26 July 2011

Cocain ya mil. 700 yabambwa Tanga

Stella Aron na Masau Bwire

POLISI Mkoa wa Tanga kwa kushirikiana na Kikosi Maalumu cha Kupambana na Dawa za Kulevya, kimekamata dawa za kulevya aina ya Cocaine zenye thamani ya
sh. milioni 700 ndani ya basi Raha leo na Tawaqal.

Dawa hizo zilikamatwa katika matukio mawili tofauti baada ya Kikosi cha Kupamba na Dawa za Kulenya kuwatilia shaka watuhumiwa hao.

Kwa mujibu wa Mkuu Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga, Bw. Jafary Mohamed, watu saba wanashikiliwa katika matikio hayo.

Alisema kuwa tukio la kwanza lilitokea Jumamosi ndani ya basi la Raha Leo katika eneo la Kabuku ambapo polisi iliwakamata watuhumiwa watatu wakiwa na kilo 12 za Cocain.

Kukamatwa kwa dawa hizo kutokana na mtego uliowekwa na kikosi hicho kwa kuwatilia shaka baadhi ya watu akiwemo mfanyabiashara mwenye asili ya Kiasia mkazi wa Magomeni, Dar es Salaam.

Mkuu huyo wa upelelezi alisema mfanyabiashara huyo alikamatwa Jumamosi saa 5:30 asubuhi, katika kizuizi cha Polisi Tanga baada ya kupekuliwa na kukutwa na baadhi ya dawa kwenye mfuko.

Alisema kuwa kikosi hicho, kilifuatilia nyendo za mfanyabiashara huyo ambaye alionekana katika Kituo Kikuu cha cha Mabasi Tanga na akimkabidhi mkazi mmoja wa Pongwe begi lililokuwa na dawa na kupanda basi la Raha Leo lililokuwa likitoka Mombasa kwenda Dar es Salaam.

Mfanyabiashara huyo alianza safari akiwa nyuma ya basi hilo akiwa kwenye gari ndogo aina ya Baloon.

Hata hivyo, basi hilo lilikamatwa baada ya kufika kwenye mizani ya Tanga na katika upekuzi walibaini kuwepo kwa dawa hizo kwenye begi.

Alisema mfanyabiashara huyo alikamatwa akiwa na mifuko mikubwa 12 ya dawa za kulevya.

"Ni mapema kuwataja majina yao kwa kuwa bado kuna watuhumiwa wengine tunaendelea kuwatafuta kutokana na kushiriki kwenye uuzaji na usambazaji wa dawa hizo," alisema Bw. Mohamed.

Alisema katika tukio la pili, jeshi hilo linawashikilia watuhumiwa wanne wakisafirisha dawa za kulevya kwenye basi la Tawaqal kutoka Dar es Salaam kwenda Mombasa.

Alisema watuhumiwa hao walikamatwa na kilo tatu na mara baada ya kukamilika kwa upelelezi watafikishwa mahakamani.

3 comments:

  1. polisi asante kazi meifanya

    ReplyDelete
  2. Waandishi mantuchanganya na uandishi wa habari zenu usiokuwa makini. kwanini mnatofautiana kwenye habari moja na gazeti la uhuru La jana? huko yameandikwa hata majina ya watuhumiwa wote. Pia hakuna basi la raha leo lanalosafiri Mombasa. Basi liliokamatwa lilitokea Tanga
    Hata hivyo tunawashukuru kwa kutupa habari hiyo ingawaje ni kwa ujumla; na tunalipongeza sana jeshi la polisi kwa kazi yao

    ReplyDelete