04 July 2011

CCM kuanika mafanikio yake Alhamisi

Na Benjamin Masese

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimejipanga kujibu mapigo kwa kuanika mafanikio yake yote tangu kuundwa kwake Julai 7 mwaka 1977, katika maadhimisho ya miaka 34 ya
chama hicho Alhamisi ijayo ili kuondoa kauli potofu kuwa 'hakuna kilichofanywa na utawala wake'.

Akizungumza na wandishi wa habari Dar es Salaam jana, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi (NEC) Bw. Nape Nnauye, alisema CCM itafanya hivyo kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania Bara.

Alisema baadhi ya watu wamekuwa wakipotosha ukweli na kuwadanganya Watanzania kuwa katika miaka hiyo 50 hakuna kizuri kilichofanywa na CCM iliyotokana na Chama cha Tanzania Afrika National Union (TANU) iliyounda mwaka 1954.

Alisema CCM imeamua kufanya shughuli hizo kwa kutumia kaulimbiu ya 'uhuru na kazi' iliyowahi kutolewa na Baba wa Taifa, Marehemu Mwalimu Julius Nyerere, siku ya mkesha wa uhuru wa Tanganyika mwaka 1961.

Alisema kauli hiyo iliwataka wananchi kujiandaa kufanya kazi kwa bidii ili kujiletea maendeleo yao wenyewe na nchi kwa ujumla na kwamba CCM inaendelea kufanya shughuli za jamii hadi siku hiyo ya maadhimisho.

Bw. Nnauye alisema maadhimisho hayo ya mwaka huu yatafanyika nchi nzima kuanzia ngazi ya matawi hadi mkoa na kufanya shughuli mbalimbali kama usafi wa mazingira, kusaidia ujenzi, kupanda miti na kutembelea wagonjwa hospitalini.

Alisema usiku wa kuamkia Julai 7, vijana wa CCM nchi nzima watakutana maeneo mbalimbali kufanya shamrashamra za kuashiria kuzaliwa kwa TANU ambapo asubuhi watashiriki katika matamasha na kujadili masuala yenye faida kwa kata, wilaya, mkoa na kitaifa kwa ujumla.

Alisema katika majadiliano hayo watakumbushana mafanikio yaliyopatikana ndani ya kipindi cha miaka 50 kwa kila wilaya na mkoa.

"Sherehe hizi zitaanza usiku wa Julai 6 kwa vijana wa CCM kutoka sehemu mbalimbali kukutana na kusherehekea ikiwa ni pamoja na kufyatua mafataki saa sita usiku kama ishara ya kuzaliwa TANU.

Kwa mkoa wa Dar es Salaam, Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete atashirikiana na vijana na kukutana na mabalozi wa nyumba 10 na kuzungumza nao," alisema.

Alisema watu wanaobeza kuwa hakuna mabadiliko ndani ya miaka ya uhuru wa Tanzania 50 wanatakiwa kufikiria kwanza na kusoma historia kabla ya kuzungumza kwa kuwa historia itawahukumu.

Alisema wanatakiwa kujadili hali iliyokwepo wakati nchi inapata uhuru na kufananisha hali ilivyo sasa katika sekta za barabara hususan za lami, vyuo vikuu, hospitali, viwanda, maendeleo, nyumba, elimu na vitu vingine.

Alisema Julai 7, itakuwa mwisho wa kauli za watu hao kwa kuwa mafanikio yote yataelezwa kwa kila wilaya, mkoa na taifa kwa ujumla.

6 comments:

  1. Mafanikio makubwa ya CCM katika Miaka 50 ya kupata UHURU ni kufanikiwa kwako kutuweka GIZANI katika karne hii ya sayansi na teknolojia. Hongereni sana CCM.

    ReplyDelete
  2. uhuru na kazi maana yake nini wakati kazi zenyewe hazipo ? uhuru na kazi utatoka wapi kwani hata umeme hakuna nchi ipo gizani? acheni kutudanganya.

