia kwa makovu hayo. Labda sheria zetu zikiwabana. Lakini kama anaingia bila kupewa sheria yoyote akishaanza kuzalisha huwezi ukamwekea mashariti. Watanzania laleni kwa njozi ya wawekezaji mtaona.
ReplyDeleteKwa nini huo mkataba usiwekwe hadharani kila Mtanzania akausoma na kuutambua kama una manufaa au hauna..
ReplyDeleteHizi tabia za viongozi wetu ku-sign mikataba bila wananchi kujua ukweli wa huo mkataba tuzikatae kwenye katiba mpya..
Kuwe na kipengele ambacho kitaweka wazi kuwa kabla ya mkataba mkubwa unahusu maslahi ya Watanzania kupitishwa, ni lazima uchapishwe kwenye gazeti la serikali japo miezi mitatu kabla ila tuusome na kuuelewa..
Wana-sign ushenzi na kutuambia kuwa na siri eti hatutakiwi kuujua..Tena uwe kwa Kiswahili
Baba wa Taifa alitambua maadui watatu. Moja akiwa ujinga! Na kwa kweli adui huyu anantutesa sana Zimbabwe wakulima weupe walinyanganywa ardhi wakajigawia wakubwa wameiwekea fensi hawalimi na ZIMBABWE ILIYOKUWA NAUZA CHAKULA NJE SASA INAOMBA! Watu mnadhani tutaendelea kungangania ardhi siku zote. Basi tizameni Singapore. Ni City state. Wakulima wachache na watu wana utajiri. Marekani wakulima wanaolisha Marekani na dunia ni pacent tatu tu. Wakilima makampuni makubwa watoto wa wakulima wakashiba wakasoma watafanya mambo mengine si kurejea kwa baba zao kijijini kulima. Na utaona waliosoma hawarejei kijijini kulima! CHADEMA kwa sasa wanaturejesha tulikotoka na tatizo ni UJINGA tu na siasa za kujitafutia umaaruf!!! Very Saad indeed.
ReplyDeleteLa mikataba kuwekwa wazi ,, hilo ni neno..
ReplyDeletehaya yote yasingekuwapo, yanapofanyika na wakajua watu wachache tu ndio inakuwa kero.
pakiwa na uzushi,rais au mawaziri waweke wazi uzushi huo !! la sivyo tunaishia kuamini tu,,
Mkapa an Hoteli kubwa sana SA.
SA wana mkataba wa machimbo miaka 100,
Barozi wa tz sweden ana mradi wa sambuasa
hiyo ni mifano.
kuna msenge mmoja anazungumzia issue yangu,
ReplyDeletewewe kam huna ardhi utajuaje uchungu wake????
mpe ardhi huyo msenge mwenzio mzalishe sana hayo mahindi..
Akikupa debe la mahindi nitaarifu nijipeleke mwenyewe Dodoma.
mjinga wewe unakubali kumpa msenge mwenzio ardhi ya mtanzania
Moani yako mazuri sana kaka kama nakuona umekunja uso kwenye kompiuta ya watu, tehteh!!, unastahili pongezi na kwa jazba uliozo nazo nakupa pole mana mkataba teyari umesainiwa na mimi ni mdau niliyekula pacent kubwa wewe ulie tu au usage chupa ubwiye, la kufanya huna zaidi ya kupepeta matusi kwenye pc za watu!!heheeeee!!sisi tunakula bata wewe endelea kutaabika juani, mana tumeshika mpini umeshikilia makali utafanyaje??ungekuwa hata umesoma ingelikusaidia angalau sasa wewe umesomea matusi endelea kujishibisha matusi hayo mimi nachat nimo kwenye kiyoyozi full kwenye vogi langu. hahaaaa!! kalagabahu masikini utakufa huna damu yote imekauka kwa kutembea juani kila siku you were born to suffer ulishaandikiwa hivyihivyo bear it my bro.
ReplyDeleteWanaogawa ardhi ya watanzania bila kuwauliza watanzania wana fanya dhambi moja kubwa sana waasisi wa taifa hili na wote waliopigania watanzania tuwe huru walitamani kuona watanzania wanajitawala na wanamiliki nchi na uchumi wao. Hawa wanao leta ukoloni kwa kupitia mlango wa nyuma kwa mwamvuli wa uwekezaji wanawatakia watanzania na vizazi vyao vijavyo maisha ya shida milele. Historia inatuonyesha kuwa mtu anajiendeleza mwenyewe na wala hatasiku moja hataendelezwa na mtu wa kutoka nje hawa si wawekezaji kama mnavyosadikishwa bali ni wachumaji wawekezaji ni watanzania wenyewe ambao hata kwenda nje kutafuta ardhi ni ndoto isiyoweza kuwezekana
ReplyDelete