05 July 2011

Five Stars yajipanga upya

Na Frank Balile

BENDI ya muziki wa taarab ya Five Stars ambayo ilipotelewa na wasanii wake katika ajali iliyotea Mikumi mkoani Morogoro, imeanza kujipanga upya.Bendi hiyo
ilipotelewa na wasanii wake zaidi ya saba, wakiwemo wafanyakazi wengine katika ajali iliyokea Machi 21, mwaka huu na kusababisha vifo vya watu 13.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kiongozi wa bendi hiyo, Ally Juma 'Ally J', alisema tayari wamepata vyombo vya muziki, hivyo wataingia kambini katika ukumbi wa Panandipanandi Ilala, kesho.

“Tumepata vyombo vya muziki, hivyo tumepanga kuingia kambini kesho kujifua kwa ajili ya kuwapa burudani wapenzi wetu baada ya kuondokewa na wasanii wetu katika ajali ya gari,” alisema.

Ally J, ambaye ni mpiga kinanda wa bendi hiyo, alisema katika jitihada zao za kujiimarisha wamefanikiwa kuwapata waimbaji na wapiga vyombo wapya ambao wataanza mazoezi kesho.

Aliwataja waimbaji wapya ni Mussa Ally ambaye ni mdogo wake marehemu Issa Kijoto, Isha Mashauzi na Mariam Mohamed, wakati Maproo Mzubia (gita la solo) na Juma Hamis (bess).

Wasanii waliofariki katika ajali hiyo ni Kijoti, Omary Hashim, Tizo Mgunda, Ramadhan Gili, Sheba Juma, Hamisa Omary na said Omary.


Ally J, alisema kuwa, wasanii wengine wanaotaka kujiunga na kundi hilo, wataanza kusailiwa Alhamisi katika ukumbi huo huo.

No comments:

Post a Comment