    ReplyDelete
  3. CCM mmefanikiwa katika sula zima la ufisadi. Wenye CHAMA mmefanikiwa kujitajirisha kupitia ufisadi wenu ili hali wananch wengi tunaishi chini ya dola moja. Madhambi ya CCM ni kama ifuatavyo:

    1)Kukwapua hela BOT kupitia Kagoda
    2)Ufisadi kupitia makampuni ya MEREMETA, DEP GREEN and TANGOLD
    3)Mikataba ya kinyonyaji na yenye mizengwe kama IPTL, RICHMOND, DOWANS
    4) uuzaji wa rasilimali za nchi kifisadi MIGODI YA MADINI, NBC, LOLIONDO to mention but a few
    5) Mkapa na washirika wake kumiliki mgodi wa KIWIRA kifisadi
    6) Kunyamzazia ufisadi wa RADAR ulifanywa na Andrew Chenge na kina Mkapa
    7) Wizi wa kura katika chaguzi mbalimbali
    8) Wizi wa EPA
    9) Ufisadi kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii (Rostam anahusika hapa na Mkapa)
    10)Ufisadi bungeni. Spika Makinda kuminya mijadala yenye maslahi kwa taifa
    11)Kuua raia wasio na hatia
    12) Kunyamazia uharibu wa mazingira uliofanywa na Barick Mto Tigite ambapo watu na mifugo iliathiriwa vibaya
    13) Kutunyima haki wananchi kupata katika yenye maslahi kwa taifa
    14) Matumizi mabaya ya fedha za serikali. Magari ya kifahari na safari nyingi za raisi nje ya nchi zisizo na tija kwa taifa
    15) Kutokuwajibika kwa viongozi waandamizi serikalini. mmeshindwa kudhibiti uchakachuaji wa petrol mpaka mkaamua kuwaumiza walalahoi kwa kupandisha kodi ktk kerosene

    Hayo ni baadhi tu ya madhambi ya serikali ya awmu ya nne. Haistahili kwa namna yeyote kuendelea kuwepo madarakani

    ReplyDelete
  4. Katika kuazimisha miaka 50 ya uhuru ni vyema kuwakumbuka waislam waliomuweka Nyerere baba wa kanisa leo madarakani kama ifuatavyo:
    1.Marehem muft Hassan bin Amir
    2.Sulemani Takadiri kiongozi wa baraza la Wazee wa TANU
    3.Tewa Saidi
    4.Hamza Azizi
    Dosa Azizi
    Bititi Mohamed alimwambia Nyerere yeye anamuogopa mungu tu
    Fimbo Mtwana pamoja na kuenzi nchango wa mzee wetu Bilali Heran Waikela-Tabora
    haya ni baadhi tu ya majina tunatakiwa kuyakumbuka hususani waislam wa Tanzania, miaka 50 ya uhuru mfumo kristo umetawala nchi hii hivyo ni vema tukajipanga kuona haki inatendeka. Nyerere amewaumiza sana babu na bibi zetu lakin mungu ndiye muamuzi.Tukumbuke pia ndg zetu waliouawa na serikali ya kafiri Mkapa, B huko mwembe chai hili nalo ni miaka 50 ya uhuru.Mimi nasema kama mashirika ya kutetea haki za binadamu yamesaidia Sudan ikagawanywa kwa misingi ya dini tunaomba na sisi watanzania tugawane nchi hii ili kila mtu awe na uhuru wa kufanya mambo kulingana na imani yake ya dini, wagala mle nguruwe ewnu kwa nafasi na sisi tule halua zet kwa nafasi ktk kuadhimisha miaka 50 ya uhuru.WAISLAM WENZANGU KUWENI MACHO KTK MIAKA HII 50 YA MFUMO KRISTO TANZANIA.

    ReplyDelete
  5. Nawashauri waandishi wa habari msiandike habari za chama cha mafisadi-ccm cha waropokaji akina Nape.Zinatia kichefu chefu ukikumbuka ufisadi wanaoufanya wa mali za Taifa letu. Acheni gazeti lao la kifisadi pia-uhuru ambalo wanalolisoma ni mafisadi na watoto wao wajiandikie hayo mafanikio ya rushwa,wizi,uzembe,utapeli kwa wananchi. Tunawasubiri kwa hamu 2015 wapumzishwe. wengine waswekwe gerezani maana lazima wafuatiliwe na kufunguliwa mashitaka

    ReplyDelete
  6. Mtoa maoni wapili kutoka chini naona bora unyamaze tu kama hauna maoni ya maana ya kutoa.Maana naona wewe unashawishi udini tu.
    Hakuna hata chamaana unachojaribu kuelezea.

    ReplyDelete