Na Zahoro Mlanzi
SAA chache baada ya kumalizika kwa mchezo wa mwisho wa Kundi A wa mashindano ya Kagame Castle Cup, Kocha Mkuu wa timu ya Simba, Moses Basena, amelilalamikia
Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu kwa Nchi za Afrika Mashariki na Kati (CECAFA,) kwa kuipendelea Yanga kuipa siku tatu za kupumzika.
Simba imemaliza kundi hilo ikiwa kinara kwa kufikisha pointi nane mbele ya Red Sea na Vital 'O, ambapo itaumana na Bunamwaya katika mchezo wa robo fainali kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, leo.
Basena aliyazungumza hayo baada ya kumalizika kwa mchezo kati ya timu yake na Red Sea juzi jijini Dar es Salaam, ambapo alisema kuwa, CECAFA haijawatendea haki kwa kuwa wamepewa siku mbili za kupumzika.
"Kwanini timu nyingine, mfano Yanga imepewa siku tatu za kupumzika, lakini sisi ni siku mbili, wao watakuwa na faida ya kupumzika na kujiandaa vizuri, tofauti na sisi," alilalamika Basena.
Pamoja na hayo, alisema katika mchezo huo, wachezaji wake walikosa umakini na ndio maana walitoka suluhu, kwani walishindwa kuzitumia nafasi nyingi walizopata.
"Wachezaji wengi nimejaribu kufuatilia, wanacheza na mashabiki, wakati mwingine badala ya kupiga mpira na kutafuta nafasi, anasubiri kushangiliwa, hicho kilituponza katika mchezo huo," alisema Basena.
Alipoulizwa swali kuhusu matokeo hayo, yanaonekana kama walikula njama ili waitoe Ocean View, wakati walikuwa na uwezo wa kuifunga timu hiyo, alisema tuhuma hizo si za kweli na huo ni mchezo na lolote linaweza kutokea.
"Nadhani umeona mwenyewe, tulipata nafasi nyingi, lakini hatukuwa na bahati na pia ieleweke hakuna timu katika mashindano hayo unaweza ukapanga kuifunga mabao mengi na hilo likatimia, kila timu ni bingwa wa nchi alipotoka," alisema Basena.
MFA MAJI HAACHI KUTAPATAPA, RATIBA ILISHAPANGWA HATA KABLA MICHEZO HAIJAANZA NA SASA JE, YANGA WANGETAKIWA WACHEZE LEO WAO KESHO WANGEDAI KUWA NAO WAMEPENDELEWA? CHEZESHA MBINU ZA MPIRA USITOE MANENO YA KUANZA KUJIHAMI!!UZALENDO HAMNA MMEWEZA KULA NJAMA YA KUWATOA NDUGU ZETU OCEAN VIEW
ReplyDeleteNA LEO NDIO MNAAGA RASMI NA SABABU ZA KUFUNGWA LEO UMESHAZITOWA USIBADILISHE MANENO HAYO YANATOSHA KWAHERI MNYAMA WA MJINI
Basena ana Matatizo yake ameshindwa kupanga timu yake anatafuta visingizio kwanni muda huu si muda wa timu kujipanga. ni kufanya kile mlichokiandaa awali ilo ndo tatizo la Makocha wa Kiswahili Badala apange mikakati ya kufanya Vizuri anaangalia Yanga Kama anataka kuwa kocha wa yanga aseme ila bahati mbaya hana kiwango cha kuifundisha yanga yeye abaki tu na Mgosi. Namshauri akitaki afanikiwa abuni mbinu zake si kuangalia ya Yanga Yanga Haiwezi tu . Naomba Mtumieni Basena Hii Msg
ReplyDeleteBy Damian . Arusha
Basena hana mpango kabisa tena amekula rushwa toka red sea ili kupanga matokeo ya sare waiondoshe ocean view,nawe mwisho wako umefika,kama sio leo basi mechi hijayo. ''dust to dust''
ReplyDeleteMangara